FAIDA 10 ZA SWALA ZA USIKU KWA MUISLAMU

Usiku ni muda ambao ni mahususi kwa ajili ya kupumzika. Lakini ALLAH ameuwekea BONUS muda huu kwa ambao watautumia kwa ibada

  •     SWALA ZA USIKU NI ZIPI?
  •      NI MUDA GANI ULIOKUSUDIWA?
  •     FAIDA ZAKE
  •     UGUMU WAKE
  •      WITO KWA WAUMINI

                  


SWALA ZA USIKU NI ZIPI?

 Katika Uislamu kuna ibada nyingi ambazo baadhi yao ni sunna na baadhi yake ni faradhi (LAZIMA) 

Katika ibada ambazo ni za faradhi ziko ambazo huswaliwa wakati wa usiku kama vile Magharibi, Insha na Subhi. Lakini ni swala ambazo ni lazima kwa muislamu yeyote kuziswali.

Swala za usiku ambazo tumezikusudia hapa ni swala za Sunna ambazo hutakiwa kuswaliwa usiku wa manane maarufu kama TAHAJJUD (Kisimamo cha usiku)

Lakini mbali na Swalati Tahajudi pia ziko swala kama  Tasbihi, witri na nyinginezo nyingi.

Kutokana na ugumu wake swala hili zimepewa umuhimu wa juu sana kwa ambaye atadumu nazo. Japo watu wengi wamekuwa wakishindwa  kuziswali. (Allaah atuwafikishe tuwe miongoni mwa wenye kuziswali.


NI MUDA GANI ULIOKUSUDIWA?

Muda maalum uliokusudiwa kwa ibada za usiku ni nusu ya tatu ya usiku. Tukisema nusu ya tatu ya usiku ni kuanzia majira ya saa saba hadi saa 11 kabla ya kuchomoza kwa Alfajiri.

Na ni vizuri zaidi kwa muislamu kulala kidogo kisha kuamka muda huu tofauti na kukaa macho na kusubiri muda ufike.


FAIDA ZAKE

Hapa ndipo somo letu hasa tumekusidia liwe. Kwani kama mtu hafahamu umuhimu wa jambo hua haoni faida kulifanya.

"Nakuomba uambatane nami ili kusoma baadhi ya faida hizi chache kati ya nyingi ambazo zimeelezwa na wanazuoni wetu."

 

1. Huongeza imani

Huu ni muda ambao una utulivu sana, kwa Baraka za ibada hizi na kujitoa kwa mja, ni wazi kuwa Allaah atamuongezea imani yake.

 

2. Humtofautisha Muislamu na muumini

Kufikia daraja ya kuwa muumini zinahitajika jitihada za ziada tofauti na ibada za faradhi ambazo Allaah amezifaradhisha. Kwa ibada hizi za usiku ni miongoni wa ibada ambazo humfikisha muislamu wa kawaida kufikia daraja hizo.

 

3. Karama kwa muumini

Karama ni katika vipawa ambavyo wamependelewa baadhi ya wachache. Kwa ibada hizi Allaah atakuruzuku kitu hiki ambacho wengi katika waislamu hawana.

Karama ni uwezo wa kutabiri jambo na likatokea, ndoto za kweli na uwezo wa kumfahamu mtu kabla hajajielezea alivyo.

 

4. Kukubaliwa kwa dua

Wakati huu ni miongoni mwa nyakati ambazo muislamu akiomba dua kwa Allah hairudi.

 

5. Kumpandisha mtu daraja

Kupanda daraja ni katika mambo ambayo ni wachache hupata nafasi hiyo. Kupandishwa daraja na Allaah hutokana na mja kujipendekeza zaidi kwa Mwenyezimungu. Na ibada za usiku ni miongoni mwa yanayoleta upandaji wa daraja.

 

6. Kuleta nuru ya uso

Kama ilivyo kwa mwenye kufanya maasi huzimwa nuru ya uso wake, hasa maasi ya zinaa. Basi kwa watu wema hung’arishwa nyuso zao na Mwenyezimungu kwa Baraka zake. Na mtu akibarikiwa uangavu wa uso basi huwa hajifichi mbele ya watu wema.

