Maajabu ya dunia ni mengi yasio idadi. Miongoni mwao ni maajabu ya mimea mbali mbali. Hapa nimekuletea mimea mitano tu ya ajabu. Endelea...
Kama tunavofahamu kuna aina nyingi za mimea duniani, tunazozijua na tusizozijua. Lakini katika mimea hiyo hiyo iko ambayo ina sifa za kustaajabisha kutokana na maumbile, muonekano, tabia au madhara yake.
Hapa chini ni mimea ya aina tano ambayo ni ya ajabu zaidi. Usisahau kuweka comment yako mwisho wa makala hii.
Muandaaji na mwandishi ni SAIDI BUNDUKI
1. MIANZI
(Mimea inayokuwa kwa haraka)
Mianzi ni miti ya jamii ya magugu ambayo muonekao wake ni kama mua. Miti hii hupatika sehemu kadhaa duniani. Kwa hapa Tanzania hupatikana sana Mkoa wa IRINGA. Pia hutumika kwa matumizi mbali mbali ikiwemo kujengea, kutengeneza vifaa vya asili kama vile kapu n.k. Lakini pia baadhi ya watu huitumia kugema pombe.
Maajabu ya mianzi ni kwamba ndio mti unaoongoza kwa kukua kwa haraka zaidi. Unaambiwa muanzi unaweza kukuwa kwa urefu wa hadi sentimeta 90 kwa siku. (Umeipata hiyo?)
2.VENUS FLYTRAP
Mmea huu huwanasa wadudu kwa majani yake kisha kuwafunika na kuwamengenya.
Majani ya mimea hii hufanya kama mtego. Mdudu anapotua katika jani la mmea huo jani hilo hujifunika ghafla kwa kasi ya chini ya nusu sekunde. Kisha mmea huo hutoa kemikali za kummeng'enya mdudu pole pole ndani ya siku kumi kisha hujifungua tena.
Venus Flytrap hupatikana katika maeneo ya CAROLINA huko nchini Marekani.
3. MANCHINEEL
(Mmea wenye sumu kali)
Suala la mimea kuwa na sumu sio geni, lakini kwa mmea huu ni ajabu zaidi kwani sumu yake ni kali na ya ajabu.
Mmea huo huwa na maji maji ya rangi ya maziwa ambayo humdhuru mtu akiyagusa tu. Ukigusa jani lake pia litakudhuru na kukusababishia vidonda na kuwa kama umemwagiwa maji ya moto.
Hutakiwi kujikinga na mvua chini ya mmea huu, kwani maji ya mvua yakichanganyikana na maji maji yake yakakuangukia mwilini yanaweza kukuwasha sana na kukusababishia madhara.
Lakini pia haitoshi, mmea huo ukichomwa moshi wake ni sumu kali na huweza kumtia upofu mtu na kumsababishia matatizo ya kupumua.
Muonekano wa matunda yake ni kama tunda la tufaha (apple) lakini lina sumu kali sana kiasi kwamba ukilila unaweza kupoteza maisha mara moja.
![]() |
Manchineel |
4. MIMOSA PUDICA
Mmea huu bwana hupatikana sana maeneo yenye misitu ya mvua nyingi huko Sumatra na Borneo nchini Indonesia.
Darasa zzuri asante sana
ReplyDelete