Umewahi kuzisikia zile hadithi za kale kuhusu nyangumi? 'Kwamba anaweza kutokeza mgongo wake nje ya maji na watu wakafanya shughuli zao ...
Umewahi kuzisikia zile hadithi za kale kuhusu nyangumi?
'Kwamba anaweza kutokeza mgongo wake nje ya maji na watu wakafanya shughuli zao zote kwa kudhani kuwa ni kisiwa?'
Basi makala hii itakupa ukweli juu ya samaki huyu na hadithi hizi kwa ujumla.
Mwandishi ni SAIDI BUNDUKI
DUNIA NA MAAJABU YAKE
Huyu ndiye mnyama na samaki mkubwa zaidi duniani. Hapa nimekuelezea baadhi ya sifa zake ambazo zitakustaajabisha.

MAAJABU YA NYANGUMI
- Ukubwa wake
- Ni mnyama asiyekunywa maji kabisa.
- Huishi kwa ndoa za mitara
- Ana mishipa mipana kupita kiasi
- Uume mrefu
- Hana Korodani
- Sauti kubwa zaidi
- Huzaa baada ya miaka mitatu tangu kushika mimba
- Karibu bahari zote duniani nyangumi wapo
- ndiye mnyama mwenye maziwa mengi zaidi
- Ana mwili mkubwa lakini pia ana macho madogo na yenye nguvu kubwa ya kuona
- Uzito wa moyo wake ni sawa na uzito wa gari ndogo kama mark II au IST (Kilo 600)
- Umri mrefu
- Mafuta mengi kwenye maziwa
- Ana uti wa mgongo kama wanya wengine
- Ulimi mzito
- Mtoto wa nyangumi hunyonya lita 600 za maziwa kila siku.
- Mdomo mpana
Vipi kuhusu hadithi tulizokuwa tukisimuliwa?
Nadhani umeshawahi kusikia hadithi za kuwa nyangumi anaweza kutengeneza kisiwa na watu kuishi na kufanya shughuli zao juu ya mgongo wake? Hadithi hizi ni za kufikirika tu na hii yote ni kutokana na ukubwa wa ajabu wa mnyama huyu. Hivyo hazina ukweli wowote
Ni mnyama mkarimu
Ingawa amejaaliwa nguvu na ukubwa kupita kiasi, lakini pia amejaaliwa na ukarimu mno. Kwani hawezi kufanya fujo dhidi ya mwanadamu. Pindi atakapoona meli, boti na chombo kingine cha majini anaweza kujirusha juu na kurusha maji ili aonekane. Kwani anajua kuwa wanadamu wanapenda kumuona. Ingawa hali hii unaweza kudhani kuwa anataka kuwashambulia lakini kumbe sivyo!!
HITIMISHO
Haya ni machache katika mengi yanayomhusu nyangumi. Je? Una chochote cha kuongezea? Basi tuandikie maoni yako hapo chini katika Sehemu ya COMMENT
Ipo vyema aisee, kumbe ndoa za wake wengi hii ndio hekima yake....?
ReplyDeleteBinadamu tu twajifanya wajuzi. Lakini viumbe wa Mungu wanatii amri
Delete