MBINU 5 ZA KUKUFANYA UNYWE MAJI MENGI ZAIDI

  MAJI NI UHAI Huwa kila ninapokaa mitamboni kwangu na kuandika makala kwa ajili yako mara nyingi huwa na kikombe changu cha maji pembeni. H...

 


MAJI NI UHAI

Huwa kila ninapokaa mitamboni kwangu na kuandika makala kwa ajili yako mara nyingi huwa na kikombe changu cha maji pembeni.


Hii ni baada ya kuzijua faida za kunywa maji katika mwili wa binadamu. Ndipo nikaamua kinywaji changu pendwa kiwe ni maji tu.


Zaidi ya asilimia 70 katika mwili wa binadamu ni maji. Maji yana kazi nyingi sana ikiwemo 
  • Kuondoa sumu mwilini
  • kusaidia mmengenyo wa chakula tumboni 
  • kuwezesha mfumo wa mzunguko wa damu kufanya kazi ipasavyo
  • Kuboresha na kuimarisha ngozi
  • Kuzuia mawe kwenye figo
  • Kuzifanya nywele kukua na kuwa na afya bora

Lakini kwa wengi imekuwa vigumu kunywa maji mara kwa mara kutokana na sababu mbali mbali. Mingoni mwa sababu hizo ni pamoja na Kutokuwa na kiu, maji kuwa na ladha mbaya lakini pia kutojua umuhimu wake

Hapa nimekuwekea mbinu 5 ambazo zitakurahisishia unywaji wako wa maji kwa kila siku na kutengeneza vema afya yako

1. FAHAMU MAHITAJI YAKO YA MAJI
Huwezi kufanya kitu bika kujua umuhimu wake, hapa kwanza lazima utambue kuwa mwili wako unahitaji maji kiasi gani?

Mahitaji ya maji ya kila siku yanapendekezwa kuwa isiwe chini ya mililita 1,920 hii ni sawa sawa na Glass 8 za kawaida.

Lakini wataalamu wa mambo ya afya wakaenda mbali zaidi kwa kupendekeza kwa wanaume wanywe maji hadi mil 3,700 na wanawake 2,700 kwa siku moja. Lakini pia hii huweza kutofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine kutokana na ugumu wa kazi anazofanya au mazoezi.

2. WEKA MAJI KARIBU KARIBU NAWE
Hii itakusaidia pindi uwapo kwenye shughuli yako ya kila siku kila mara ukionapo kinywaji chako itakurahisishia kunywa maji mara kwa mara. 

Hiki ni kikombe changu cha maji ambacho kinakuwa karibu yangu kila ninapochapisha makala zangu kama hii.


Na huwa nahakikisha kila kinapokauka nakijaza tena, basi naweza kunywa zaidi ya vikombe 10 kwa mchana mmoja.

3. TUMIA MAJI BADALA YA VINYWAJI VINGINE
Jitahidi kuweka maji kama kinywaji chako kikuu na punguza unywaji wa vinywaji ambavyo kwa asimilia kubwa vina kemikali ambazo zina athari katika mwili wako. Mfano soda na baadhi ya juis za viwandani.

4. ONGEZA LADHA
Huenda kutokuwa na ladha kwa maji kukakuchosha. Lakini unaweza kuongeza ladha katika maji yako ama tafuta kichocheo ambacho kinaweza kukufanya kunywa maji mengi zaidi. Kunywa maji yenye limau au ndimu ni miongoni mwa njia nyepesi za kuyatia ladha maji na kukuvutia kunywa.
Lakini pia unaweza kula baadhi ya vyakula ambavyo huongeza kiu, kama vile karanga, korosho n.k.

5. KULA VYAKULA VYENYE MAJI MENGI
Yapo matunda na vyakula ambavyo vina asilimia kubwa ya maji ndani yake. Hivi vitakuwa msaada mkubwa sana kwako na ni m badala mzuri wa kunywa maji hasa kwa wale ambao ni wavivu kunywa maji

Tikiti maji, Matango, saladi ni miongoni mwa vyakula hivyo

Soma na makala hii

Bila shaka ukizifuata nyia hizo tano zitakurahisishia kufikia kiwango cha kawaida cha kunywa maji kila siku. Tunahitaji kuishi na maji ni UHAI hivyo lazima tupendane kwa kupeana elimu kama hizi.

Baada ya kumaliza kusoma makala hii, tuandikie maoni yako hapo chini sehemu ya COMMENT.

Asante sana kwa kuwa nasi

COMMENTS

BLOGGER: 2


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MBINU 5 ZA KUKUFANYA UNYWE MAJI MENGI ZAIDI
MBINU 5 ZA KUKUFANYA UNYWE MAJI MENGI ZAIDI
https://1.bp.blogspot.com/-Sj5LDYGF864/YBZ5A9i0fDI/AAAAAAAAb4U/oQEsDmvZuKg9OK45QJRRpjkTaCeh5x2QACLcBGAsYHQ/s320/images%2B%25287%2529.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-Sj5LDYGF864/YBZ5A9i0fDI/AAAAAAAAb4U/oQEsDmvZuKg9OK45QJRRpjkTaCeh5x2QACLcBGAsYHQ/s72-c/images%2B%25287%2529.jpeg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/10/kunywa-maji-kwa-njia-hizi-10.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/10/kunywa-maji-kwa-njia-hizi-10.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content