Hii ni ziara ambayo bwana Mudi hatoisahau. Ni pale alipoingia jijini Dar na kupokelewa mapokezi mazuri sana sana

1. Sijui nivue shati?, kwa nilivo na usongoNiandike hizi beti, liwe wazi langu GongoWacha nipige saluti, Nikupe huu mchongoNI FARAJA YA MAISHA, ZIARA YANGU YA BONGO
2. Safari Darisalama, sijawahi fikiriaKinywa kipana nasema, haijawahi tokeaKukonga wangu mtima, mpaka ninarejeaZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
3. Nyundo gonga msumari, niwache nisimulieMaana hii safari, sijaona mfanoweMsafiri si kafiri, Nimekiri mtambueZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
4. Myaka tatu na kiasi, tungali twafanya kaziNa bwana JIMY LUCASI, tokea enzi na enziMungu kafanya wepesi, kujuana wazi waziZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
5. Akajalia Jalali, guu ingia njianiIlikuwa juma pili, mei tatu ISHIRINI (2020)Nikaepushwa ajali, Nikaingia JIJINIZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
6. Maeneo ya Tabata, Karibu na SegereaMwenyeji nikampata, nyumbani nikasogeaChangamoto sikupata, Roho ilinituliaZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
7. Majira yalipofika, tuliketi zungumzaNa wenzangu washirika, Heppy, na dada ElizaKaka Doto na MONIKA, LEA nae naelezaZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
8. Walinikirimu sana, ndugu hawa wakarimuSijawahi pata ona, Kunipa kubwa nidhamuMinyama ilyonona, ni zaidi ya karamuZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
9. Walinitembeza Kila, kona kwenye zao sektaOfisi kuu ILALA, Kimanga hadi TabataTukicheka, kunywa, kula, na stori tukipataZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
10. Sapraizi ya juu, ni zaidi ya ushindiHadi makao makuu, "KARIBU SHABAN SINDI"Thamani hii ya juu, kupendwa na langu kundiZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
11. Upendo wa nyota tano, mmenipa "BIG UP"Ni kwa hii tunzo nono, Yani huduma ya SWAPNimekuwa ni mfano, mambo sasa CHAP CHAPZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
12. Niwapeni sifa gani?, God bless you DIAKunipa hii nishani, sina cha kuwaambiaMubarikiwe kazini, Nazidi kuwaombeaZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
13. Upendo tudumisheni, Hii zawadi ni tunuHwenda siku za mbeleni, nikawa shemeji yenuHapo kwa dada fulani, nimeshazama mwenzenu😅ZIARA YANGU YA BONGO, NI FARAJA YA MAISHA
14. Mimi sio mshairi, nimetunga kwa shaukuNi mibovu mistari, kama miguu ya kukuSINDI SHABAN nakiri, imeisha hii lukuZIARA YANGU YA BONGO, SITOKUJA ISAHAU
Sahiri limeandikwa kwa ajili ya Mohammed Shaban Sindi
dah hongera mtunzi
ReplyDelete