JE? UNA MATATIZO YA KUSAHAU? - JITIBU KWA NJIA HIZI 10


Kusahau (sana) ni miongoni mwa tabia ambazo zinaweza kumfanya mtu ajisikie vibaya na hatimaye kujichukia. Hali inaathiri watu wengi sana, wakubwa na wadogo. Lakini kwa watu wazima (hasa wazee) ni kubwa zaidi.

Dementia ni hali ambayo huwatokea mara nyingi watu wa umri mkubwa. Hali hii huambatana na kusahau kuliko pitiliza. Yaani mtu anaweza kusahau mpaka vitu vya kawaida kama mfano kiti, pazia, meza na kadhalika.

Pia hali ya kurudia swali hilo hilo kila mara na kuchanganyikiwa. Lakini hali hii huletwa na magonjwa fulani kama vile - Alzhimer's disease (hali hii ni hatari)

Tukiachana na hiyo ambayo huwakumba wazee zaidi, ila katika hali ya kawaida kuna aina 7 za matatizo ya kusahau
1. TRANSIENCE (Kusahau kwa muda mfupi)
Hii ni hali ya kusahau matukio kwa muda mfupi uliopita. Matatizo haya humfanya mtu asahau habari ambayo ameipata ndani ya muda mfupi. Ingawa habari ambayo mtu haihitaji kuitumia mara kwa mara ni rahisi kuisahau.

Japokuwa hali ya kusahau mambo kwa muda mfupi inaweza kuonekana kama ni dalili ya udhaifu wa kumbukumbu, wanasayansi wa masuala ya akili huiona hali hiyo kuwa ni ya manufaa kwani huisafisha akili kwa kuondoa kumbukumbu ambazo hazitumiki na kuingiza kumbukumbu mpya na zenye manufaa.

2. ABSENTMINDEDNESS
Aina hii hutokea pale ambapo mtu hatilii maanani jambo fulani. Kwa mfano unaweza kusahau ulipoweka kitu chako kwa sababu tu hukuitilia maanani wakati unaiweka. Huenda wakati unaweka ulikuwa unawaza mambo mengine.

Aina hii ya usahaulifu pia huweza kuathiri baadhi ya mambo yako ya msingi

3. BLOCKING (Kutokumbuka mara moja)
Hii inaweza kuwa ni aina kubwa zaidi ya kusahau. Ni pale ambapo mtu anaulizwa swali na kushindwa kujibu papo kwa hapo. Huu ni usahaulifu ambao akili inashindwa kuifikia kumbukumbu mara moja.

Wanasayansi wanaamini kuwa usahaulifu huu ni kawaida hasa kulingana na umri (umri mkubwaa) wa mtu unavyozidi kuongezeka.

4. MISATTRIBUTION (Kumbukumbu potofu)
Kumbukumbu potofu hutokea wakati mtu anapokumbuka sehemu ya jambo kwa usahihi, lakini akakosea maelezo kadhaa kama vile wakati, mahali, au mtu husika.

Usahaulifu mwingine wa aina hii ni pale unapoamini kwamba dhana uliyokuwa nayo ni halisi wakati ukweli ni kwamba ilitokana na kusoma mahali au kuisikia kwa watu wengine, lakini ukawa umesahau ukweli huo.

Kuhusiana na matatizo mengine ya kupoteza kumbukumbu, kumbukumbu potofu huendana na umri. Mtu anapozidi kuzeeka anakuwa anaingiza habari chache zaidi kwenye akili yake, kwani akili yake inakuwa haina uwezo wa kudaka habari kwa haraka.

5. SUGGESTIBILITY (Kudaka habari potofu)
Kudaka habari potofu pia kunaathiri mfumo wa kumbukumbu, ambapo mtu huiweka habari hiyo katika akili yake akifahamu kwamba ni jambo la kweli wakati siyo kama alivyoliona wakati likitokea. Alidanganyika.

6. BIAS (Kumbukumbu iliyojenga dhana tayari)
Kumbukumbu ya mtu ambayo tayari imejenga dhana fulani inayotokana na mambo aliyoyaona, imani fulani, mambo ambayo ameyapa mwenyewe kipaumbele, itamletea matatizo.

Dhana ambayo tayari unayo kichwani ni dhahiri itaathiri mawazo yako, hivyo kila ukitaka kukumbuka jambo fulani mawazo yako na dhana zako ni lazima yatatawaliwa na habari ambayo unaikumbuka.

Lakini, pamoja na hali hii, wanasayansi hawajafanya utafiti mkubwa kuhusu dhana aliyo nayo mtu na jinsi inavyoweza kuathiri kumbukumbu zake, pia hawajafahamu vyema iwapo hali hiyo huenda sambamba na umri.


7. PRISTENCE (Kumbukumbu mbaya)
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kusahau mambo kila wakati lakini katika matukio mengine, kuna watu ambao huteseka kwa kuwa na kumbukumbu mbaya ambazo hutaka kuzisahau, lakini wanashindwa.

