Unaambiwaje? Ndege inaweza kupaa hata ikiwa injini yake moja haifanyi kazi. Lakini kubwa zaidi inaweza kutua salama hata injini zote zikizima.

Usafiri wa ndege ni usafiri ambao unatumia teknolojia kubwa sana. Wengi katika watu huwa hatufahamu mengi kuhusiana na usafiri huu zaidi ya wataalamu na wengine wachache.
Huenda hujabahatika kupanda ndege, lakini hili halikufanye ujisikie mnyonge. Hapa nimekuorodheshea mambo 25 ambayo yatakushangaza kuhusiana na ndege. (Tunazungumzia ndege kubwa za abiria hasa za kimataifa)
"Tuandikie maoni yako sehemu ya COMMENT chini kabisa baada ya makala hii"
1. Ladha kinywani hupungua ukiwa angani
Ati nini?
"Naaam" Ukiwa unasafiri na ndege angani zaidi ya futi elfu 30, basi theluthi moja ya ladha katika kinywa chako hupotea. Ndio maana wengi hulalamika kuwa vyakula vya kwenye ndege ni vibaya.
Basi leo nakupa siri hii kuwa vyakula vya kwenye ndege sio vibaya, na wapishi wake ni wazuri tu. Ila hiyo ndio hali halisi.
2. Wafanyakazi hulipwa ndege iwapo angani tu
Hii ina maana kuwa rubani hulipwa kwa masaa ambayo amerusha ndege. Hali kadhalika na wahudumu wengine wa ndege.
3. Hata injini ikizima, ndege huendelea
Ndege inaweza kusafiri muda wa masaa matano baada ya injini kugoma kufanya kazi.
Wataalamu wanasema:- Ndege inaweza kuruka kwa injini moja pekee, lakini kubwa zaidi ni kwamba inaweza kutua salama kabisa hata ikiwa injini zote zimezima.
4. Hewa ya ndani ya ndege ni halisi
Unaweza kuhisi kiu na ukavu wa hewa hasa ndege inaporuka na kutua. Ni kwa sababu mfumo wa hewa wa ndani ya ndege ni halisi kama vile upo ndani ya jangwa la sahara.
5. Mfumo wa taa katika mabawa
Ni vigumu kwa rubani mmoja kuiona ndege nyingine wakati wa usiku. Hivyo katika bawa la kushoto kuna taa nyekundu na bawa la kulia kuna taa ya kijani.
Hizi huwawezesha marubani kutambuana kuwa ndege fulani iko upande gani na inaelekea wapi.
6. Vipi abiria akifa ndani ya ndege?
Abiria akifia ndani ya ndege, mwili wake hubaki sehemu alipo (kwenye siti yake) mpaka mwisho wa safari kwa uchunguzi zaidi.
Lakini baadhi ya ndege kubwa zina sehemu maalum ya kuhifadhi miili. Mwili huo unaweza kupelekwa huko na kufunikwa isipokuwa uso.
7. BLACK BOX - Sio jeusi
Bila shaka umewahi kusikia kuhusiana na kifaa hiki. Mara ndege inapopata ajali na kuteketea wataalamu hutafuta kifaa hiki kwanza (Black box)
Hiki ni kifaa ambacho hutunza kumbukumbu za safari zote za ndege. Japo kimepewa jina la black box lakini halina rangi nyeusi.
Black box yaweza kuwa rangi ya chenza au nyekundu. Tazama picha ifuatayo;-

8. Wakati wa kuruka na kutua ni hatari zaidi
Wakati wa kuruka na kutua kwa ndege ni nyakati ambazo marubani huziogopa sana kulingana na hatari yake.
Ni wakati ambao rubani huwa macho na makini zaidi kuliko kipindi kingine wakati wa safari.
9. Marubani hujiburudisha
Kwa ndege za masafa marefu, marubani wanapata muda wa kupumzika na kufanya mambo mengine. Wanaweza kusikiliza mziki, kupiga soga, kucheza game n.k.
Soma
Mambo 10 usiyoyajua kuhusu marubani wa ndege
10. Nyuma ya ndege ni salamaUnaambiwa siti za nyuma zina usalama zaidi kuliko siti nyingine ikitokea hatari.
11. Ndege ina uwezo wa kusababisha radi
Kukatiza kwenye mawingu kwa ndege kunaweza kuzusha radi angani. Ingawa ni vigumu kuiathiri ndege kutokana na mifumo yake ilivyo.
12. Urefu wa nyaya zake
Ndege za boeing 747 ina waya zenye urefu wa maili 140 - 150 (endapo zikiunganishwa)
13. Marubani hula vyakula tofauti. Hii kama ikitokea mmoja kupata machafuko ya tumbo basi mwingine anaweza kumalizia safari.
14. Ni usafiri salama zaidi duniani
Katika nyanja za usafiri, ndege ndio usafiri salama zaidi kuliko aina zote za usafiri (majini, nchi kavu). Ni rahisi kusikia ajali barabarani, relini, majini lakini ni mara chache kusikia ajali za angani.
Na mara nyingi ikitokea basi hakuna anayetoka.
15. Siti za V I P za ndege ambazo ni gharama zaidi duniani hufikia mpaka dola elfu thelathini ($ 30,000) hii ni takriban milioni 70 ya kitanzania.
16. Baadhi ya ndege za masafa marefu huwa na vitanda maalum kwa ajili ya wataalamu wa ndege (engineers) pamoja na marubani
17. Kuishi karibu na njia za ndege ama viwanja vya ndege kunaweza kusababisha athari na magonjwa ya moyo.
18. Ndege yenye kasi zaidi spidi yake ni mara mbili ya spidi ya sauti.
19. Kila wakati - Angani kuna zaidi ya ndege 9,700. Mbapo kuna kadiriwa watu zaidi ya milioni 1.2 wapo angani kila siku.
Nikukumbushe tu kuwa hapa tunazungumzia ndege kubwa za abiria. Lakini pia ziko ndege aina ya helicopter ambazo pengine ungependa kujua mawili matatu kuhusiana nazo. Nimekuwekea makala hiyo hapo chini.
Soma
Mambo 8 usiyoyafahamu kabisa kuhusu Helicopter
20. Ndege nyingi za abiria zina sehemu ya kuwekea majivu ya sigara
Tangu kuwekwa kwa marufuku ya uvutaji sigara ndani ya ndege ni miaka 25 sasa. Lakini ndege nyingi zimewekwa kikasha cha kuwekea majivu ya sigara (ashtray) ili ikitokea mtu ameamua kuvunja sheria basi asidondoshe majibu hayo chini na kusababisha moto.
Kwahiyo kuwekwa kwa ashtray haimaanishi kuwa unaruhusiwa kuvuta - HAPANA.
Asante kW elimu baba imekaa poa iyo.lakini umefanya upendeleo umezungumzia ndege za wazungu tu kuna zile zetu umezitenga na zina maajabu kiliko zao hao.
ReplyDeleteHa ha ha haaa... Tatizo zile material yake hayapatikani ki holela. Hivyo tunashindwa kupata data kamili kuhusiana.
DeleteLakini siku moja tutaleta mada yake
Asante kW elimu baba imekaa poa iyo.lakini umefanya upendeleo umezungumzia ndege za wazungu tu kuna zile zetu umezitenga na zina maajabu kiliko zao hao.
ReplyDeleteGood
ReplyDeleteDah mada nzuri sana mwanangu
ReplyDelete