HATARI 5 ZINAZOSABABISHWA NA KUKAA CHINI MUDA MREFU

Moja ya matatizo yaletwayo na kukaa kwa muda mrefu ni kufa ukiwa bado kijana. Soma makala hii kuona madhara mengine

_________________

Bila shaka somo hili linatuhusu sana sisi ambao tunakaa mda mrefu katika Computer / magari / mafundi nguo n.k. Na kibaya zaidi ndio mfumo wetu wa maisha ya kila siku. 

Tutapona kweli?

Lakini ambacho tunatakiwa kujua ni kwamba kukaa chini sio tatizo, bali tatizo ni kukaa chini kwa muda mrefu bila kunyanyuka hasa kukaa mkao ambao si salama hususan kama hufanyi mazoezi kabisa.

  • Hapa nimekuorodheshea madhara matano (5) ya kukaa chini kwa muda mrefu.

1. MAUMIVU YA UTI WA MGONGO
Hii huwakuta wengi katika ambao hukaa chini kwa muda mrefu, nadhani hata nawe ni shahidi juu ya hili. Hii ni kutokana na kupinda kwa uti wa mgongo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya DNA nchini India imegundua kuwa wagonjwa wengi wenye matatizo ya uti wa mgongo ni vijana wa miaka 20 - 30 na wengi wao ni ambao hufanya kazi za kukaa chini kwa muda mrefu.

Kwa miaka ya sasa ugonjwa wa uti wa mgongo na mgongo kwa ujumla umekuwa ni janga liwakumbalo wengi, na ni kutokana na kufanya kazi za kukaa kwa muda mrefu.

2. UWEZEKANO WA KUPATA KISUKARI
Uwezekano wa kupata kisukari kwa mtu mwenye tabia ya kukaa chini muda mrefu ni zaidi ya mara 14 ya watu wengine. Kama unataka kuepukana na matatizo haya kwa asilimia kubwa basi acha / Punguza kukaa chini kwa muda mrefu bila kunyanyuka.

3. HATARI YA KUPATA KANSA YA TITI

Ni rahisi kupata kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana 

Mara nyingi magonjwa haya ya kansa yameonekana kujitokeza kwa watu wengi ambao kwa lugha nyepesi tunawaita KULA - KULALA. Yaani watu ambao hawapenndi kazi wala mazoezi ya viungo.

Hii ndio maana wanawake wengi hupatwa na kansa ya TITI kwa sababu wengi wao ni watu wa kukaa muda mrefu bila kujishughulisha.

4. HATARI DHIDI YA MAGONJWA YA MOYO
Matatizo katika njia ya upumuaji ni moja ya matokeo makubwa ambayo unaweza kuyapata ukiwa ni mtu wa kukaa kwa muda mrefu na hatari yake ni zaidi ya mara 147 kwa sababu ya kutopata oksijeni ya kutosha.

Kadiri unavyokaa masaa mengi ndivyo vimeng'enya ambavyo hufanya kazi ya kuunguza mafuta mwilini huwa na nguvu chache. Hii moja kwa moja ina uhusiano na tatizo la unene kutokana na mafuta kutokuunguzwa vizuri mwilini.
5. KUFA UKIWA BADO KIJANA MDOGO
  • Nadhani hakuna anayependa kufa mapema.
  • Shirika la afya duniani limesema mtindo wa kukaa masaa mengi kwenye kiti ndiyo unaohusika na kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi katika nchi nyingi zilizoendelea.

Na uzito kupita kiasi ni moja ya tatizo kubwa la afya kwa mtu mzima yoyote kuwa nalo ingawa wengi hawaelewi hilo. Watu wengi hasa wa Afrika wakiwa wanene au wenye uzito mkubwa ndiyo hudhani hiyo ni afya kumbe sivyo.

  • Uzito na unene kupita kiasi huja na matatizo mengine makubwa ikiwa ni pamoja na matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kisukari, stroke (Kupooza), kukosa usingizi n.k na haya yote yanaweza kupelekea wewe kufa ukiwa bado kijana.
  • Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2014 ulitoa hitimisho kwamba kukaa kwenye kiti masaa mengi ni moja ya sababu ya vifo vya mapema kwa watu wengi.
  • Mtandao wa Huffington ulienda mbali zaidi na kusema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu kwa siku ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6 na kuwa kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaua watu wengi zaidi duniani kote kuliko hata UKIMWI.
TANBIHI

Pamoja na kuwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa, bado unatakiwa utumie muda fulani kukaa pia, usisimame masaa yote kutwa nzima, ukisimama masaa matatu tumia nusu saa nyingine kukaa hivyo hivyo mpaka siku yako inaisha.

Nini maoni yako? umekaa muda mrefu kwenye kiti na unapata mojawapo ya madhara yaliyoandikwa hapa? 

Tuandikie maoni yako hapo chini.....


COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: HATARI 5 ZINAZOSABABISHWA NA KUKAA CHINI MUDA MREFU
HATARI 5 ZINAZOSABABISHWA NA KUKAA CHINI MUDA MREFU
Moja ya matatizo yaletwayo na kukaa kwa muda mrefu ni kufa ukiwa bado kijana. Soma makala hii kuona madhara mengine
https://1.bp.blogspot.com/-JuGXjVX70tc/X89Sw9kVULI/AAAAAAAAbbQ/y_b0JwIyrLY1zO22Siub5s3o-Sldhu6GQCLcBGAsYHQ/s320/sitting-the-new-smoking-64195753.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-JuGXjVX70tc/X89Sw9kVULI/AAAAAAAAbbQ/y_b0JwIyrLY1zO22Siub5s3o-Sldhu6GQCLcBGAsYHQ/s72-c/sitting-the-new-smoking-64195753.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/09/hatari-5-zinazosababishwa-na-kukaa.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/09/hatari-5-zinazosababishwa-na-kukaa.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content