1. KUSHUSHA HADHI YA BLOG YAKO
Endapo msomaji akipitia machapisho yako na kujua kuwa ume kopy kutoka katika blog nyingine basi msomaji anaweza kuishusha hadhi ya blog yako na kutokurudi tena.
Isitoshe anaweza kutafuta blog ambayo umekopy hilo chapisho na kuifuatilia. Kama kweli uko makini na kazi yako basi ni vema kuumiza akili na kuandika makala ambazo zinaweza kumvuta msomaji na kupenda kutembelea blog yako.
Kwa kupata elimu zaidi juu ya uandishi wa makala unaweza kusoma;-
Mbinu za kuandika makala bora - 1
Mbinu za kuandika makala bora - 2
2. KUKOSA WATEMBELEAJI
Mteja akichungulia na kuona machapisho yako ni yale ambayo hupatikana katika blog maarufu, basi hawezi tena kubaki katika blog yako na utakuwa umeshakosa watembeleaji.
Kwa mfano mteja alitembelea tovuti ya Bongoclass na kusoma mada fulani, kisha mada hiyo akaikuta tena kwenye blog yako ni wazi kuwa hawezi tena kurudi kwako.
3. KUDUMAZA AKILI
Wakati wenzako wanaumiza akili ili kupata mada ambazo zitawakonga watembeleaji wewe una kopy na ku paste na kuweka kwenye blog yako. Huu si ujanja bali ni kudumaza akili yako na matokeo yake ni kazi kukushinda mapema.
Umiza akili, soma sana vitabu, fanya tafiti mbali mbali, andika kwa ajili ya msomaji wako ili aburudike na uwepo wake kwako.
4. KUSHITAKIWA
Hujawahi kuona kuwa baadhi ya watu huwa hawapendi machapisho yao kunakiliwa bila idhini yao? (copy right)
Hii inaweza kupelekea kufungwa jela ama kulipa faini kama ambaye umekopy machapisho yake atakukamata na kuamua kulishughulikia suala hili kwa mujibu wa sheria.
5. KUTOKUAMINIKA
Msomaji hawezi kumuamini mtu ambaye hajiamini. Kutokuwa na uwezo wa kuandika makala zako mwenyewe ni kutojiamini. Jiamini na unachokifanya na kumuaminisha anayekuamini.
6. KUKOSA MATANGAZO
Makampuni na watu wenye biashara zao hawawezi kuweka matangazo yao sehemu ambayo haina uhakika. Hata kama ni wewe ndiye ambaye unataka kutangaza huwezi kutangaza na blog ambayo inanakili habari / makala kutoka sehemu nyingine.
badala yake utakwenda kule kwenye chanzo chenye kuaminika.
7. KUFA KWA BLOG
Blog nyingi zimekufa, blog nyingi hazina machapisho kwa muda mrefu. Miongoni mwa sababu ambazo zimepelekea hivyo ni wamiliki wa blog hizo kunakili machapisho kutoka kwenye blog nyingine.
Soma makala hii
Mwisho wa siku anaona kuwa jambo analolifanya halina maana na kuamua kuachana na mambo hayo.
SI VIBAYA KUFANYA HIVI
Kwakuwa baadhi yetu ndo tunaanza tasnia hii (blogging), kuna wakati inatuwia vigumu kupata cha kuandika. Hivyo unaweza kufuata njia hizi hapa chini ambazo zitakusaidia.
*Badala ya kukopy na ku paste, unaweza kusoma kuongeza ujuzi kisha kama utapenda unaweza kutengeneza makala ambayo itafanana na ile ambayo ulisoma katika blog fulani.
* Kama andiko umelipenda, unaweza kuomba idhini kwa mmiliki wa blog hiyo na akakupa idhini ya kuliweka. Au pia unaweza kuweka link ya blog husika kwa wasomaji wako na kuelekea huko ili kupata makala hiyo.
Ikitokea umekosa kabisa wazo la kuandika basi usijisikie vibaya kwani ni kawaida kwa mwandishi.
Hapa chini nimekuwekea maujanja ya jinsi gani utafanya endapo umekosa cha kuandika katika blog yako.
Soma
Njia 4 za kufanya kama umekosa cha kuandika kwenye blog yako
Safi sanaaaa,
ReplyDelete