SAPRAIZ YA KIFO (SEHEMU YA 1)

                                       

                                       
___________________
___________________
  • Umewahi kuondokewa (kufiwa) na ndugu ama rafiki uliyekuwa unamtegemea?
  • Alikufa katika mazingira gani?
  • Athari gani ya maisha amekuachia ambayo unaikumbuka?
  • Kwanini unatamani uwepo wake mpaka leo?

Katika historia hii ambayo nimeiita "Sapraiz ya Kifo" Nimeeleza sehemu ya maisha yangu ambayo niliondokewa na rafiki wa kweli watatu ambao walikuwa ni mihimili mikubwa sana kwangu.

Endelea nayo ili kujua mazingira ya kuondokewa nao jinsi yalivo niathiri.

Usisahau kuweka maoni yako katika sehemu ya COMMENT chini kabisa ya makala hii.


*_______________*

Baada ya kufeli mtihani kule chuo cha ufundi stadi (VETA) kwa kuchaguliwa fani ambayo sikuipenda (Carpenter) tulijadiliana na baba kuwa anipeleke Madrasa nikaongeze kidogo elimu ya dini nami nilikubaliana naye.

Kuanza maisha mapya Madrasa

Ikumbukwe kuwa huu ulikuwa ni mwaka 2010 mwezi wa kwanza. Baada ya maandalizi kukamilika nilikabidhiwa pale madrasa na nilikabidhiwa kwa kijana mmoja ambaye aliitwa Mohammed Bakari (mwanafunzi)

Utaratibu wao pale ulikuwa hivi, ukishakabidhiwa kwa walimu na taraibu zote kukamilika, unatafutiwa mwanafunzi mwenzako ambaye atakuwa anakuelekeza taratibu ndogo ndogo za pale ili kuzoea maisha ya bwenini n.k

 Siku ya kwanza ilikuwa ni ngumu sana kwani nilifikiria sana kuhusiana na familia yangu niliyoizowea. Kwani pale hakukuwa na yeyote ninaye mfahamu hivyo sikuwa na wakuongea naye.

“Ndugu yangu hapa lazima uwe makini sana, jitahidi kuchunga vitu vyako kwani kuna wizi sana. Usijaribu kugombana na yeyote hata kama atakutukana. Toa taarifa kwa waalimu” Huu ni baadhi ya wosia alonipa bwana Mohammed, kaka yangu ambaye nilikabidhiwa kwake. Kwa muonekano alionekana kunizi umri kidogo kama miaka miwili ama mitatu. Kwamaana kwamba alikuwa ni kijana mwenzangu.

Wanafunzi pale hugawigwa makazi katika mabweni kulingana na makabila. Hasa kwa yale makabila ambayo yalikuwa na watu wengi kama vile wasambaa, warangi, wazigua na wapare. (Mimi ni mzigua)

Kwa asilimia zaidi ya 90 muda ambao watu walikuwa free lugha ambayo ilikuwa hutumika ni lugha za kikabila. Hivyo pale kwa jamaa zangu walikuwa wakiongea kizigua mwanzo - mwisho.

Kutokana na muonekano wangu, hakuna ambaye alifikiri kuwa nilikuwa naweza kuongea kizigua hasa baada ya kuwatambulisha kuwa natokea Wilaya ya Pangani na sio wilaya ya Handeni watokapo wao. Hii ni kwasababu wilaya ya Pangani iko mwambao wa Pwani, sehemu ambayo wakazi wake wengi hawawezi kuzungumza kizigua.

Siku moja walikuwa wakipiga stori za kuchekesha sana, nilijikaza lakini mwisho wa siku ikabidi nicheke sana.. Jamaa zangu walishituka sana na kutazamana kisha kunitazama kwa pamoja………..........

***************************** 

ENDELEA

Mmoja wao (Shafii) akauliza kwa kizigua “ebwana  kumbe unaelewa kizigua? Nikamwambia ndio bwana naelewa sana na kila mnachoongea naelewa (Nami nilijibu kwa kizigua)

Tangu hapo nami nikawa natumia lugha ya kizigua pale magetoni. Na hapa ndipo ambapo nilipata kuelewa kwa ufasaha zaidi na kuzungumza kizigua.

Msimamo na sheria zilikuwa kali sana pale Madrasa na mkosaji aliadhibiwa vikali bila kuzingatia umri wala elimu yake. Madam ni mwanafunzi basi alipewa alichostahiki. Niliogopa sana pale ambapo niliona watu wakubwa zaidi yangu na wenye elimu kubwa wakiadhibiwa ipasavyo. Ukizingatia mimi nimeondoka kijijini kwetu nikiwa mwalimu leo nami niadhibiwe? Hiyo ilinifanya kuwa na nidhamu sana. Nilijitahidi kutekeleza majukumu yote yaliyowekwa. Hivyo adhabu ambazo nilikutana nazo zilikuwa ni za kawaida na za wote (wakati mwingine)

Miezi kadhaa baadaye nilikuwa tayari nimezoea mazingira yale ingawa bado nilikuwa nakumbuka sana nyumbani hasa Madrasani kwetu ambako nilipapenda sana.

Rafiki zangu walikuwa wakiniliwaza sana hasa kwa stori ambazo zilikuwa zina uhalisia unaofanana na Kijijini kwetu, hasa pale linapokuja suala la DUFU kwa sababu nilikuwa napenda sana.

Moja katika matukio ambayo nilikuwa nafurahia sana ni pale ambapo tulikuwa tukisafiri na kundi kubwa la wanafunzi katika gari la pamoja kwa ajili yak wenda katika maulidi (Hasa nje ya mji wa Tanga)

Sheikh wetu mkuu katika Madrasa ile(ambaye kwa sasa ni marehemu) Hakuwa ananifahamu hata kidogo.

Hii ni kutokana na kutokuwa karibu na wanafunzi wa madarasa ya chini lakini pia wanafunzi walikuwa ni wengi zaidi ya mia sita (600)

Siku moja ilikuwa ni siku ya mapumziko (ALHAMISI) kama ilivyo ada nilijiandaa kwenda mjini kwa ajili ya matembezi na kununua baadhi ya mahitaji binafsi kama vile mboga n.k

Wakati natoka bwenini nikapita karibi na ilipo Ofisi kuu ya Sheikh wetu. Nikasikia sauti nzito ikiniita “SAIDII”…….. Kugeuka nyuma nikaona ni Mzee ananiita,,,, tena kwa jina langu halisi kabisaaa...

Nilishtushwa sana na kitendo kile, imekuaje mzee aniite jina langu fasaha wakati hakuwa akinifahamu hata kidogo? Niliogopa sana......

 ITAENDELEA....................

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SAPRAIZ YA KIFO (SEHEMU YA 1)
SAPRAIZ YA KIFO (SEHEMU YA 1)
https://1.bp.blogspot.com/-l6x1_DNenXM/Xz_G3vKJZ3I/AAAAAAAAXVU/E5aJCT3862Ya42_AIQfvzNDUcJDNseeTgCLcBGAsYHQ/w364-h183/mfano%2Bhai.png
https://1.bp.blogspot.com/-l6x1_DNenXM/Xz_G3vKJZ3I/AAAAAAAAXVU/E5aJCT3862Ya42_AIQfvzNDUcJDNseeTgCLcBGAsYHQ/s72-w364-c-h183/mfano%2Bhai.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/07/suprize-ya-kifo-sehemu-ya-1.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/07/suprize-ya-kifo-sehemu-ya-1.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content