
Muandaaji wa makala hii ni SAIDI R BUNDUKI
01. NI SALAMA ZAIDI
Ni miongoni mwa maswali ambayo huulizwa sana na watu kuwa "Ni kweli kuwa helicopter ni salama zaidi ya ndege za kawaida? (Air plane)
Utafiti wa kwanza ulionesha kuwa helicopter ni salama zaidi ukilinganisha na ndege ndogo kama vile ndege binafsi (Private jets) sambamba na ndege maalum kwa ajili ya tax.
Hii ni kutokana na madhara ya hali ya hewa kuziathiri zaidi ndege hizi ndogo.
02. HELICOPTER INA MIPAKA MAALUM
Wakati wa hali mbaya ya hewa inashauriwa kuwa si salama sana kuruka angani.
Wakati wa kiza (usiku) hairuhusiwi pia kuruka
Pia ingawa ina uwezo wa kukaa angani kwa muda mrefu (kunata) lakini pia haishauriwi sana kusafiri nayo kwa masafa marefu.
03. INA MAJINA TOFAUTI
Si umeshawahi kusikia jina la 'CHOPA'? Basi hili ni miongoni mwa majina yake maarufu sana. Kila jina limepachikwa kutoka katika nchi fulani kwa sababu maalum.
Baadhi ya majina hayo ni kama vile COPTER, WINDMILL, WHIRLYBIRD lakini pia yako majina ambayo hutumiwa na wanajeshi kumaanisha helicopter kutokana na sababu zao maalum.
04. INA KELELE NA HUYUMBA SANA
Huenda watu wengi wanaogopa kupanda helicopter kwa sababu ya kelele zake na tetememko wake.
"NDIO"
Helicopter huwa na kelele nyingi sana hasa wakati wa kuruka kutokana na mfumo wa mashine yake. Umbo lake hufanya kuwa na mtetemeko wakati wa safari. Sasa unafikiri watu wanapenda kutetemeshwa wakiwa angani?
LA HASHA!
Soma pia
Mambo 20 usiyoyafahamu kuhusu usafiri wa ndege
05. INAWEZA KUSHAMBULIWA NA NDEGE
Ndege aina ya TAI hudhani kuwa helicopter ni ndege mwenzao na ni adui kwao. Lakini pia mbali na helicopter ni kwamba tai hushambulia pia DRONES (camera za kuruka angani).
Tai ana uwezo wa kuruka mpaka futi 6000 kwenda juu, hivyo hudhani kuwa huko angani hakuna uwezekano wa mashine kufika zaidi ya ndege kama yeye.
06. INA UWEZO WA KUFIKA JUU YA MLIMA EVAREST
Mlima evarest ndio mlima mrefu zaidi duniani. Na una urefu wa futi 29,029
Je? zitawezaje kufika kilele cha mlima huo wakati helicopter zina uwezo wa kuruka futi hadi 10,000?
Ukweli ni kwamba ziko helicopter maalum ambazo zimeundwa kwa ajili ya kufika huko. Hizi zina uwezo wa kukata upepo wenye kasi zaidi na kuruka juu zaidi ya hapo.
08 KWENYE DHARURA NI BORA ZAIDI
Kutokana na muundo wake ni nzuri katika matukio mengi tofauti. Inaweza kupenya sehemu nyingi tofauti na ndege nyingine. Lakini ina uwezo wa kuenda paze zote yaani mbele, nyuma na pembeni.
Pia helicopter ina uwezo wa kunata hewani kwa muda mrefu zaidi ikiendelea na shughuli nyingine za uokozi n.k.
Mafuriko, machafuko, vitani, uzimaji wa moto kwenye majengo marefu na mbugani ni sehemu ambazo helicopter hufanya vizuri zaidi.
09. MIL MI - 26 NDIO HELICOPTER KUBWA DUNIANI
Kwa kawaida helicopter ina uwezo wa kubeba watu watano mpaka 6. Lakini helicopter hii ya kivita ya RUSSIA ina uwezo wa kubeba wanajeshi 80
![]() |
COMMENTS