Kwa upande wa kanda za pwani m buyu ni mti unao ogopwa sana kwa sababu waganga na wachawi huutumia kwa matambiko. Hizi ni faida za matunda yake
Mibuyu ni miti ambayo hupatikana sana maeneo ya kanda ya kati ya Tanzania mikoa Kama Dodoma na Singida.
M'buyu huzaa matunda ambayo hujulikana kama ubuyu. Ni matunda ambayo ni makubwa na tunda zake ndizo hasa hutumika na wanadamu. Unaweza kumung'unya tunda zake au kutengeneza juis.....
Leo nakueleza kwa kina faida za ubuyu (hasa unga wake)
Chukua ubuyu mbichi kisha utwange na kupata unga. Tengeneza juis yake na uwe unatumia kila siku glass moja (Hasa usiku) hutibu magonjwa yafuatayo:-
![]() |
Mti wa mbuyu |
- Kwakuwa ubuyu una vitamin C mara sita zaidi ya machungwa, hivyo husaidia katika mambo haya.
- Inasemekana kuwa ubuyu una madini ya Calcium mara mbili zaidi ya maziwa ya ng'ombe.
- Pia ubuyu una madini ya Chuma, magnesium na potasium
- Kuongeza kinga ya mwili
- Hulinda mwili
- Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
- Huwasaidia wagonjwa wa presha ya kushuka na wagonjwa wa figo
- Ina magnesium ambayo husaidia kuimarisha mishipa ya moyo
- Huongeza nuru ya macho
- Husaidia kujenga neva za fahamu za kichwa
TAHADHARI
Watu wengi wa mekuwa wakiwenga rangi mbali mbali katika ubuyu ili kuleta muonekano wenye kuvutia. Baadhi ya rangi hizi zina kemikali na huenda zikawa na athari kwa mtumiaji.
COMMENTS