Hebu tuanze kwa kuimba kidogo "Happy birthday to you, happy birthday to you, Happy birthday dear BUNDUKI Happy birthday to you&quo...
Hebu tuanze kwa kuimba kidogo

"Happy birthday to you,
happy birthday to you,
Happy birthday dear BUNDUKI
Happy birthday to you"
*******************
Mwezi wa kumi (October) ni miongoni mwa miezi ambayo wamezaliwa watu wengi maarufu Duniani.
Hawa ni baadhi yao
- Waziri Mkuu wa Uingereza - THERESA MAY (Odtober 1)
- Rais wa Urusi - FLADMIR PUTTIN (October 7)
- Waziri Mkuu wa Israel - BENJAMIN NETTANYAHU (October 21)
- Rais wa Rwanda - PAUL KAGAME (October 23)
- Rais wa Kenya - UHURU KENYATA (October 26)
Lakini pia baadhi ya watu maarufu kwa hapa Nchini kwetu ni pamoja na
- Msanii mkubwa wa muziki wa bongo flavour - NASIBU ABDUL maarufu kama DIAMOND PLATINUMZ (October 2)
- Rais mstaafu wa Awamu ya nne DR JAKAYA MRISHO KIKWETE (October 7)
- Rais wa sasa wa Tanzania DR JOHN POMBE MAGUFULI (October 29)
KWANINI TULIANZA KWA KUIMBA?
Kwa sababu nami ni miongoni mwa ambao walizaliwa katika mwezi huu.
Nilizaliwa tarehe 12 /10 /1989. Huenda nami siku moja nikawa maarufu kama walivyo hao waliotangulia
Soma historia yangu kwa ufupi kwa kubofya hapa chini
Leo nikiwa ninatimiza umri wa miaka 31. Nimeona nikushirikishe katika hili ambalo huenda ulikuwa hulifahamu.
Watu wengi wamekuwa wakiimbiwa wimbo wa "HAPPY BIRTHDAY TO YOU" pale zinapofika siku zao za kuzaliwa. Huenda nawe umeshawahi kuimbiwa au kumuimbia mwingine wimbo huu au umeshawahi kuusikia ukiimbwa. Lakini je? Unamfahamu aliyetunga na kuimba wimbo huu?
Wimbo huu unajulikana ulimwenguni kote na huimbwa zaidi ya mara elfu moja kwa siku. Asili ya wimbo huu ni wimbo usemao "Good morning to you all" ambao ulitungwa na wadada wawili mmoja wapo akiwa ni mwalimu wa shule ambaye alijulikana kwa jina la Mildred J Hill na nduguye Patty Smith Hill mwaka 1893 huko Louisville KY nchini Marekani.
Lakini kuna machache ya kufahamu kuhusu wimbo huu;-1. Kabila ya kuwa hivi, wimbo huu ulikuwa ni "Good morning to you all" yaani Habari za asubuhi wote. Na ulikuwa ni wimbo ambao wanaimba watoto wa chekechekea waingiapo darasani
COMMENTS