Jamaa anamuimbia mke wake ambaye anarudi nyumbani baada ya kukorofishana na kuondoka kwa muda mrefu
Mshkaji yupo wima, kukuona warejea
Kuiona yake nyama, baada ya kupotea
Japo walinisakama, mwisho wake
wakanywea
Niombee kwa karima, upendo wetu udumu
Nimezichoka drama, walimwengu walizua
Walisema ya kusema, ila hukuwasikia
Nyumba ile nimehama, mtaa nimesogea
Niombee kwa karima, upendo wetu udumu
Karibu hapa ni kwako, wakukutoa hakuna
Na hao visokonoko, wabaki kujitafuna
Wambie hapa ni mwiko, hii meli ya
wachina
Niombee kwa karima, upendo wetu udumu
Fanya vyote uniteke, Nileweshe mi
nilewe
Na waseme waropoke, usisikie mayowe
Kama kuongeza mke, nitakuongeza wewe
Niombee kwa karima, upendo wetu udumu
Zidisha wivu mamii, nafasi hii nakupa
Mimi ndo wako dadii, usikudunde mshipa
Akijileta masii , Vunja mtu nitalipa
Niombee kwa karima, upendo wetu udumu
Tumuombe Maulana, upendo wetu udumu
Tuweze kushikamana, kwa raha na hali
ngumu
Usiku hata mchana, wanga wasituhujumu
Hapa kwako umefika, ringa, vimba
jishauwe
Ringa, vimba jishauwe,kwangu wewe ni
mshindi
Waache hao nguruwe, watashindia mahindi
Wala wasikusumbuwe, Mumeo ni MUDI SINDI
Wewe ndio mama lao, nami ndio baba lao
By: Mohammed S Shaban
COMMENTS