BABA RUDI UNIVIKE

Unaweza kuondokewa na mtu muhimu na mambo yako kuyumba ukatamani bora arudi. Mtunzi anamlilia mmoja katika watu wake muhimu

Nimesema visikike, angalau kwa umbali
Kwa wanaume na wake, ali ala kulli hali
Tangu baba uondoke, sinae wa kujadili
Baba rudi univike, medondosha sarawili

Umekwenda wapi baba? Mbona hujaniarifu
Mwana usawa wakaba, nalala kwenye sakafu
Nani atakae ziba, pengo lako takatifu
Baba rudi univike, medondosha sarawili

Tulipanga mengi hasa, tutekeleze mi nawe
Si maswala ya siasa, ni mambo yetu mi nawe
Leo nimeshakukosa, uliko unielewe
Baba rudi univike, medondosha sarawili

Umekwenda wapi faza, miji yote sikuoni
Si Dodoma wala mwanza, kote haupatikani
Mwanao ninakuwaza, nijekutia machoni
Baba rudi univike, medondosha sarawili.

Fikira zinapishana, IBUN ni kwa babae
Mebaki moyo wanena, sina wakusema nae
Majanga yamepandana, sasa nani nimwambie?
Rudi lau mara moja, nikunong’oneze kitu.

Ulimwengu ni mzito, bora mlima sayuni
Ulimwengu ni wamoto, bora maji ya kunguni
Ulimwengu ni mkato, wera wembe wa dukani
Rudi lau mara moja, nikunong’oneze kitu.

Yapo mengi majaribu, yalonizidi umuri
Kila siku naharibu, sijafanyha jambo zuri
asa naona aibu, kama lopata sifuri
Rudi lau mara moja, nikunong’oneze kitu.

Baba wapi umekwenda? Nikupe namba za simu
Unitafute huenda, nipunguze yangu hamu
Kama upo GENDA GENDA, nimuagize ADAMU
Rudi lau mara moja, nikunong’oneze kitu.

Nalia bila machozi, ni siri ya moyo wangu
Naficha hisia hizi, wasijue walimwengu
Hata kwenye usingizi, nakuota ndugu yangu
Rudi tupange mipango, tuendeshe jambo letu.


(tar 17.04.2017 – jumatatu saa 9:20 usiku wa manane)

NA; SAIDI BUNDUKI

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: BABA RUDI UNIVIKE
BABA RUDI UNIVIKE
Unaweza kuondokewa na mtu muhimu na mambo yako kuyumba ukatamani bora arudi. Mtunzi anamlilia mmoja katika watu wake muhimu
https://1.bp.blogspot.com/-IIipIJ16VAE/X7JF9VYI27I/AAAAAAAAaoE/tHY5zsGPXpQeGaMQAGSzvjd6GgT2HqAYgCLcBGAsYHQ/s320/95830012-silhouette-of-business-man-sitting-alone-sad-and-serious-male-sit-and-hug-his-knee-alone-of-closeing.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-IIipIJ16VAE/X7JF9VYI27I/AAAAAAAAaoE/tHY5zsGPXpQeGaMQAGSzvjd6GgT2HqAYgCLcBGAsYHQ/s72-c/95830012-silhouette-of-business-man-sitting-alone-sad-and-serious-male-sit-and-hug-his-knee-alone-of-closeing.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/06/baba-rudi-univike.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/06/baba-rudi-univike.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content