Wakati mwingine ubongo unaweza kufikia ukomo wa kufikiri. Kitu hiki huwaumiza sana waandishi. Lakini hili ni suluhisho
Ubongo hupenda mambo mazuri kila wakati na huwa mara nyingi haupendi kusumbuliwa au sio? Ubongo hupenda ku relax na kula raha wakati wote.
Hii huweza kuwa ni tabia mbaya ambayo inaweza kukuathiri katika shuguli zako za kila siku hasa kama wewe ni mwandishi kama mimi.
Je? wewe ni muandishi, blogger, mtunzi au mhamasishaji katika mitandao mbali mbali ya kijamii na huna IDEA?
Hapa nakufungulia dunia kwa mambo haya manne (4) ambayo yatakufanya upate mawazo ya kitu kizuri ambacho unaweza kuandika.
Tunaweza kuiita mada hii pia ni;-
'JINSI YA KUPATA IDEA YA KUANDIKA MAKALA'
1. TOKA NJE YA NYUMBA YAKO
Umekaa sehemu moja kwa muda mrefu? Hususan ndani ya nyumba yako au ofini kwako. Mazingira ambayo umeyazowea kuwa hayawezi kukupa fikra mpya. Hii ni kawaida katika akili ya mwanadamu.
Vilivyoko ndani ya nyumba yako au sehemu yako ya kazi mara nyingi huwa ni vile vile siku zote. Akili inakuwa imevizowea na kutokuona tofauti.

2. ONDOA VIKWAZO MBELE YAKO
Wazo zuri huja penye utulivu. Kama umepata wazo ambalo unataka kulifanyia kazi basi unatakiwa kuondoa vitu vyote ambavyo vitakusumbua kwa namna yoyote.
Zima TV, Simu weka kimya (silence), Zima redio na pia kama unatumia kuandika kwenye Kompyuta yako ni bora kuzima intanet ila pale ambapo utaihitaji. Ni vizuru kutumia programu za kuandikia badala ya kuandika moja kwa moja kwenye ukurasa wa blog yako.
Pia wakati unaandika makala zako unaweza kutumia kalamu na karatasi / kitabu kisha baadaye utahamishia kwenye laptop yako (Kama nifanyavyo mimi)
3. SOMA MAANDIKO YA WENZAKO
Haimaanishi kuwa usome ili unakili - HAPANA.
Lengo ni kupata mawazo mapya ili huenda ukayafanyia kazi na kupata kitu kipya. Soma sana vitabu vya watu mashuhuri, pitia sana blog za watu maarufu hasa ambazo zinajihusisha na mambo kama yako.
TAHADHARI !!
Epuka kunakili machapisho ya wengine kwani injini pekuzi kama GOOGLE huwa zinatambua kuwa chapisho hilo lilichapishwa kwa mara ya kwanza mahala gani. Na pia blog yako inaweza kushushwa viwango mara moja.
Hizi hapa ni hasara za kunakili (kukopy) makala kutoka blog nyingine
Soma
4. ANZA KUANDIKA
Si ulikuwa hujui cha kuandika? Si umetoka nje umetulia sehemu? Basi anza kuandika kuhusiana na chochote unachokiona.
Andika kuhusu chochote ambacho kinakujia katika akili yako. Andika, andika kisha andika tena na tena. Kadiri unavyoandika ndivo fikra za kuandika zinavyo kaa sawa na hatimaye kuandika vitu vya maana zaidi.
ZINGATIA HAYA WAKATI UNAANDIKA WAZO
* Wazo ambalo utalipata liandike mpaka umalize
* Ukipata wazo jipya liandike pembeni kisha endelea na wazo la awali kwanza
* Siku zote ubongo wako ni adui yako. Hivyo jitahidi kujizuia na mambo ya starehe ambayo ubongo wako utataka wakati unaandika mawazo yako. Kama vile kuperuzi katika mitandao ya kijamii, kuangalia video n.k.
Lakini unaweza kuwa umepata kitu cha kuandika lakini vile vile ukafeli kwa sababu hujaandika katika mtiririko ambao unaweza kumvutia msomaji wako.
Nimeona nisikuache hivi hivi. Hapa chini nimekuwekea njia za kuandika makala bora na msomaji wako akavutiwa nayo;-
Soma hizi
COMMENTS