Siku moja unaweza ukajisaidia haja ndogo na ukapatwa na mshituko kutokana na rangi yake. Makala hii inaelezea rangi za mkojo na maana zake.
Dondoo za afya
Mifumo yote ya mwili hushirikiana
katika utendaji kazi, hivyo linapotokea tatizo katika mfumo fulani huweza
kuonekana kwa mabadiliko kadhaa ambayo baadhi yake hutokea nje ya mwili.
Mkojo huweza kuwa ni matokeo ya baadhi ya matatizo
yaliyoko mwilini hasa katika mfumo wake. Leo nikudokeza kidogo baadhi ya
mabadiliko ya rangi za mkojo na maana zake.
Usisahau kushuka chini sehemu ya 'COMMENT' na kutuachia maoni yako, pia unaweza kushauri kuwa ni nini tuongeze katika mtiririko wa mada zetu;-
ENDELEA NAYO;-
1. (MKOJO) Mweupe kabisaa
Unakunywa maji mengi kupita kiasi, huenda
ukashauriwa kupunguza kidogo.
2. Njano iliyochanganyika na kijani
Hii rangi ni ya kawaida na inamaanisha kuwa mwili
wako una afya na unakunywa maji kiasi kinachohitajika. Baki hapo hapo.
3. Manjano mpauko
Rangi hii pia ni kawaida, haina kiashiria chochote
cha maradhi.
4. Njano iliyokolea
Hii ni kawaida lakini unashauriwa kuongeza kunywa
maji zaidi
5. Njano inayokaribiana na rangi ya
asali
Rangi hii huashiria kuwa mwili wako hauna maji ya
kutosha, unatakiwa kunywa maji mengi.
6. Rangi ya kahawia
Rangi hii humaanisha kuwa huenda ukawa una matatizo
katika ini lako ama tena huenda una upungufu mkubwa wa maji mwilini.
Unashauriwa kunywa maji ya kutosha lakini pia usisite kumuona daktari.
7. Rangi ya machungwa iliyoiva
Huenda ukawa na upungufu wa maji mwilini, lakini pia
huenda sambamba na uwezekano wa matatizo katika ini au mfuko wa nyongo hivyo
muone daktari.
8. Rangi ya buluu au kijani
Hii huweza kusababishwa na rangi ya chakula, athari
za dawa ama maambukizi ya bakteria. Muone daktari
9. Rangi ya pinki inayokaribia
nyekundu
Kama hujatumia matunda au chakula chenye rangi hiyo basi huenda
kuna damu katika kibofu cha mkojo. Huenda ikawa si ishara mbaya sana ila
inaweza kuwa ishara ya ugonjwa wa figo, matatizo kwenye njia ya mkojo n.k.
Muone daktari
10. Mkojo wenye mapovu
Hueza kusababishwa na matatizo ya figo ama protini
zilizozidi mwilini. Kama tatizo hili likitokea mara kwa mara muone daktari kwa
ushauri.
safi
ReplyDelete