NJIA 10 NYEPESI ZA KUONDOSHA HASIRA

Jazba haijawahi kumuacha mtu salama. Lakini hapa nimekupa njia za kupunguza na kuiondoa kabisa ili kuepukana na madhara yake ambayo ni makubwa.

Naomba nikukumbushe tu kuwa "Wewe ni wa thamani sana kwetu hasa kwa kitendo hiki cha kiungwana ambacho umekifanya kwa kuacha kazi zako na kutembelea ukurasa wetu huu" 

Tunasema 'Asante sana'

ENDELEA NA SOMO;-

Wahenga walisema "Hasira hasara"

Msemo huu wa wahenga una maana kubwa sana, lakini maana yake huwezi kuiona pale ambapo tayari utakuwa na hasira / Jazba. 

Kitu cha muhimu ni kuufanyia kazi na kuuweka akilini kwa wakati huu ambao una furaha na bashasha kwa kusoma makala hii ambayo itakufanya upunguze stress ulizonazo.

Kwani
Kila mtu hupita katika hali hii, ingawa uwezo wa kuidhibiti hasira hutofautiana baina ya mtu na mtu kutokana na maumbile / Uzito wa jambo husika n.k.

Ni mambo gani husababisha harira / Jazba?

Jibu la swali hili kwa ujumla ni kwamba "Ni vitu vyote ambavyo vinatuzunguka katika maisha ya kila siku. Kinachokufurahisha sasa baadaye kinaweza kukuudhi.

Naogopa tu nisije nikakuudhi kwa maneno mabaya katika makala yangu hii. Nami naahidi ukisoma mpaka mwisho utafurahia.

Tunaposema vitu vinavotuzunguuka ni kama vile watu, wanyama na vinginevyo. Ambavyo vimeambatana na maneno, vitendo, ishara n.k.

Ni yapi madhara yaletwayo na hasira?

Madhara ni mengi, lakini baadhi ya hayo ni kama vile;-

Kuua

Kujiua

Kujeruhi / Kujeruhiwa

Aibu katika jamii

Kuishia jela (Kifungoni)

Kupoteza mali

Kupoteza heshima

Kupoteza watu muhimu mf;- mke/mume, watoto n.k

Kupoteza malengo katika maisha

Magonjwa mbali mbali kama magonjwa ya moyo n.k

Nimeorodhesha kwa ufupi hayo madhara kwa kuamini kuwa yapo wazi na hakuna haja na maelezo ya ziada. 

"Endapo maelezo hayajajitosheleza unaweza kutuambia kupitia sehemu ya COMMENT chini kabisa ya makala hii".
 
Hayo ni baadhi tu ya madhara na matokeo ya Hasira / Jazba kama haikudhibitiwa ipasavyo.

Hapa nakupa njia 10 za kuweza kudhibiti hasira yako

Kama utafuata njia hizi kuna asilimia kubwa ya kuweza kushinda maamuzi yako mabaya ambayo ungeyafanya baada ya kughadhibika.

Lakini pia unaweza kuchagua chache au moja tu ambayo ni nyepesi kwako na kuifanyia kazi

1. Ondoka eneo la tukio

Huenda aliyekusababisha ukakasirika unae hapo, basi jambo la busara kwako wewe ambaye umefanikiwa kusoma makala hii ni kuondoka mahala pale haraka iwezekanavyo.

Kama wote mkichukua uwamuzi huu itapendeza zaidi

2. Nyamaza

Waswahili walinena;- "Akushindae kwa kuongea mshinde kwa kunyamaza"

Wengine wakongeza kuwa "Ulimi huponza kichwa"

Hivyo pale ambapo unaona kuna madhara yanataka kujitokeza hasa kwa kukerana kwa kujibishana, unashauriwa kunyamaza na kukaa kimya kabisa.

Ikiwezekana fuatisha na ushauri namba moja hapo juu.

