NITAONGEA NA NANI?

Nani anaweza akatunza siri zangu ili niongee naye?


Nitaongea Na Nani? Nimpe Yanonisibu
Siri Zangu Za Moyoni, Awe Ana Ziratibu
Kwa Ukweli Simuoni, Wote Wana Majaribu
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Na Mimi Ni Mwanadamu, Yako Yanayoniuma
Huwa Nakuwa Na Hamu, Vikwazo Vyangu Kusema
Nimwambie Nani Humu, Atae Nitunza Jama
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Ni Mengi Yananikwaza, Moyo Umejaa Kutu
Nalia Na Kunyamaza, Moyo Wa Mtu Msitu
Sauti Nataka Paza, Ila Naogopa Watu
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Mambo Mengi Yaniliza, Zaidi Ya Hamsini
Mchana Kwangu Ni Kiza, Sina Raha Maishani
Mengi Yananiumiza, Mwaminifu Simuoni
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Nimuamini Fulani?, Ila Yule Domo Kaya
Zitafika Mtaani, Na Siri Zangu Ni Mbaya
Nimwambie Wa Pembeni?, Huyu Naye Hana Haya
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Nimwambie Huyu Bwana?, Huyu Ana Kisirani
Siku Tukiparangana, Atamwaga Vyote Chini
Huyu Sio Muungwana, Tanitia Hatiani
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Nimwambie Yule Pale? Yule Kajawa Dharau
Simmwagie Mchele, Leo Kesho Kasahau
Mwanzo Wa Ngoma Ni Lele, Mwisho Apindua Dau
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Nimpe Nani Za Moyo? Siri Zangu Awe Nazo
Kila Nimwonae Siyo, Kubeba Hana Uwezo
Nabaki Piga Miayo, Najiongeza Mawazo
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Moyo Wangu Waniuma, Umejawa Taharuki
Mengi Yananisakama, Tena Ni Mengi Lukuki
Naenda Mikono Nyuma,Kichwa Chini Hakitoki
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Kila Mtu Anawaza, Ila Mengine Puuo
Mawazo Yanaumiza, Usikie Kwa Wenzio
Mwenzenu Yananiliza, Najikaza Ki Chanuo
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Moyo Wangu Ni Mgumu, Zaidi Ya Mwamba Geu
Mambo Yaliyomo Humu, Nyingi Ni Sitosahau
Nataka Punguza Sumu, Nitulie Angalau
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Ya Rabbi Nafsi Yangu, Naijutia Kwakweli
Yale Ya Tangu Na Tangu, Ni Mengi Na Nishafeli
Muumba Watu Na Mbingu, Nipoze Ewe Jalali
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Mungu Baba Nisitiri, Walimwengu Hawawezi
Nitunzie Zangu Siri, Nakuomba E Mwenyezi
Unitie Ujasiri, Niuache Na Ushenzi
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?

Nalia Chozi La Maji, La Damu Limesha Goma
Kwa Mannani Nataraji, Kupata Kilichochema
Ni Bahati Si Kipaji, Kwa Haya Niliyosema
Nizungumze  Na Nani, Awezaye Tunza Siri?SAIDI BUNDUKI @ 2018

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: NITAONGEA NA NANI?
NITAONGEA NA NANI?
Nani anaweza akatunza siri zangu ili niongee naye?
https://lh3.googleusercontent.com/-QPjt_bRPrLA/X7JKuCbZS2I/AAAAAAAAaoU/FWxkhjgZoRUByjMLHWEQ3T1EhA4Az1AGACLcBGAsYHQ/w240-h186/image.png
https://lh3.googleusercontent.com/-QPjt_bRPrLA/X7JKuCbZS2I/AAAAAAAAaoU/FWxkhjgZoRUByjMLHWEQ3T1EhA4Az1AGACLcBGAsYHQ/s72-w240-c-h186/image.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/06/nitaongea-na-nani.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/06/nitaongea-na-nani.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content