Kuendelea kwa kumbukumbu mbaya na zenye matukio yasiyopendeza au yenye kuleta hisia mbaya ni moja ya matatizo ya kumbukumbu.

Baadhi ya kumbukumbu hizi huonesha matukio ya kutisha na mengine ambayo huwa ni ya kufikirika na hivyo kuleta hisia mbaya.

Kumbukumbu hizi kwa watu wengi hutokana na matatizo ambayo waliyapata kama vile kudhalilishwa kijinsia kama kubakwa, kulawitiwa au matukio waliyoyapata wakiwa vitani.

NJIA HIZI 10 ZIFUATAZO ZITAKUSAIDIA KUIMARISHA UWEZO WAKO WA AKILI NA KUTOSAHAU PAPO KWA HAPO.

1. fanya kazi moja kwa wakati mmoja

Hii itaepusha kuchanganya mambo na kuchanganyikiwa. Jiwekee utaratibu wa kufanya kazi / jambo moja kisha ukisha maliza unaweza kuendelea na jingine.

Kuchanganya mambo kunaweza kukufanya kujisahau na kuvuruga ratiba.

2. Fanya mazoezi ya viungo

Iko wazi kuwa mazoezi ya viungo ni tiba ya maradhi mengi na huuweka mwili kuwa na afya njema. Sambamba na afya ya mwili pia huimarisha afya ya akili. 

Jijengee utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku. Unaweza kupiga push up, kukimbia, kuruka kamba, kutembea  na kadhalika. Fanya hivi kila siku.

Soma

FAIDA 20 ZA KUFANYA MAZOEZI YA VIONGO

3. Tafuna big G (bazoka) 

Unaambiwa utafunaji wa big G huifanya  mishipa ya kichwa kuwa mamkini zaidi (active). Mishipa inapokuwa active ni rahisi kukumbuka mambo kwa haraka

4. Kucheza game 

Cheza game ambazo zinaumiza akili zaidi, mfano ni kama kucheza Draft, Puzzle na nyinginezo.

5. Usingizi wa kutosha

Kitaalamu unatakiwa kwa siku moja usikose kulala masaa takriban 8. Kulala muda wa kutosha huufanya ubongo kupumzika na kukumbuka mambo vizuri.

6. Ongeza maarifa

Jijengee utaratibu wa kuongeza maarifa na ujuzi. Kusoma vitabu ni miongoni mwa njia sahihi za kuongeza maarifa na akili mpya kila siku. Akili inapokuwa makini na uwezo wa kukumbuka mambo ndipo unapoongezeka.

             


Soma pia

FAIDA KUBWA 7 ZA KUSOMA VITABU

7. Jipe muda wa kutafakari

Kujipa muda wa kutafakari (meditation). Kaa sehemu tulivu yenye mandhari nzuri kama vile bustanini, shambani, mtoni, ufukweni na kadhalika. Hii ni moja ya njia nzuri ya kuipa afya akili yako.

8.  Epuka msongo wa mawazo

Epuka kuwa na msongo wa mawazo, ama tunaweza kusema kuwa epuka vyanzo ambavyo vinaweza kukufanya uwe na msongo wa mawazo. Usiruhusu msongo wa mawazo utawale ubongo wako. Msongo wa mawazo huathiri kwa kiasi kikubwa sana uwezo wako wa kukumbuka.

9. Punguza  / Acha pombe

Unywaji wa pombe (hasa kupitiliza) huathiri seli za kichwa pamoja na uwezo wako wa kufikiri /kukumbuka na kuwa makini

10. Panga ratiba ya mambo yako

Unaweza  kujiwekea utaratibu kwa kuandika mambo ambayo unataka kuyafanya ndani ya siku, wiki au mwezi. Pitia ratiba yako ili kujua jambo litakalo fuata baadaye.

NYONGEZA

Kupoteza kumbukumbuku ni chanzo cha mambo yeko mengi kukwama. Jitahidi kufuata njia hizo hapo juu kuimarisha ufahamu wako.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: JE? UNA MATATIZO YA KUSAHAU? - JITIBU KWA NJIA HIZI 10
JE? UNA MATATIZO YA KUSAHAU? - JITIBU KWA NJIA HIZI 10
https://1.bp.blogspot.com/-3c7c7m_raEA/X89PfvQk65I/AAAAAAAAbX8/emj7yezh_WcK1yaTogxoPDZm-hEPHMSRQCLcBGAsYHQ/s320/GettyImages-157249895.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-3c7c7m_raEA/X89PfvQk65I/AAAAAAAAbX8/emj7yezh_WcK1yaTogxoPDZm-hEPHMSRQCLcBGAsYHQ/s72-c/GettyImages-157249895.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/11/je-una-matatizo-ya-kusahau-jitibu-kwa.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/11/je-una-matatizo-ya-kusahau-jitibu-kwa.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content