SAPRAIZ YA KIFO (SEHEMU YA 2)

_____________________
_____________________

ILIPOISHIA

  • Wakati natoka bwenini nikapita karibu na ilipo Ofisi kuu ya Sheikh wetu. Nikasikia sauti nzito ikiniita “SAIDII”…….. Kugeuka nyuma nikaona ni Mzee ananiita,,,, tena kwa jina langu halisi kabisaa

 Nilishtuka na kuogopa sambamba na kuwaza kuwa Mzee jina langu amelijuaje? Hili swali sijabahatika kulipatia jibu Mpaka leo. Nilikwenda na kumsikiliza alichokuwa anahitaji, alitaka nikamuite kinyozi wake.

 MUNGU amhifadhi Sheikh wetu na amuweke mahala pema peponi. (AMEN)

Usisahau kuweka maoni yako katika sehemu ya COMMENT chini kabisa ya makala hii.

****************

ENDELEA........

  •  Tukio la kuangukiwa na nyumba / kibanda tukiwa tumelala fofofo

Baadhi ya walimu walikuwa na mashamba sehemu mbali mbali, hivyo kuna muda walihitajika baadhi ya wanafunzi kwenda kusaidia kazi za shambani.

 Siku moja nilijiunga na msafara wa baadhi ya wanafunzi wenzangu kwa ajili ya kwenda (RAGO) shambani maeneo ya Mkanyageni njia ya kutokea Tanga kuelekea Muheza. 

Kwakuwa shamba lilikuwa lipo mbali, tulipaswa kuchukua akiba ya chakula cha kutosha kwa muda ambao tungekuwepo kule. Hasa ukizingatia kule shambani ni mbali sana na huduma za kijamii kama vile hospitali, migahawa, maduka n.k

 Miongoni mwa mahitaji ambayo mwalimu alikuwa anatuandalia ilikuwa ni pamoja na dawa kwa ajili ya dharura.

Shambani kazi ilikuwa ni nzito sana, hapa ni sehemu ambayo ilinifanya kuwa mkakamavu sana (Japo nilikuwa shupavu kabla)

 Kazi ilikuwa ni palizi (Kupalilia mahindi) ambayo tulikuwa tukianza saa 12 asubuhi mpaka saa tano tunakunywa uji, kasha tunaingia tena shambani mpaka saa nane mchana tunawateuwa watu wawili wanakwenda kupika. Baada ya kula tunapumzika kidogo halafu tunaendelea na kazi mpaka jua kuzama na kurudi kibandani kwa shughuli nyingine.

 Siku ya kwanza kufika shambani tulitengeneza kibanda ambacho tulikitumia kwa shughuli zetu ikiwemo mapishi na malazi.

 Hiki kilikuwa ni kipindi cha mvua nyingi sana kama unavofahamu tena wakati wa palizi (kwa wale wakulima) hasa wakati wa usiku.

 Siku moja tukiwa tumelala (Usiku) fofofo. Nilikuwa kama naota hivi kusikia moja ya nguzo za kibanda zikikatika. Kumbe ulikuwa ni ukweli kabisa kibanda kilikuwa kinatuangukia. Ndani ya sekunde kama thelathini kibanda kile kilituangukia na kutufunia tukiwa tumelala.

 Hakuna ambaye aliwahi kutoka nje, shida ikawa sasa ni namna ya kutoka na wakati huo mwenzetu mmoja tulimsikia akipiga kelele sana kuwa amebanwa na anaumia.

Hofu ilitanda sana hasa pale ambapo tumebanwa na kufukiwa na nyasi za kibanda, na hakuna ambaye aliwahi kutoka nje, kibaya zaidi mwenzetu anapiga kelele anaumia. Aisee niliogopa sana.

ITAENDELEA....................

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SAPRAIZ YA KIFO (SEHEMU YA 2)
SAPRAIZ YA KIFO (SEHEMU YA 2)
https://1.bp.blogspot.com/-17GFynQmDkc/Xz_G_17i6kI/AAAAAAAAXVc/q0ScgyGp1q8Ix1slbKTK3QS1spZwdGs4QCLcBGAsYHQ/w364-h183/mfano%2Bhai.png
https://1.bp.blogspot.com/-17GFynQmDkc/Xz_G_17i6kI/AAAAAAAAXVc/q0ScgyGp1q8Ix1slbKTK3QS1spZwdGs4QCLcBGAsYHQ/s72-w364-c-h183/mfano%2Bhai.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/07/sapraiz-ya-kifo-sehemu-ya-2.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/07/sapraiz-ya-kifo-sehemu-ya-2.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content