PENZI KIKOHOZI

1. Alosema kikohozi, hakukosea kusema Kuhusu haya mapenzi, nimemeza si kutema Linanidondoka chozi, nashindwa kurudi nyuma Yanipasa kufunguka...

1. Alosema kikohozi, hakukosea kusema
Kuhusu haya mapenzi, nimemeza si kutema
Linanidondoka chozi, nashindwa kurudi nyuma
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
 
2. Uvumilivu ni kazi, Na umenipita wima
Nimeona niwe wazi, pendo limenisakama
Kwa kusi na kaskazi, meli kwako imezama
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza
 
3. Akili imeniganda, naomba usilaumu
Uwe pete niwe chanda, isitiri yangu hamu
Kiukweli NAKUPENDA, Naomba ulifahamu
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

4. Kimya kimeniathiri, niliogopa kusema
Ukweli hili nakiri, nabeba hii lawama
Nakupenda mwanamwari, tuliza wangu mtima
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

5. Nimeipenda rangiyo, umejaaliwa kweli
Midomo pua sikio, macho yako ya goroli
Tafadhali sema ndio, uwe wangu wa halali
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

6. Ewe binti fulani, Nielewe ndugu yangu
Neno langu la moyoni, Wewe ni wa ndoto yangu
Ila pia samahani, Kama hili kwako chungu
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

7. Niamini nisemacho, sitaki kukuchezea
Kwa mimi nipendacho, nami uje funga ndoa
Na chochote utakacho, kweli nakutimizia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

8. Naomba wako uturi, mtoto unanukia
Nataka nikusitiri, uwe wangu malikia
Nitunzie hii siri, mashoga kuwaambia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

9. Na kama nimekuudhi, msamaha nipatie
Vigezo sijavikidhi, usisite niambie
Wangu nakuomba radhi, Jibu zuri nipatie
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

10. Kumi beti ya tamati, kalamu nawachilia
Nakikunja kibusati, Shairi namalizia
Mebaki msamiati, Je? Utaniridhia
Yanipasa kufunguka, Kimya kitanimaliza

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: PENZI KIKOHOZI
PENZI KIKOHOZI
https://1.bp.blogspot.com/-i1coHnMVYTY/YAqS6Q9OEHI/AAAAAAAAbyc/Gs4KG45mBc8el_mSAgpnrDcFMx2-n4BcQCLcBGAsYHQ/s0/download%2B%25281%2529.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-i1coHnMVYTY/YAqS6Q9OEHI/AAAAAAAAbyc/Gs4KG45mBc8el_mSAgpnrDcFMx2-n4BcQCLcBGAsYHQ/s72-c/download%2B%25281%2529.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/11/blog-post.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/11/blog-post.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content