Wosia kwa kijana wangu Mohammed S Shaban (Babu Z) Pale alipokuwa anaoa tarehe 4 / 5 / 2018
1. Nne, tano, moja nane, bwanga lachukua jiko
Limechoka masebene, na mambo yaso mashiko
Ubachela na ujane, hivi
sasa kwake mwiko
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
2. Kwanza
fahamu kijana, hii ndowa ni ibada
Thawabu kwa Maulana,
hukuzidishia huda
Sasa wacha uvulana,
mshukuru kila muda
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
3. Mpende
mkeo sasa, wazamani potezea
Acha mambo ya hanasa, hiyo
ni sumu ya ndoa
Huo mpya ukurasa, waulize
wanojua
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
4. Na
waseme wasemao, baki msimamo wako
Waache na mambo yao,
mthamini mke wako
Mke ni kama mwanao, na ndie
mwandani wako
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
5. Ndoa
tamu ni mapenzi, wala sio mabishano
Umpende umuenzi, mpe mazuri
maneno
Mpe mambo ya uswazi,
umkande kama ngano
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
6. Wanawake
ni wazito, kidogo uvumilie
Wana mambo ya kitoto, na
hilo ulitambue
Hilo tu ni kama joto,
lazima akusumbue
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
7. M
bembeleze mtoto, asijutie kwa MUDI
Mpulize manukato, uturi pia
na udi
Na pale penye uzito,
mmuombe MAUJUDI
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
8. Ibada
usisahau, mungu atakuuliza
Umeshaongeza dau, majukumu
umekuza
Wacha marafiki jau, wasije
kukuumiza
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
9. Muepushe
na makundi, watamteka akili
Wako wengi hawapendi,
kuliona jambo hili
Watampaka ufundi, umbea wa
kijahili
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
10. Mpe
haki yake mwana, kwako hakufwata rede
Akitaka kumkuna, mzee amsha
dude
Huyo sio dada bwana,
kafuata mshedede
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
11. Hapo
umesitirika, achana na hao mchwa
Toa haki kwa hakika, kamwe
hutokuja achwa
Akija akichepuka, kung’uta
panga la kichwa
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
12. Kuna
wale mamluki, wapenda kuiba iba
Nyumbani hawabanduki,
wajifanya baba baba
Ukimwona toa nduki,
akisimama ni roba
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
13. Kumbuka
wazazi posho, japo ulonayo robo
Kuna leo kuna kesho,
usijifanye kizibo
Ukiipata korosho,
usilisahau bibo
Oa z bwana mudi, zingatia
mambo haya
14. Nakufunda
ndugu mudi, japo mimi sio kungwi
Nimesema makusudi, sauti
iso na mwangwi
Maneno yangu saidi,ni
machungu kama sungwi
Oa z mwana mudi, zingatia
mambo haya
15. Natia
nanga bandari, geti natia kitasa
Chakufanya ukariri, neno la
hili darasa
Ukiyaona shubiri, mimi
nimesha kuasa
Mungu akuwafikishe, ufunge
ndoa salama
COMMENTS