ZIARA YANGU YA BONGO

Hii ni ziara ambayo bwana Mudi hatoisahau. Ni pale alipoingia jijini Dar na kupokelewa mapokezi mazuri sana sana

1. Sijui nivue shati?, kwa nilivo na usongo
Niandike hizi beti, liwe wazi langu Gongo
Wacha nipige saluti, Nikupe huu mchongo
NI FARAJA YA MAISHA, ZIARA YANGU YA BONGO

2. Safari Darisalama, sijawahi fikiria
Kinywa kipana nasema, haijawahi tokea
Kukonga wangu mtima, mpaka ninarejea
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

3. Nyundo gonga msumari, niwache nisimulie
Maana hii safari, sijaona mfanowe
Msafiri si kafiri, Nimekiri mtambue
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

4. Myaka tatu na kiasi, tungali twafanya kazi
Na bwana JIMY LUCASI, tokea enzi na enzi
Mungu kafanya wepesi, kujuana wazi wazi
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

5. Akajalia Jalali, guu ingia njiani
Ilikuwa juma pili, mei tatu ISHIRINI (2020)
Nikaepushwa ajali, Nikaingia JIJINI
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

6. Maeneo ya Tabata, Karibu na Segerea
Mwenyeji nikampata, nyumbani nikasogea
Changamoto sikupata, Roho ilinitulia
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

7. Majira yalipofika, tuliketi zungumza
Na wenzangu washirika, Heppy, na dada Eliza
Kaka Doto na MONIKA, LEA nae naeleza
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

8. Walinikirimu sana, ndugu hawa wakarimu
Sijawahi pata ona, Kunipa kubwa nidhamu
Minyama ilyonona, ni zaidi ya karamu
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

9. Walinitembeza Kila, kona kwenye zao sekta
Ofisi kuu ILALA, Kimanga hadi Tabata
Tukicheka, kunywa, kula, na stori tukipata
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

10. Sapraizi ya juu, ni zaidi ya ushindi
Hadi makao makuu,  "KARIBU SHABAN SINDI"
Thamani hii ya juu, kupendwa na langu kundi
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

11. Upendo wa nyota tano, mmenipa "BIG UP"
Ni kwa hii tunzo nono, Yani huduma ya SWAP
Nimekuwa ni mfano, mambo sasa CHAP CHAP
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

12. Niwapeni sifa gani?, God bless you DIA
Kunipa hii nishani, sina cha kuwaambia
Mubarikiwe kazini, Nazidi kuwaombea
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

13. Upendo tudumisheni, Hii zawadi ni tunu
Hwenda siku za mbeleni, nikawa shemeji yenu
Hapo kwa dada fulani, nimeshazama mwenzenu😅
ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA

14. Mimi sio mshairi, nimetunga kwa shauku
Ni mibovu mistari, kama miguu ya kuku
SINDI SHABAN nakiri, imeisha hii luku
ZIARA YANGU YA BONGO, SITOKUJA ISAHAUSahiri limeandikwa kwa ajili ya Mohammed Shaban Sindi

COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: ZIARA YANGU YA BONGO
ZIARA YANGU YA BONGO
Hii ni ziara ambayo bwana Mudi hatoisahau. Ni pale alipoingia jijini Dar na kupokelewa mapokezi mazuri sana sana
https://1.bp.blogspot.com/-Lb4DKN2MIRw/X7JM91dygAI/AAAAAAAAao0/r2ZPIhep9DgzlPK7sT9Er7E7NslwD7iiQCLcBGAsYHQ/s320/dar-es-salaam-sobecki-01.adapt.1900.1.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-Lb4DKN2MIRw/X7JM91dygAI/AAAAAAAAao0/r2ZPIhep9DgzlPK7sT9Er7E7NslwD7iiQCLcBGAsYHQ/s72-c/dar-es-salaam-sobecki-01.adapt.1900.1.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/05/ziara-yangu-ya-bongo.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/05/ziara-yangu-ya-bongo.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content