Kuna wakati unaweza kuwa katika mahusiano na mtu ambaye humpendi. (Ikumbuke tu kuwa hii ni kazi ya sanaa lakini)

Penzi pendezo la moyo, kwa uliye mkhiyariMoyo
usemapo ndiyo, na mwili huwa tayariKwa
jumla yote hayo, ndio pendo hutabiriila
wewe sikupendi, na wala huna kasoro Nimechora kwenye jiwe, hakuna nilichopataLiwalo
basi naliwe. Nilichoka kukuotaUlinipa
nini wewe, mpaka nikakufata?ila
wewe sikupendi, na wala huna kasoro Mejikuta nakutaka, siku isiyo na saaHeti
swaga zikashuka, kwako? Laa laa laaNikakuona
wacheka, hukutaka kukataaila
wewe sikupendi, na wala huna kasoro Ukenda kwa zako shoga, haraka kunitangaza“Jama
niwape m boga?, tayari kunitangazaYule
nilo mtakaga, leo amenitongozaila
wewe sikupendi, na wala huna kasoro Ulinipa nini dada, nashindwa kutafakariNafikiri
kila muda, hwenda ikawa SIHIRIKweli
mapenzi uroda, ila hii ni shubiriila
wewe sikupendi, na wala huna kasoro Tuwapo ndani wawili, hisia sina kabisaNakuona
ka rijali, mpaka pozi nakosaNafanya
kufosi mwili, sije niona KIBISAkwakweli
inaniuma, sina njia ya kufanya
Kizito kitendawili, zaidi ya vya wahengaKichwa
changu chajadili, nahisi machenga chenganikipiga
moja chali, nishapoteza uwingakwakweli
inaniuma, sina njia ya kufanya
Wanipenda ki ukweli, hilo halinaga wasiYasemekana
hulali, nisije nikakuasiLakini
bado najali, upendo kwako nafosikwakweli
inaniuma, sina njia ya kufanya Ukiniona furaha, washindwa hata kusemaManeno
yangu mzaha, karibu uwe kilemaWapenda
yangu fasaha, niendapo uko nyumanaumia
roho yangu, mungu wangu nisamehe Si kwamba wewe m baya, sijawa na mana hiyoSi
kwamba wewe Malaya, si mtu wa mambo hayoSi
maharage ya MBEYA, kuiva pasi mboyoyonaumia
roho yangu, mungu wangu nisamehe Uko radhi nile mimi , wewe ulale na njaaU
radhi upigwe ngumi, unilinde mimi “daa”Yote
tisa ila kumi, “wataka witwe mamaanaumia
roho yangu, mungu wangu nisamehe Nakuonea huruma, kwakweli nakuumizaJinsi
ninavokuchuma, ndugu nitakumalizaRoho
yangu yaniuma, bora ungejiongezanaumia
roho yangu, mungu wangu nisamehe Mapenzi ni msawazo, si ya nguvu wala dawaAlama
mlizonazo, angalau ziwe sawaLipatikane
tulizo, kila mtu awe powanaumia
roho yangu, mungu wangu nisamehe Nashindwa kukuambia, ubinadamu ni kaziKila
nikifikiria, siwezi tena siweziIla
moyo waongea, kulikoni kinywa wazinaumia
roho yangu, mungu wangu nisamehe
Najua ni yako
haki, kunipenda si hatiaSi
kama hustahiki, kuwa wangu malikiaIla
mapenzi ashiki, kwako haijatimiaNinajisikia
dhiki, nahisi nakuonea Unahaki msichana, kuwa na umpendaeKupata
mno endana, maishani uwe naeKwa
kuwa umeniona, mimi ndio nikufaeMuombe
Mola jalali, anipe penzi na wewe Sipendi nikusaliti, siijui kesho yanguKwakuwa
mejidhatiti, basi sina budi kwanguTwende
nyumbani kibiti, wajue wazazi wanguNitakuoa
mamii, nikutulize dadaa.
Shairi hili limetungwa na SAIDI. R. BUNDUKI
Siku: alhamisi tar 12/10/2017… huu ni ukumbusho wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Wakati huo anatimiza miaka 28
COMMENTS