Mwandishi aliadimika sana katika utunzi wa mashairi kutokana na changamoto mbali mbali. Sasa amerudi hivi
Mtunzi ninochipuka, natangaza halaiki
Mana niliadimika, nilikua siandiki
Kutokana na pirika, maisha na nyingi dhiki
Nimerudi ulingoni, shairi tenzi na visa
Nishakitoa kibanzi, kiloshika zangu nyusi
Kimenasuka kitanzi, gari limeshika kasi
Shairi visa na tenzi, ngano za abunuwasi
Nimerudi ulingoni, shairi tenzi na visa
COMMENTS