MIJI 10 HATARI ZAIDI BARANI AFRIKA

Amani ni muhimu, lakini baadhi ya miji husifika kwa sifa za uvunjifu wake. Wacha tuione hii miji kumi

   
      

    Kusafiri katika sehemu mbali mbali Duniani ni jambo la kufurahisha na kustarehesha kwa kujua mengi ikiwemo mila, desturi na tamaduni mbali mbali.

    Lakini ishu hii inaweza kuwa hatari pale ambapo umetembelea moja katika maeneo yanayokuwa matukio mabaya zaidi ya kihalifu.

     Lazima kuwa na tahadhari juu la hili;-

     Hivyo basi;-
    Kwa kutambua umuhimu wa hili, leo nitakuletea miji (MAJIJI) 10 hatari na yenye matukio mabaya zaidi hapa barani Afrika. 

    Hebu pitia ujionee pengine inawezekana ikawa ni  katika miji ambayo unakusudia kwenda hivi karibuni ili uchukue tahadhari mapema...... 


     Na JE? miji iliyomo katika Tanzania yetu imo???


1. Rustenburg (South Africa)
Mji huu uko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Huu ni mji wenye uhalifu zaidi kwa Afrika ya kusini. 

Vurugu za kisiasa, utekaji, ulaghai na kila aina ya uhalifu hufanyika katika jiji hili. Picha ya chini ni muonekano wa baadhi ya sehemu za mji huo.
Houses for Sale and Rent in Rustenburg | Pam Golding Properties


2. Pietermaritzburg (south Africa)
Huu ni mji ambao unashika nafasi ya pili kwa uhalifu nchini Afrika kusini na Afrika kwa ujumla. Wizi wa silaha, ubakaji, Uvunjaji wa majumba, uvutaji wa madawa ya ulevya bila kusahau wizi wa magari n.k

Matukio zaidi ya elfu 14 yaliripotiwa kwa mwaka 2015 na chini ni muonekano wa mji huo.
                                  Starting just outside Pietermaritzburg - Journalism.co.za3. Benghazi (Libya)
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka baada ya kuondoka kwa Muammar Gaddafi vilizuka katika nchi ya Libya hasa katika mji huu wapili kwa ukubwa wa Benghazi. Hivyo mji huu umekuwa ni hatari kwa mashambulio ya kigaidi.

Mbali ya hayo pia uhalifu barabarani, dhulma dhidi ya wanawake hasa ambao ni wageni na wasiovaa hijabu.
                              Libya: more violence to come as groups jockey for control before ...


4. Johannesburg (South Africa)
Huu ni mji mkubwa zaidi Afrika ya kusini na unaokadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 4. Miaka ya karibuni mji huu umekumbwa na kashfa   ya kesi nyingi za uhalifu hasa ubakaji.
        
                                      Johannesburg – The City of Gold - Biker Bravado


5. Durban (South Africa)
     Katika jimbo la Kwazulu Natal huu ndio mji mkubwa zaidi na ni miongoni mwa miji ambayo hutembelewa na watalii wengi kuanzia watalii wa ndani na nje na ni mji ambao upo baharini. 

     Jiji hili hutumiwa zaidi kwa uhalifu unaotokana na uhalifu. Yaani adhabu ya mwizi kutoka kwa raia katika maeneo hayo ni kifo tu. 
                                            Durban City Skyline - Picture of Starlite Aviation Group, Durban ...


6. Lagos (Nigeria)
Katika nchi ya Nigeria huu ndio mji Mkubwa zaidi, lakini pia ifahamike kuwa ni miongoni mwa miji mikubwa zaidi Duniani na bila kusahau Nigeria ndio nchi yenye watu wengi zaidi Afrika. Mji huu unakadiriwa kuwa na ziadi ya watu milioni 21.

Wizi wa kutumia silaha majumbani, madukani, barabarani ni majanga yaliyokithiri sana katika mji muhimu.

Lakini pia ubakaji, unyanyasaji na utekaji nyara ndio vituko vinavyolitikisa zaidi jiji hili. Lakini sambamba na hayo pia majambazi huwapora watu katika maeneo yenye msongamano wa magari barabarani wazi wazi bila kificho.

                                       Lagos Nigeria: What Is There To Love? - Nomad Africa Magazine ...


7. Cape Town (South Africa)
Maarufu kama JIJI LA BANDARI nchini Afrika ya kusini. Ingawa ni mji mkuu kisheria nchini humo lakini umekuwa na kashfa mbaya katika masuala ya uhalifu ulimwenguni. 

Shughuli za madawa ya kulevya, wizi na ujambazi na rushwa ni jambo la kawaida sana. Magenge ya kihalifu yamekuwa tishio zaidi katika nyakati zote usiku na hata mchana.
   
                                            10 Things to Do in the Cape Town City Centre - cometocapetown.com


8. Port Elizabeth (South Africa)
"Windy city" ama tena jiji la Upepo, ni kutokana na mandhari yake ya pwani kuwa na upepo mwanana wa baharini na kulifanya kuwa kivutio kikubwa cha watalii. 

Kama ilivyo baadhi ya miji mingine ya Afrika kusini suala la uhalifu wa barabarani kuwa ni jambo la kawaida basi katika mji huu nao kiwango ni kikubwa sana sambamba na mashambulizi dhidi ya wageni ni asilimia nyingi zaidi.

                                                    Port Elizabeth: Safety, What to Do, and How to Get there


9. Luanda (Angola)
Huu ni mji mkuu katika nchi ya ANGOLA, lakini kuanzia miaka ya 2016 uligubikwa na wimbi la mauwaji ya halaiki, ujambazi uliokithiri , wizi na uporaji na hata ubakaji. Katika baadhi ya maeneo ni hatari zaidi kutembea ukiwa peke yako hasa katika nyakati za usiku.
 
                                                Luanda, capital of Angola, important city, primary port, major ...


10. Nairobi (Kenya)
Wachilia mbali kuwa mji mkuu katika nchi ya Kenya, lakini pia ndo kitovu cha uchumi wa nchi. Lakini ukiachana na hayo ni mji ambao umekumbwa na tuhuma za makosa mengi ya jinai. 

Unyang'anyi wa kutumia silaha, wizi wa majumbani, utekaji nyara na ujambazi ni miongoni mwa kadhia mbaya katika jiji hili ambalo ni kitovu cha uchumi nchini Kenya. Lakini pia tuhuma za ugaidi ni miongoni mwa matukio ambayo ni tishio jiji hili.

                                                   7 Days Tanzania Safari | Starting From Nairobi Kenya

Asante kwa kuwa nasi

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MIJI 10 HATARI ZAIDI BARANI AFRIKA
MIJI 10 HATARI ZAIDI BARANI AFRIKA
Amani ni muhimu, lakini baadhi ya miji husifika kwa sifa za uvunjifu wake. Wacha tuione hii miji kumi
https://1.bp.blogspot.com/-gwUQZZ1-V5Q/X6FN9AsWKrI/AAAAAAAAaAA/hT7S_K__sR8zTRXphWRQQkPMNF3M6D0UACLcBGAsYHQ/w319-h166/avoid-armed-robbery.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-gwUQZZ1-V5Q/X6FN9AsWKrI/AAAAAAAAaAA/hT7S_K__sR8zTRXphWRQQkPMNF3M6D0UACLcBGAsYHQ/s72-w319-c-h166/avoid-armed-robbery.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/05/miji-10-hatari-afrika.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/05/miji-10-hatari-afrika.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content