YAFAHAMU MADARAJA 10 MAREFU ZAIDI DUNIANI

Daraja ni 'Ulalo uliojengwa juu ya maji kwa ajili ya kuwawezesha watu kuvuka upande wa pili' 

Lakini pia yako madaraja ambayo yamejengwa kwa ajili ya kuepuka misongamano ama manufaa mengine ya wanadamu.

Hapa nimekuletea orodha ya madaraja 10 marefu zaidi duniani. Madaraja haya nimeyachanganya kwa ujumla yaani yaliyojengwa juu ya maji, angani na vile vile njia za reli.

Muandaaji na Mwandishi ni Saidi Bunduki


 10. MENCHAC SWAMP BRIDGE

Daraja hili linapatika katika nchi ya Marekani Jimbo la Louisiana na lina urefu wa maili 22.8 ambazo ni sawa na futi 120,000 (Laki moja na elfu ishirini) au kilomita 36. Urefu huu ni sawa na viwanja 366 vya mpira wa miguu.

Ikiwa daraja hili limeshika nafasi ya kumi, je? yanayoendelea mpaka namba 1 yatakuwa na urefu gani?... endelea na makala hii kujifunza zaidi.


 Hapa chini ni sehemu ya daraja hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mnamo mwaka 197909. WUHAN METRO BRIDGE
Hili ni daraja la reli lililoko juu ambalo hupita katika mji Mkubwa na wenye idadi kubwa ya wa Wuhan huko nchini CHINA. Daraja hili lilikamilika mnamo mwaka 2009 ambapo line ya kwanza ilikamilika mnamo mwaka 2004. Kutokana na kupita kwa kiasi kikubwa cha maji ya mto Yangtze na mto Han ndipo wakaamua kuongeza line nyingine.


Daraja hili lina urefu wa maili  23 sawa na futi 124,000 au kilomita 37. Hapa chini Nimekuwekea Sehemu ya picha ya daraja hilo.08. LAKE PONTCHAR TRAIN CAUSEWAY BRIDGE

Unaambiwaje? Hili ndilo daraja refu zaidi duniani katika madaraja ambayo yamepita chini ya maji. Hizi ni takwimu za mwaka 2011. Ila ukichukua madaraja yote kwa ujumla hili linashika nafasi ya 8 kama ilivyo hapa kwenye orodha hii.

Pitia na makala hii

FAHAMU KUHUSU MICHEZO MAARUFU YA GOOGLE DOODLE

Daraja hili lina urefu wa maili 23.83 sawa na kilomita 38 na lina LINE mbili zilizoachana. Daraja hili limekatiza katika ziwa Pontchartrain huko katika jimbo la Louisiana ya kusini nchini Marekani na lilijengwa mwaka 1969. Picha yake ni kama linavoonekana hapo chini.07. BEIJING GRAND BRIDGE

Huu ni miongoni mwa miradi mikubwa ya reli ya mwendokasi nchini China ambayo huunganisha miji mikubwa ya Beijing na Shanghai. Daraja hili lilikamilika mwaka 2010 na urefu wake ni maili 29.92 sawa na kilomita 48.


Kielelezo cha chini kuonesha Daraja hilo.06. BANG NA EXPRESS WAY

Hili ni miongoni mwa madaraja marefu zaidi ya nchi kavu duniani. Mfumo wake ni wa kuvutia na kustaajabisha. Urefu wake kwa ujumla ni futi 177,165 ambazo ni sawa na kilomita 54. Daraja hili liko nchini Thailand katika mji wake mkuu ambao ni BANKOK.
05: WEINAN WEIHE GRAND BRIDGE

Daraja hili lililoko katika miji ya Zhengzhou na Xi'an nchini CHINA lina urefu wa futi 261,000 ambazo ni sawa na kilomita 79.5
04: TIANJIN GRAND BRIDGE

Tianjin ni mji wa nne kwa ukubwa nchini CHINA ambao upo katika pwani kati ya mjia wa Beijing na Shanghai. 

Daraja hili limepewa jina la mji huu na lilikamilika mnamo mwaka 2010 na kufunguliwa rasmi mwaka 2011. Urefu wake ni futi 373,000 ambazo nia sawa na kilomita 113.

Kwa hapa Tanzania huu ni zaidi ya Umbali wa kutoka Mbeya hadi Tunduma. Nimekuwekea picha yake hapa chini.

  

Pitia na makala hii

MIJI KUMI HATARI ZAIDI BARANI AFRIKA


  03: CANGDE GRAND BRIDGE

Hili ni daraja ambalo limeshika nafasi ya  tatu kwa urefu katika madaraja ya njia ya reli. Urefu wake ni futi 380,000 ambazo ni sawa na kilomita 115. 

Daraja hili lilikamilika mwaka 2010 na linapatikana nchini China. Tunaomba radhi kwani Hatukufanikiwa kupata picha yake.


02: CHANGHUA - KAOSIUNG VIADUCT
Daraja hili lilijengwa huko Taiwan mwaka 2004. Unaambiwa mpaka kufikia mwaka 2010 hili ndilo lilikuwa daraja refu kuliko yote Duniani. Urefu wake ni futi 516,000 ambazo ni sawa na kilomita 157

Ni miongoni mwa madaraja ya reli ya treni za mwendokasi huko Taiwan.
01: DANYAN - KUNSHAN GRAND BRIDGE

Dayan - kunshan Bridge lilikamilika ujenzi wake mnamo mwaka 2010 na kufunguliwa rasmi mwezi wa sita mwaka 2011. Daraja hili ni sehemu ya reli ya mwendo kasi ya Beijing kuelekea Shanghai nchini CHINA.

Fahamu pia

SEHEMU 5 ZA AJABU DUNIANI

Urefu wake ni futi 540,000 ambazo ni sawa na kilomita 164. Na hili mpaka sasa ndilo hushikilia rekodi ya madaraja marefu zaidi Duniani (Kwa madaraja ya aina zote yaani nchi kavu, majini na relini) Picha yake ni hii hapa chini


Je ? una maoni / ushauri au mapendekezo?

Tuandikie hapo chini katika sehemu ya COMMENTS

COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: YAFAHAMU MADARAJA 10 MAREFU ZAIDI DUNIANI
YAFAHAMU MADARAJA 10 MAREFU ZAIDI DUNIANI
https://1.bp.blogspot.com/-kSxs3zYaJko/X8DeQEDAHnI/AAAAAAAAa-E/Z69RCT3PErsDia0FVob7WX0RNtblnlkcACLcBGAsYHQ/w579-h206/Manchac_Bridge.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-kSxs3zYaJko/X8DeQEDAHnI/AAAAAAAAa-E/Z69RCT3PErsDia0FVob7WX0RNtblnlkcACLcBGAsYHQ/s72-w579-c-h206/Manchac_Bridge.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/09/yafahamu-madaraja-10-marefu-zaidi-dunini.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/09/yafahamu-madaraja-10-marefu-zaidi-dunini.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content