UGONJWA WA INI

Fahamu walau kwa uchache kuhusiana na ugonjwa wa ini

UGONJWA WA HOMA YA INI

Huu ni ugonjwa ambao hushambulia ini na kuathiri utendaji kazi wake. Husababishwa na virus waitwao HEPATITIS VIRUS

Kama tunavofahamu kuwa Moja katika viungo muhimu vilivyo katika mwili wa binadamu ni INI.

Wataalamu wa mambo ya afya wanasema kuwa ini lina kazi zaidi ya 400 lakini kubwa katika hizo ni kuchuja na kuondoa sumu katika damu.

SABABU ZA UGONJWA WA INI
NI MAMBO YAPI HASA HUSABABISHA UGONJWA HUU?
 • Unywaji wa pombe kupitiliza imekuwa ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu, lakini pia sumu katika damu husababisha kuvimba kwa ini na kusindwa kufanya kazi ipasavyo na husababisha ugonjwa huu ambao kwa kitaalamu huitwa HEPATITIS  
 
AINA ZA VIRUSI VYA UGONJWA WA INI
Virusi vya ugonjwa wa Ini vimegawanyika katika aina 5 ambazo ni A, B, C D na E wakati B na C ndivyo huathiri kwa zaidi ya asilimia 95.
 • Homa ya ini ni miongoni mwa magonjwa ambayo huuwa zaidi watu  
kwani zaidi ya watu milioni 2 hufa kwa mwaka kutokana na maradhi haya. 

VIPI UNAWEZA KUAMBUKIZWA UGONJWA WA INI?
Virusi vya homa ya INI husambaa kupitia maji maji ya mwili kama vile Damu, Manii, Mate na maji mengine mwilini. Hivyo basi tunaweza kuona kuwa ugonjwa huu husababishwa kupitia;-
 1. Kujamiiana na mtu mwenye maambukizi bila kutumia kinga
 2. Kutoka kwa mama mwenye maambukizi kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua
 3. Kuongezewa damu ya mtu mwenye maambukizi
 4. Kuchangia baadhi ya vitu na mtu mwenye maambukizi. mfano miswaki, taulo, vitu vyenye ncha kali kama wembe, sindano n.k 

 NI ZIPI DALILI ZA UGONJWA WA INI?
Mara nyingi ugonjwa huu huwa hauna dalili, mtu anaweza kukaa nao kwa muda mrefu bila kujijua huku akiwaambukiza wengine. Lakini baadhi ya dalili zake kwa baadhi ya watu ni pamoja na;-
 • Kupoteza hamu ya kula
 • Mwili kuchoka
 • Kichefuchefu na kutapika
 • Mabadiliko ya mkojo na kuwa rangi nyeusi mfano wa COCACOLA
Pia unaweza kupitia hapa kujua kuhusu mabadiliko ya rangi za mkojo.

Dalili nyingine ni;-
 • Kupungua uzito
 • Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano kama unavoona hapo katika picha ya chini
UGONJWA WA HOMA YA INI (HEPATITIS) : MAMBO MUHIMU KUFAHAMU
Jicho na ngozi ya muathirika

 
NI IPI TIBA YA UGONJWA WA INI
Mpaka sasa ugonjwa huu hauna tiba maalum kwani ini likishafika kiwango cha kuharibika au kupata saratani ya ini basi kifuatacho hapo ni kifo.

Lakini badala yake ipo tiba ya lishe ambayo hufaa kutumia kutokana na tatizo hili kuwa kubwa na kuathiri wa tu wengi.

Hizi ni Natural antibiotics ambazo husaidia kuuwa bakteria na vizus pamoja na kuzipa nguvu kinga za mwili. Lakini pia

 • Huupa nguvu mwili
 • Kuongeza virutubisho na kujenga afya bora
 • Kuondoa magonjwa nyemelezi
Pamoja na ugonjwa huu kuwa hatari kwa watu wote, lakini yako makundi ya watu ambayo yapo katika hatari zaidi kupata maradhi haya.-
 1. Watoto wachanga (walio zaliwa na maambukizi kutoka kwa mama)
 2. Wanaofanya biashara za ngono (kujiuza)
 3. Wanaume wafanyazo mapenzi ya jinsia moja 
 4. Wanaojidunga dawa za kulevya
 5. Mwenye mpenzi mwenye ugonjwa huu
 6. Wanaoishi na mgonjwa wa ini
 7. Wafanyakazi wa huduma za afya

'CHANJO YA UGONJWA WA INI'
Chanjo ya ugonjwa wa ini ni sindano tatu. Yakwanza ni baada ya kupimwa, ya pili ni baada ya mwezi mmoja na ya tatu ni baada ya miezi sita.

Ni muhimu zaidi kuwapatia chanjo watu hawa-
 • Watumiaji wa madawa ya kulevya
 • Watoto wote
 • Ambao wamefanya mapenzi na mtu zaidi ya mmoja ndani ya kipindi cha miezi 6
 • Wenye maradhi ya kudumu ya ini
 • Wafanya biashara ya ngono
 • Wanaoishi na waathirika
 • Lakini pia chanjo ni muhimu kwa watu wote. Kwani hatujui ni nani kati yetu ameathirika

TANBIHI / UZINDUSHI
Virusi vya ugonjwa wa ini vina uwezo wa kukaa nje ya mwili kwa zaidi ya siku saba vikiwa bado na uwezo wa kumuambukiza mtu mwingine. Hata vikiwa vimekauka mfano kama ni damu au maji maji katika nguo. 

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: UGONJWA WA INI
UGONJWA WA INI
Fahamu walau kwa uchache kuhusiana na ugonjwa wa ini
https://1.bp.blogspot.com/-jZkwRBu1zdc/XwICx2Cz0UI/AAAAAAAAVzc/fu9JOHozznAB3iCSoWK6vo_9reZnd0GEwCK4BGAsYHg/w400-h158/CpZYutMWEAA3lJh.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-jZkwRBu1zdc/XwICx2Cz0UI/AAAAAAAAVzc/fu9JOHozznAB3iCSoWK6vo_9reZnd0GEwCK4BGAsYHg/s72-w400-c-h158/CpZYutMWEAA3lJh.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/07/ugonjwa-wa-ini.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/07/ugonjwa-wa-ini.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content