3. Tumia maji

Ikiwezekana jimwagie maji kichwani /  Oga / Tawadha (kwa muislamu

Katika hadithi za Mtume Muhammad amesema kuwa "Hasira hutokana na shetani, na shetani ameumbwa kwa moto, na moto huzimwa na maji. Hivyo atakapopata hasira mmoja wenu basi na atawadhe"

4. Cheka

Sio kumcheka aliyekukera/kukuudhi bali cheka kwa kujifariji na kuamini kuwa hali ulionayo itapita na ni jambo dogo tu.

5. Hesabu juu kwenda chini (yaani 100 - 1)

Hapa ni pale ambapo umedhamiria kusema / kutenda kitu kibaya kutokana na hasira ulonayo. 

Haijalishi nani amekukera, jipe muda hesabu kuanzi 100 hadi 1 au kuanzia 10 hadi 1 na utakapo maliza hapo huenda ukapata njia nzuri ya kuhukumu jambo ambalo ulitaka kulifanya.

6. Samehe

Njia nzuri ya kusamehe ni kutambua kuwa binadamu wote wana mapungufu. Na unapokuwa na hasira basi chukulia kuwa aliyekuudhi ana mapungufu makubwa zaidi kuliko binadamu wote na wewe ni kama umekalika. Basi utamuona kama mtu asiye na maana na utaepuka hicho kikombe.

7. Shuka chini (Relax)

Hasira humuamrisha mtu kupanda juu, yaani kama amelala basi atakaa, na kama amekaa basi atasimama n.k

Sasa kama ukijazibika ni vema ukashuka chini, kama ulisimama basi kaa, na kama ulikaa basi ikiwezekana lala na u relax (Jiachie mwili wako)

8. Vuta pumzi ndefu

Fanya kama mtu anayefanya mazoezi ya yoga, vuta pumzi ndefu mara kadhaa utaona pole pole unaanza kushuka na kurudi kawaida.

9. Fanya mazoezi

Ukiachana na mazoezi wakati wa hasira, ila ni muhimu pia kujihusisha na mazoezi walau kwa uchache katika maisha yetu. Hii husaidia sana kupunguza sumu nying mwilini ambazo husababisha kuzidi kwa hasira pale unapokerwa.

10. Soma maandiko

Vema kama utaweza kusoma maandiko ya dini yako. Hii ni njia ya kupata mazingatio na ni njia kubwa huenda kuliko zote hapo juu. 

Kama itashindikana basi tafuta sehemu tulivu na soma vitabu vyovyote hakika utakuwa sawa na kila kitu kitakwenda kama ipasavyo.

N.B
Kuna watu ambao wamekuwa na ugonjwa wa hasira nyingi sana kiasi cha kupelekea kutokujitambua wakati huo.

Ushauri kwa watu hawa ni vema kuonana na wataalamu wa afya huenda hawako sawa ki maumbile.

Asante sana kwa kuwa nasi
Naomba usikasirike kwa kukuchukulia mda wako.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: NJIA 10 NYEPESI ZA KUONDOSHA HASIRA
NJIA 10 NYEPESI ZA KUONDOSHA HASIRA
Jazba haijawahi kumuacha mtu salama. Lakini hapa nimekupa njia za kupunguza na kuiondoa kabisa ili kuepukana na madhara yake ambayo ni makubwa.
https://1.bp.blogspot.com/-Uxal99MMWUk/XyEsVbyIUYI/AAAAAAAAW2o/RO2TZ3vXzFI7-ngxkgXPukaunr7jm-OhwCLcBGAsYHQ/s320/Anger-Management-Counselling.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-Uxal99MMWUk/XyEsVbyIUYI/AAAAAAAAW2o/RO2TZ3vXzFI7-ngxkgXPukaunr7jm-OhwCLcBGAsYHQ/s72-c/Anger-Management-Counselling.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/06/trachoma-disease-ugonjwa-wa-macho.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/06/trachoma-disease-ugonjwa-wa-macho.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content