 

7. Njia ya kumshukuru Allah

Tumetakiwa kumshukuru Mwenyezimungu kwa mema anayotufanyia. Miongoni mwa kushukuru kwa dhati kabisa ni kujitahidi katika ibada zake. 

 

8. Hufungua mafundo ya shetani

Mja anapokwenda kulala sheitwani kumfunga mafundo matatu na kumbembeleza kwa maneno matamu kuwa “LALA USIKU NI MREFU”

 

Hivyo;-

  •  Unapoamka na kumsabihi Allaah – Umefungua kifundo cha kwanza
  • Unapotawadha umefungua kifundo cha pili
  •  Unaposwali umefungua kifungo cha tatu

 

9. Makazi mema Peponi


Iko pepo maalum kwa ajili wanaoswali swala za tahajudi za usiku.

 

10. Ni sababu ya wanandoa kurehemewa

Mke na mume wanapoamka na kuswali usiku hurehemewa na Mwenyezimungu na kupataa Baraka njema katika ndoa yao.

 

Usiamke kuswali ukamuacha mwenza wako akiwa amelala bila udhuru wowote

Kila jambo huwa na uzito wake, hasa mambo ya kheri huwa na uzito sana ukizingatia kuwa sheitwani naye ana mchango katika hilo.


UGUMU WAKE

Bila shaka utakubaliana name kuwa usiku ni muda wa kupumzika ama sivyo? Sasa miongoni mwa ugumu wa swala hizi ni kuwa zinahitajika uamke muda ambao watu wengi wanakuwa wamepumzika.

Hii ndio maana ALLAAH akaifanya bora kuliko swala nyingine zote ambazo huswaliwa muda wa kawaida. Lakini pia ni muda mgumu hasa katika maeneo ambayo yana baridi kali kwani muda huu ndipo baridi huzidi.

Lakini pia sambamba na hilo pia ni muda ambao unatisha kwa kuwa usiku unakuwa umetulia sana na hakuna kelele nyingi za vitu wala watu

Na siku zote njia ya kufanikiwa huwa ni ngumu, hakuna kufanikiwa bila kujipinda. Hivyo tujitahidi kujipinda katika hili.

Kwa mwenye kutia nia ya dhati na akamuomba Allaah hawezi kuona uzito juu ya ibada zake na kila kitu kitakuwa chepesi inshaallaah.


WITO KWA WAUMINI

Naiusia nafsi yangu pamoja na kuwausia ndugu zangu katika kujitahidi juu ya hili. Duniani tunapita na makazi yetu ni akhera hivyo tujitahidi katika njia ambazo zitatufikisha.

Hakika utukufu ni kutafuta radhi za Allaah kwa kujikurubisha katika ibada zake hasa hizi ambazo si wengi wanazifanya. Kwani m bora wa watu ni Yule mwenye kumcha Mwenyezimungu na si vinginevyo.

MWENYEZIMUNGU ndiye mjuzi zaidi

COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: FAIDA 10 ZA SWALA ZA USIKU KWA MUISLAMU
FAIDA 10 ZA SWALA ZA USIKU KWA MUISLAMU
Usiku ni muda ambao ni mahususi kwa ajili ya kupumzika. Lakini ALLAH ameuwekea BONUS muda huu kwa ambao watautumia kwa ibada
https://1.bp.blogspot.com/-Lfw8RHFy5F8/YAqOvno-YVI/AAAAAAAAbxI/vqsclR02OGYOjfO0Hn93woNMZmdzOtcJwCLcBGAsYHQ/s320/image%2B%25282%2529.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-Lfw8RHFy5F8/YAqOvno-YVI/AAAAAAAAbxI/vqsclR02OGYOjfO0Hn93woNMZmdzOtcJwCLcBGAsYHQ/s72-c/image%2B%25282%2529.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/11/faida-12-za-swala-za-usiku-kwa-muislamu.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/11/faida-12-za-swala-za-usiku-kwa-muislamu.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content