BISMILLAAHIR RAHMAANIR RAHIIM
Leo ni siku ya Ijumaa, ni sikukuu kwa muislamu na ni siku bora kuliko siku zote za wiki.
Kutokana na ubora wake, Allaah ameweka ibada nyingi ambazo ni suna na ni muhimu kufanyika katika siku hii. Leo nitakutajia chache ambazo nitafanikiwa Inshaallaah.
Kuoga kwa ajili ya swala ya ijumaa
Kuvaa nguo nyeupe
Kupaka manukato (Pafyumu)
Kusoma surat AL KAHFI (SURA YA 18)
Kunyoa nywele na kukata kucha
Kuwatembela na kuwatazama wagonjwa
Kuwahi msikitini
Kumswalia Mtume Muhammad Swallallaahu Alaihi Wasallam kwa kusema "Allaahuma swali alaa Muhammad, Yaa Rabbi swalli alaihi wasallim" Kadiri ya uwezo wako.
Hizi ni chache katika nyingi, Hivyo tunausiana kuwa tujitahidi kudumu na sunna hizi katika siku kama ya leo.
Unaweza kuorodhesha sunna nyingine hapo katika Komment sehemu ya chini.
Asante na Mungu akubariki.
COMMENTS