Huu ni wosia kwa wote walio oa na walio olewa. Mtunze mwenzako wa ndani kwani wa nje hawana shukurani
Mtunze Mkeo BADI, Malaya hana shukuru
Zitunze za ndoa HADDI, Sheria yatuamuru
Shikilia itikadi, ya Mungu usikufuru
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Tunza ndoayo Hamadi,
michepuko inadhuru
Kwa nidhamu na weledi, epuka hao kunguru
Wataka wakufaidi, wakukokee tanuru
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Malaya hana SUUDI, kama mtoza ushuru
Anakufanya mradi, akwendeshe ka SUBARU
Maumivu ukirudi, kama mepigwa sururu
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Wapo wazuri wa BODI, mithili ya mkaguru
Utakapo bisha hodi, mwepesi kukuamuru
Ukiingia hurudi, PIGA ASTAGHAFIRU
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Wengine waliachika, kwa tabia zao mbaya
Kwa miaka na miaka, shauri ya umalaya
Akikwona akutaka, akubebeshe MIWAYA
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Wakikwona una mke, wakutafutia njia
Wakupate wakuteke, mipango yako kuuwa
Wakufanyia makeke, mwisho talaka watoa
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Wakisha kuyavuruga, wanajisweka pembeni
Vigeregere wapiga, wakusema barazani
Wacheka wakikusaga, “MUONENI HAYAWANI”
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Michepuko sio dili, madharaye ni makuu
Hupotosha maadili, kumuudhi alo JUU
Madhara lile na hili, kutwa kushamiri tuu
Siendekeze
malaya, hana mapenzio na wewe.
Wengine malengo yao, kukutumia kimwili
Kwasababu walo nao, kutwa kutafuta mali
Hawakidhi haja zao, wakiwa ndani wawili
Malaya
hana shukuru, zinduka mwana wa kwetu
Wengine wataka pesa, kama hali yako shwari
Vimacho wavipepesa, wakikuona na gari
Lazima vitakutesa, usipokuwa ngangari
Malaya
hana shukuru, zinduka mwana wa kwetu
Mtunze mkeo fundi, wengine wapita njia
Watakuganda ka gundi, kama utawachekea
Usijewapa ushindi, mkeo kumkimbia
Malaya
hana shukuru, zinduka mwana wa kwetu
Shika familia yako, nje kuna mazigazi
Aliye wako ni wako, usimuone BAZAZI
Usitafute ujiko, kwa vijike vya uswazi
Malaya
hana shukuru, zinduka mwana wa kwetu
Shikamana na wakwako, mfundishe na ujuzi
Waache waso mashiko, wafanye ni wapuuzi
Zingatia maandiko, Aloyanena Azizi
Pambana na
hali yako, kwenda ukafika mbali.
Mtunzi;- Saidi Rashidi Bunduki.
Siku;- Jumatatu tarehe 09/10/2017 saa 20:10 usiku.
Ufafanuzi wa baadhi ya
maneno
BADI : jina
la Mtu
HADDI : Mipaka
ya Mwenyezi mungu katika dini
SUUDI : Heri
BODI : Mwili
BAZAZI : Mpumbavu
MIWAYA : UKIMWI
PIGA ASTAGHAFIRU : Muombe
msamaha Mwenyezi Mungu
COMMENTS