Moja katika magonjwa ya zinaa ambayo yalitikisa sana enzi za nyuma kabla ya kuenea kwa ukimwi. Lakini pia bado yapo (GONORRHEA)
Bila shaka umeshawahi kuusikia ama kuugua ugonjwa huu. Huu ni ugonjwa wa ZINAA ama ugonjwa unaotokana na kujamiiana. Ugonjwa huu husababishwa na bakteria wanaoitwa Neisseria Gonorrhea ambao huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
SABABU
Kama tulivyosema hapo juu kuwa ugonjwa huu huenezwa na bakteria ambao wanakaa katika uke au uume wa mwathirika.
Hivyo sababu yake kubwa ni kufanya mapenzi ambayo si salama. Lakini pia mtoto anaweza kuambukizwa wakati wa kuzaliwa endapo mama atakuwa ameathirika na ugonjwa huu.
DALILI
Inasemekana kuwa nusu ya wanawake walioambukizwa ugonjwa huu hawaoneshi dalili yoyote hivyo ni rahisi sana kumuambukiza mwanaume ambaye atafanya naye mapenzi bila kutumia kinga.
Lakini pamoja na hilo, hizi ni miongoni mwa dalili zake;-
Lakini pamoja na hilo, hizi ni miongoni mwa dalili zake;-
- Maumivu wakati wakati wa kukojoa
- Maumivu sehemu za siri
- Kutoka uchafu sehemu za siri
Jinsi ya kujilinda
- Tumia kinga (condom) wakati wa kujamiiana
- Usishiriki na mwenzawako vifaa vyako vya kufanyia mapenzi mfano sex toys n.k.
- Pima na mwenzi wako kabla ya kukutana
TIBA YAKE
Unashauriwa baada ya kupata maambukizi ya kisonono basi muone daktari haraka iwezekanavyo.
USHAURI
Ingawa kwa sasa ugonjwa huu hautajwi sana lakini unashauriwa kutofanya ngono zembe ili kujikinga na magonjwa mengine hatarishi.
KUMBUKA KUWA KINGA NI BORA KULIKO TIBA
KINGA KUBWA YA UGONJWA HUU NA MAGONJWA MENGINE YA NGONO NI KUACHA ZINAA TU.
Imeandaliwa na Saidi Bunduki kwa msaada wa mtandao
'Pia unaweza kutoa maoni yako hapo chini juu ya Makala zetu za afya kuwa nini unataka tuzungumzie'
MAZINGATIO
KINGA KUBWA YA UGONJWA HUU NA MAGONJWA MENGINE YA NGONO NI KUACHA ZINAA TU.
Imeandaliwa na Saidi Bunduki kwa msaada wa mtandao
'Pia unaweza kutoa maoni yako hapo chini juu ya Makala zetu za afya kuwa nini unataka tuzungumzie'
COMMENTS