MAMBO 10 YA KUSHANGAZA KUHUSU KANGAROO

Pamoja na kwamba huutumia mkia wake kwa ajili ya kupata balansi, lakini pia huutumia kama mguu mwingine wa tatu.

Je unamfahamu Kangaroo? 

Kangaroo ni jamii ya wanyama ambao hujulikana kitaalamu kama macropods 

Jina hili maana yake ni wanyama wenye  "mguu mkubwa" Mguu huu ni mkia  wao ambao huwasaidia kuukita chini kisha kupiga hatua au kuruka.

Katika jamii ya wanyama hawa, huyu ndiye macropod mkubwa zaidi.

Katika makala hii utajuwa yafuatayo

 • Kangaroo wana ukubwa gani?
 • Kangaroo hupatikana wapi?
 • Maajabu yao ni yapi?
 • Kangaroo wanakula nini?
 • Vipi kuhusu kupigana kwao?

Maoni yako ni muhimu sana, hivyo baada ya kusoma makala hii tuachie maoni yako chini kabisa ya makala hii


 • UKUBWA WA KANGAROO
Kangaroo mkubwa anaweza kufikia urefu wa futi 5 mpaka 6 kwenda juu, wakati uzito wake ni katika ya kilo 23 mpaka 55. Madume huwa na uzito mkubwa kuliko majike.

Soma pia

 • JE? KANGAROO HUPATIKANA WAPI?
Wanyama hawa hupatikana kwa wingi sana katika Nchi ya Australia

 • MAMBO YA KUSHANGAZA KUHUSU KANGAROO


1. HAWEZI KURUDI NYUMA

Kangaroo anashindwa kurudi nyuma kwa sababu mkia wake jinsi ulivyo mkubwa na wenye misuli humfanya hawezi kuruka nyuma. 

Watu wa nchi ya Australia ambako Kangaroo ni wengi zaidi, wameichukua hii kama hamasa ya kwamba "Mbele daima, hakuna kurudi nyuma"


2. WANA MAJINA TOFAUTI

Kangaroo dume huitwa boomers, kangaroo wa kike huitwa Flayers, watoto wao huitwa joeys.

Wakati huo huo kundi la kangaroo huitwa mob, troop au court. Kangaroo ni wanyama ambao wanapenda kuwa katika makundi, yaweza kuwa makundi madogo kati ya 3 - 5, au hata makundi makubwa ambao hufika mpaka 100.

Kundi kubwa la Kangaroo

3. AKIKIMBIZWA HUKIMBILA KWENYE MAJI

Kangaroo si mnyama anayewindwa sana na wanyama, ila mara kadhaa hutokea hata kuwindwa na binadamu hivyo hupenda kukimbilia zaidi kwenye maji.

Lengo la kukimbilia kwenye maji ni kumzamisha adui yake na kuweza kumtoroka. Lakini pia kama ulikuwa hujui kangaroo ni miongoni mwa wanyama ambao hurusha sana mateke. jambo ambalo ni hatari hata kwa binadamu.


4. WENGI WAO HUTUMIA MKONO WA KUSHOTO

Ingawa tumezowea kuona kwa binadamu kuwa baadhi yao hutumia mkono wa  kushoto, basi ni vile vile kwa kangaroo wako ambao hutumia mikono yao ya kushoto katika shughuli zao kama vile kulisha na utunzaji wa familia.


5. HAWATOKI JASHO

Kangaroo hawana tezi zinazosababisha jasho. Hivyo hutegemea zaidi kupumzi katika kivuli wakati wa joto.

Wanapohitaji kupata baridi hulamba mikono yao na manyoya yao.


6. UZAZI WA AJABU

Mtoto wa kangaroro anapozaliwa huwa ni mdogo sana kiasi cha kulingana ukubwa na mbegu ya maharage.

"Naaam usishangae ndivyo ilivyo"

Baada ya kuzaliwa akiwa na ukubwa wa nyuki, basi hutambaa katika manyoya ya mama yake mpaka kufika katika mfuko maalum wa mama yake na kukaa hapo kwa ajili ya kukua. Hapo anaweza kukaa hata mwaka mmoja.

