Fanya mazoezi kila siku ili kujenga afya yako na uishi maisha marefu na ya amani zaidi
Mtu mwingine anaposikia neno 'mazoezi' huona kuwa ni jambo la watu maalum tu, lakini hapana kila mtu anahaki ya kufanya mazoezi kila siku kulingana na mtindo wake maisha. Lakini pia unaweza ukawa unafanya kazi ambazo zenyewe ni mazoezi tosha bila kujijua (ni vizuri)
Hapa nimejitahidi kukufahamisha faida za kufanya mazoezi, ili kama katika maisha yako hufanyi mazoezi basi anza leo. Na pia nimekuwekea njia kadhaa za mazoezi kwa mtu
Twende sawa
Maoni yako tunayahitaji zaidi katika sehemu ya Comment - chini kabisa ya post hii, usisahau kutuandikia utakuwa umetisha sana.
HIZI NI FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI
1. Kudhibiti uzito wa mwili
2. Kuzuia magonjwa yasioambukiza
3.
Kupunguza presha
4.
Kusaidia mfumo wa kupumua
5.
Kutengeneza misuli yenye nguvu
6.
Afya ya akili
7.
Kupata usingizi murua
8.
Kujiepusha na baadhi ya tabia mbovu
9.
Kutibu mishipa ya nguvu za kiume
10.
Kumsaidia mama mjaimzito kuwa na nguvu
11.
Kuondoa sumu mwilini na kudhibiti joto
12.
Kudhibiti cholestrol
13.
Kuboresha afya ya ngozi]
14.
kutokupata saratani kwa urahisi
15.
Kuondoa mfadhaiko (stress)
16.
Kuondoa homa ndogo ndogo mwilini
17.
Kuongeza hamu ya kula
18.
Kuongeza uwezo wa ubunifu
19.
Hukomaza mifupa
20.
Kutopatwa na kisukari kwa wepesi
Namna bora ya kufanya mazoezi kwa mtu wa kawaida.
Inatakiwa angalau ndani ya dakika 30 kwa siku hasa kwa mtu anayeanza na kisha anaweza kuongeza mpaka dakika 60 (saa 1). Pia inatakiwa angalau isiwe chini ya mara 3 ndani ya wiki moja.
Si lazima kwenda gym, unaweza kufanya mazoezi rahisi yafuatayo
- Kutembea kwa mguu walau kwa muda wa dakika hizo kila siku
- Kupanda ngazi katika majengo marefu badala ya kutumia lift
- Kufanya baadhi ya shughuli za nyumbani mbali mbali ikiwezekana utoke jasho
- Kucheza mpira
- Kuruka Kamba
- Kupiga Pusha up (Angalau 30 kwa siku)
- Kukimbia
- Kuchuchumaa na kuinama kwa muda mrefu
- Kunyanyua vitu vizito n.k
COMMENTS