Kuna baadhi ya matukio ambayo ukiyakumbuka yanaleta kicheko na furaha ingawa wakati huo ilikuwa ni huzuni. Leo nakugusia kidogo kisa cha wizi wa machungwa.
Wakati naishi Pangani mjini, miaka kadhaa iliyopita tulikuwa na kawaida ya kwenda shamba kwa mjomba wetu ambaye alikuwa anaishi huko. Kule shambani kunaitwa MNAZI MMOJA. Kwa kawaida huwa tunaondoka siku ya ijumaa jioni na kurudi siku ya jumapili kwa maandalizi ya shule.
Siku hiyo wenzangu walitangulia siku ya ijumaa, mimi kutokana na shughuli zangu binafsi ikanibidi niende siku ya jumamosi.
Nilipofika karibu na shambani nilikutana na kijana
mwenzangu ambaye yeye anakaa kule kule Shambani, alikuwa ametumwa dukani kununua unga, hivyo
aliomba tuende wote kisha turudi wote.
Wakati tunarudi tulipita katika shamba moja na kukuta kifungu kikubwa cha machungwa na kuanza kuyatamani. Mwenzangu alinisihi kuwa tule machungwa yale kwani mwenye shamba anamfahamu vizuri na ni jamaa yake wa karibu.
Tulianza kuyachakata yale machungwa yawatu kwa kutumia kucha zetu na meno yetu kana kwamba yakwetu vile, (kumbe ni wezi) - mara mwenye shamba huyoo kaingia tena akiwa ameshika kisu mkononi.
Nasikia jamaa anatwambia “Anhaa kumbee nyie ndio wezi wa machungwa yangu ee, mimi kila siku namtafuta mwizi kumbe ndio nyie??” - Ngoja leo niwakomeshe
Tulinyamaza bila kujitetea chochote. Nikamtazama mwenyeji wangu bwana Yahaya kama angejitetea chochote lakini nae alibaki kuwa kimya.
Nikasema hapa leo kazi ipo, Jela itatuhusu
Jamaa aliendelea kusema kuwa sasa itabidi tuyale machungwa yale mpaka tuyamalize yote. Kumbuka kwamba machungwa yale yalikuwa ni zaidi ya 5,000 (elfu tano).
Unajua ilikuwaje?
Itaendelea sehemu ya pili.
USIKOSE
COMMENTS