Madume hukaa muda mrefu zaidi kuliko majike.


6. ANAWEZA KUSITISHA MIMBA

Kangaroo akishazaa ana uwezo wa kushika mimba kwa mara nyingine. Kisha akaisitisha mimba hiyo mpaka pale ambapo mtoto aliyepo katika kipochi cha mbele kwa mama yake atakapokuwa tayari kutoka na kujitegemea.

Picha ya chini inamuonesha kangaroo jike ambaye yupo na mwanae katika kipochi chake.


7. NI WENGI KULIKO WATU

Hii ni kwa nchi ya Australia ambako hupatikana.

Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika mwaka 2019 ilibainika kuwa na idadi ya watu nchini humo ni milioni 25 wakati idadi ya kangaroo ilikuwa ni zaidi ya milioni 48.


08. MKIA WAKE HUUTUMIA KAMA MGUU

Pamoja na kwamba huutumia mguu wake kwa ajili ya kupata balansi, lakini pia huutumia kama mguu mwingine wa tatu.

Matembezi yao ni ya kipekee, hukita chini mkia wake na kuruka juu. Kwani mkia ni mguu sambamba na miguu yake.


09. HUPIGANA (BOXING)

Kangaroo dume hupigana ili kujua nani mwenye nguvu zaidi na uimara. Hapa kangaroo jike huangalia kuwa ni dume gani imara na kuamini kuwa watoto wao wanaweza kuwa imara pia.

Wanapopigana hushikana kwa mukono yao ya mbele na kupigana kwa miguu. Lakini pia wanao uwezo wa kukita mikia yao na kupigana kwa kutumia miguu yao ambayo ina nguvu sana.

Kangaroo boxing

10. Kangaroo pia hujipendekeza na kujionesha kwa wanawake wao. Kitendo ambacho hutunisha misuli yao mbele ya mwanamke na atakayekuwa na misuli mikubwa ana uwezekano mkubwa wa kupendwa zaidi.

 • KANGAROO WANAKULA NINI?

Kangaroo ni jamii ya wanyama walao majani. Hivyo hula nyasi, mauwa, mwani, wadudu n.k

Soma pia

Makala maalum kuhusiana na radi na mambo ya kuepuka

Nadhani mpaka hapa umepata mawili matatu kuhusu mnyama huyu. Je una kingine cha kuongeza kumhusu? Tuandikie maoni yako hapo chini.

COMMENTS

BLOGGER: 4
 1. Inaonekana ni mnyama punguani zaydi kuliko wanyama wote mana mwili mkubwa lakini kichwa kama cha panya,lakini pia nyama yake ni nzuri zaydi kulinganisha na wanyama pori wengi mana ina kiwango kidogo cha maduta, likini pia inaonekana ndio wanyama wenye vibamia kuliko wanyama wote mana kama wanazaa viumbe vidogo kama nzi nawaza tu hizo papuchi zao zitakua kama njia ya sindono vile, sasa ikiwa majike ni hivyo vip kuhusu madume yao???.

  ReplyDelete
 2. Kwani tanzania hamna kangaroo jama?

  ReplyDelete


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MAMBO 10 YA KUSHANGAZA KUHUSU KANGAROO
MAMBO 10 YA KUSHANGAZA KUHUSU KANGAROO
Pamoja na kwamba huutumia mkia wake kwa ajili ya kupata balansi, lakini pia huutumia kama mguu mwingine wa tatu.
https://1.bp.blogspot.com/-p9nIJdc37bM/X6zfp3WwXdI/AAAAAAAAagM/GE7AjWZhZnwWzHXp-cr0WVcUAvuM2LVSgCLcBGAsYHQ/w428-h201/6T4VL6SNJFFLFE3TG2JSQVLMWA.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-p9nIJdc37bM/X6zfp3WwXdI/AAAAAAAAagM/GE7AjWZhZnwWzHXp-cr0WVcUAvuM2LVSgCLcBGAsYHQ/s72-w428-c-h201/6T4VL6SNJFFLFE3TG2JSQVLMWA.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/11/mambo-10-ya-kushangaza-kuhusu-kangaroo.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/11/mambo-10-ya-kushangaza-kuhusu-kangaroo.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content