Husda (al-hiqd) ziko aina mbili;
1. Husda nzuri
2. Husda mbaya
1. Husda nzuri ni ile ambayo umemuona mwenzio amejaaliwa neema ya mali na elimu ukatamani nawe uwe kama yeye. Haya ni mambo ya kupendekezeka kwani ni kujitamania mazuri ya Akhera. Hadithi ifuatayo inaelezea aina hii ya husda:
Kutoka kwa Abu Sa'iyd ambaye amesema: "Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna husda isipokuwa kwa mawili; mtu aliyepewa na Allaah Qur-aan akawa anaisoma nyakati za usiku na nyakati za mchana akasema [huyo mtu anayemhusudu] “Allaah Angelinipa na mimi mfano alivyopewa fulani ningelifanya kama anavyofanya”. Na mtu aliyepewa mali na Allaah akawa anaipa haki yake kwa kuitoa akasema huyo mtu, “Allaah Angelinipa kama alivyopewa fulani ningelifanya kama anavyofanya”)) [Ahmad na wengineo kwa usimulizi mwengine]
عن أبي سعيد قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :((لا حسد إلا في اثنتين : رجل آتاه الله القرآن فهو يتلوه آناء الليل وآناء النهار , فيقول الرجل : لو آتاني الله مثل ما آتى فلانا فعلت مثل ما يفعل , ورجل آتاه الله مالا فهو ينفقه في حقه فيقول الرجل : لو آتاني الله مثل ما آتى فلانا فعلت مثل ما يفعل)). أحمد
Hivyo husda kama hii haimdhuru mtu na wala mtu mwenye kuhusudu kwa kutamani kupata neema kisha afanye mema hapati dhambi kuwa na husda kama hiyo.
2. Ama husda isiyopasa mtu kuwa nayo kwa nduguye Muislamu ni ile iitwayo 'al-hiqdil-haqiyqiy' (husda ya kweli) nayo ni kuwa na chuki na kutamani neema aliyonayo mwenzio imuondoke na makatazo hayo tumepata mafunzo yake kama ifuatavyo:
2. Ama husda isiyopasa mtu kuwa nayo kwa nduguye Muislamu ni ile iitwayo 'al-hiqdil-haqiyqiy' (husda ya kweli) nayo ni kuwa na chuki na kutamani neema aliyonayo mwenzio imuondoke na makatazo hayo tumepata mafunzo yake kama ifuatavyo:
((Wala msitamani alichowafadhili Allaah baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika waliovichuma, na wanawake wana fungu katika waliovichuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu)) [An-Nisaa: 32]
(( وَلاَ تَتَمَنَّوْاْ مَا فَضَّلَ اللّهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَى بَعْضٍ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُواْ وَلِلنِّسَاء نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ وَاسْأَلُواْ اللّهَ مِن
ALLAAH NDIYE MJUZI ZAIDI
COMMENTS