Watoto wengi utawakuta wana matatizo ya meno kuoza. Unajua tatizo nini? Soma makala hii niliokuandalia
DONDOO ZA AFYA
Katika kipengele chetu cha afya, Leo tutazungumzia kidogo magonjwa ya meno, kwa kitaalamu hujulikana kama (Dental carrie). Ugonjwa huu umegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kuna ule ambao huathiri zaidi MENO na ule ambao huathiri FIZI.
Tunajitahidi kuandika kwa ufupi sana ili tusikuchoshe msomaji wetu. Lakini pia usisahau kushea na mwingine elimu hii, ku comment bila kusahau kutu follow katika mitandao yetu ya kijamii kama vile
1. Ugonywa wa meno kuoza
Huu ni ugonjwa unao sababishwa na bakteria ambao hula masalia ya chakula hususan vyakula vya sukari. Asidi ambayo hutolewa kutokana na bakteria ambao huozesha meno. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 60 - 90 ya watoto wa shule duniani wana tatizo la kuoza meno. Lakini kwa Tanzania watoto wenye umri kati ya 4 - 6 mmoja kati ya watoto watatu husumbuliwa na tatizo hili.
Chanzo kikuu cha ugonjwa huu ni vyakula vyenye sukari nyingi hasa kwa watoto mfano wa biskuti, pipi, chokoleti, soda kashata, aisikrimu, ubuyu wenye sukari n.k.
2. Ugonjwa wa fizi
Huu ni ugonjwa unaotokana na uambukizi na unaathiri fizi, mifupa na misuli inayoshikilia jino kwenye taya. Kutopiga mswaki kwa ufasaha ambapo husababisha kuwepo kwa utando laini ambao hujishikiza kwenye meno na hivyo kuruhusu vijidudu vya bakteria vinavyoishi kwenye kinywa kuzalisha kuzalisha sumu ambayo huathiri fizi.
Baadhi ya vitu vinavyoathiri fizi ni pamoja na
· Uvutaji wa sigara
· Mabadiliko ya homoni kwa wanawake
· Ugonjwa wa kisukari
· Magonjwa Mengine kwa mfano Saratani na UKIMWI
DALILI ZAKE
1. Fizi kuvimba ama kuonekana katika rangi nyekundu
2. Maumivu kwenye fizi na kutoa damu
3. Kuhisi maumivu wakati wa kutafuna chakula
ANGALIZO
Ni vema kuchua tahadhari mapema na kujiepusha na visababishi vya magonjwa haya ambavyo tumevieleza hapo juu ikiwemo kuacha kula vyakula vya sukari kwa watoto sambamba na kuachakuvuta sigara kwa watu wazima.
keep it up bunduki....see you at the top
ReplyDelete