Nufaika na silaha hizi TANO (5) madhubuti za uandishi ambazo zitamfanya msomaji kupeandezwa na makala zako kila siku

Huu ni muendelezo wa makala inayohusiana na uandishi wa bora wa machapisho.
Pia tunaweza kusema ni
"Njia za uandishi wa makala bora" ama tena
"Mbinu za uandishi wa makala nzuri"
Tulishaeleza njia muhimu mbili katika makala ya kwanza. Kama imekupita unaweza kubonyeza HAPA chini
Maoni yako kwetu ni ya thamani sana, hivyo ni vema baada ya kumaliza kusoma makala hii, shuka chini sehemu ya COMMENT na utuandikie.
ENDELEA........,
Sasa Baada ya
- 1. Kuchagua mada
- 2. Kichwa cha habari
3. ANDIKA CHAPISHO / MAKALA YAKO
Ingawa hii iko wazi. Lakini pia ni muhimu kuzingatia baadhi ya mambo
- Chagua wakati sahihi
Hapa ni kulingana na ratiba zako za kila siku. Huenda una kazi nyingie ambazo ni nje ya uandishi. Kama ndivyo basi angalia muda ambao akili itakuwa imetulia na uko huru.
Itakusaidia kuepuka makosa katika uandishi.
- Chagua sehemu sahihi
Hapa tunazungumzia sehemu sahihi za aina mbili
- Mahala ulipo wakati unaandika
Huwezi vizuri kuandika huku unatembea, unakula, umelala au umesimama. Ni vema kuangalia sehemu sahihi ambayo utakuwa umekaa na umetulia bila bughudha yoyote.
- Programu sahihi
Hii nayo ni miongoni mwa sehemu sahihi kuzingatia kulingana na wewe mwenyewe.
Wengine hupenda kuandika katika baadhi ya Programu kama Microdoft Office n.k
Lakini wengine huandika moja kwa moja katika uwanja wake wa Blogger.
Zote ni sahihi utaangalia wewe ipi ni nzuri kwako

- Jiburudishe
Unaweza kusindikiza kazi yako na moja ya vitu ambavyo unapenda ili usichoke mwili na akili.
Kwa wapenzi wa kahawa, juis, soda, karanga na kadhalika. Weka pembeni yako kiburudisho chako ili uweze kuongeza hamasa wakati wa jambo lako.
Baadhi yao hupenda kusikiliza muziki (Kama hautokuchanganya)
- Zingatia kanuni za uandishi
Msomaji huburidika sana pale anaposoma andiko ambalo limeandikwa kwa lugha fasaha iliyozingatia misingi ya uandishi.
Ni muhimu kuzingatia
- Sentesi (Zisiwe ndefu na zinazochosha)
- Aya (Ziwe fupi fupi)
- Alama mbali mbali kama vile nukta, koma, alama ya kuuliza na kadhalika
- Matumizi ya lugha
(Usichanganye lugha mfano - kiswahili na kiingereza) isipokuwa inapobidi.
Usitumie lugha za matusi
Pia ni vizuri kama utatumia maneno ya kushawishi na kuburudisha na yatakayomfanya msomaji kujiona kama yuko nawe kwa wakati huo.
4. MATUMIZI YA PICHA
Hiki ni kipengele muhimu katika uandishi wa machapisho ya blog.
Lakini itategemea ni jambo gani ambalo unalizungumzia. Kwa baadhi ya machapisho si lazima kuweka picha.
Pale ambapo utalazimika kuweka picha zingatia yafuatayo;-
- Ubora wa picha
Msomaji huchoshwa na picha ambayo haijamvutia kutokana na kutokuwa na ubora.
Hii inaweza kumfanya aache kusoma na kutoka katika blog yako au kutofuatilia tena makala zako.
- Uhusiano wa picha na mada
Haiwezekani mada yako inazungumzia ugonjwa wa MALARIA halafu unaweka picha za michuano ya ligi za UEFA.
- Tumia picha kama kielelezo
Huenda unatueleza kuhusiana na Ziara yako ambayo uliifanya sehemu fulani. Kila sehemu ulipiga picha ili kuwavutia watazamaji.
Basi hii unaweza kutumia maneno machache na kuiacha picha izungumze na kumfanya msomaji avutike zaidi.
Pitia makala hii ya ARUSHA TOUR uone jinsi nilivyo kuwekea na vielelezo vya picha mbali mbali na jinsi zinavovutia au tena pitia hii- ARUSHA TOUR - 2
5. UHARIRI / EDITION
Wakati huu ndio unahitaji utulivu kuliko wakati wote. Akili yako yote iwe hapa
Unajua kwanini?
Hii ndio hatua ya mwisho ya upishi wa chakula chako kabla ya kwenda kwa mlaji.
Hivyo fanya yafuatayo wakati wa kuhariri (Editing)
- Soma kwa sauti (neno kwa neno)
Jifanye kama wewe ndiye msomaji wa makala hiyo, soma kwa sauti kana kwamba kuna mwalimu amekusimamia anakusikiliza.
Ikiwezekana mualike rafiki yako na usome mbeye yake kisha naye asikilize mtiririko wa sentesi za mada yako.
- Mpelekee mtu mwingine (Mtaalamu)
Kama kuna mtu (Mtaalamu) unayemuamini, baada ya kuandika makala yako mpe asome mbele yako. Akukosoe kama ikibidi.
- Sahihisha bila kuhofia
Usione uzito kufuta / kurekebisha sehemu kubwa ya maandishi yako ili kuweka sawa. Kwani msomaji wako anatakiwa apate kitu ambacho ni bora.
Hivyo jihakikishie kwanza ubora wewe mwenyewe kisha mpe msomaji wako kwa maana sasa unaweza kuchapisha makala yako.
Hizi ni baadhi ya mbinu chache ambazo nimekukusanyia ili nawe uzifahamu.
Kama kuna nyongeza / makosa yoyote unaweza kutuandikia hapo chini katika sehemu ya COMMENT.
Mpaka hapa nikushukuru kwa ushirikiano wako wa kuweza kuwa nami mpaka mwisho wa makala hii.
Naamini mambo haya tukiyafanyia kazi mimi nawe, tunaweza kufanikiwa na kufika mbali katika kazi zetu za uandishi.
Mungu abariki kazi ya mikono yako.
COMMENTS