MARUBANI HUJIBURUDISHA NA NINI WAWAPO SAFARINI? (FAHAMU MAMBO 10)

Huwa unajiuliza marubani wa ndege wanakabiliana vipi na uchovu wa safari kwa zaidi ya masaa 10?

 Je ni kwa muda wote huo wanakuwa kwenye usukani?

Lakini ndege za siku hizi kuna mahala unaweza kuweka mfumo automatic wa uendeshaji (Auto pilot) Je ? Kwa muda huo rubani anakuwa na kazi gani?

Ukweli ulioko ni kwamba nao kuna muda wana relax na kuburudika kwa mambo kadhaa.

Haya ni baadhi ya mambo 10 ambayo hukuyajua juu ya waongoza ndege (pilots) ambayo  mara nyingi hufanya ili kujiliwaza na uchovu wa safari ndefu.

1. Kucheza game

Wengi katika marubani hupenda kucheza game zinachochangamsha akili (puzzle) . Tofauti na kuangalia tv ama kusoma vitabu. Vitu ambavyo hupunguza umakini wa ubongo kwa wakati huo.


2. Kusikiliza radio / mziki

Rubani anaweza kujiburudisha kwa kusikiliza music ama kusikiliza radio katika headphone zake ambazo huzitumia kwa mawasiliano na waongozaji ndege walio chini.

 Headphone hizo zina uwezo wa kukata music ama radio pale ambapo kuna mawasiliano yamekuja kwa wakati huo.


3. Kujifunza zaidi

Mara  chache wanaweza kupata fursa ya kujifunza zaidi. Yaweza kuwa kujifunza lugha ngeni, sambamba na hilo pia wanaweza kuutumia muda huu kwa kujisomea zaidi masomo yao binafsi.


4. Kula

Kama tunavofahamu kuwa marubani hula vyakula vya aina tofauti ili kulinda afya zao ili itakapotokea dharura kwa mmoja wao hasa mchafuko wa tumbo basi mmoja anaweza kulifikisha salama gurudumu hilo. 

Hivyo marubani wawapo safarini hula kama watu wengine (abiria)

Lakini yapo mengi ya kushangaza kuhusiana na usafiri wa ndege. Soma makala hii hapa chini kufahamu zaidi.

Soma

Mambo 20 usiyoyafahamu kuhusiana na usafiri wa ndege


5. Hufikiria juu ya hatari zinazoweza kujitokeza

Kama umewahi kupanda ndege bila shaka umeshawahi kuwaza juu ya chochote kibaya ambacho kinaweza kutokea. Ama sivyo?

Basi huko peke yako juu ya hofu hiyo, marubani wako nao huwaza hilo hata pale ambapo hakuna dalili ya hitilafu yoyote. Lazima wafahamu mahala walipo wako karibu na uwanja gani wa ndege ili ikitokea hitilafu wakimbile hapo mara moja ili kuokoa maisha yako.


6. Kubarizi na Kuchungulia dirishani

Ni kawaida kwa abiria awapo kwa muda mrefu katika ndege huchoka na kuamua kugeuza macho yake kutazama anga jinsi ilivyopambwa mawingi yake. Hali kadhalika kwa marubani kufanya hivi zaidi. 


7. Umbea kidogo

Kama ilivyo kwa wafanyakazi wowote wenye mafungamano mazuri, lazima kuna muda kazi zinapopungua kuzua umbea wa mawili matatu. Aidha kuhusiana na muajiri wao au vinginevyo,

Marubani nao ni watu kama wewe na kuna muda wanatamani kufanya mambo ya kijamii kama hayo. Sikwambii sasa kwa marubani wa kike.


8. Kupitia ratiba yao ya safari

Kwa sasa i pad imekuwa maarufu kwa marubani. Wachilia mbali matumizi mengine lakini pia huunganishwa na mifumo maalum ya ratiba yake ya ndege. Hivyo wakati akiwa angani kuna baadhi hupitia ratiba yake ya safari na kujua nini kinatakiwa kufanyika katika muda huo au baadaye.


9. Kulala

Ndege ziko tofauti. Lakini baadhi ya ndege kubwa za masafa  marefu huwa na vitanda vya siri kwa ajili ya waongoza ndege (pilots)

Vitanda hivi vipo katika vyumba maalum ambavyo havipo mbali sana na chumba cha V I P. Lakini pia mbali na vyumba vya kupumzikia pia zipo bafu, vyoo na kadhalika.


10. Kujipiga picha (Selfie)

Mara nyingi hufanya hivyo pale ambapo wanakuwa huru safarini. Ingawa si ruhusa kwa abiria kuingia kwa rubani (cockpit) ila kwa ruhusa maalum.

Vipi kuhusu picha inayoonekana hapo juu?

Picha hiyo inamuonesha rubani mmoja Raia wa nchi ya Brazi anayejulikana kwa jina la Daniel Contino akiwa ametokeza mwili wake nje akiwa hewani na kujipiga picha. Ukweli wa picha hiyo ni kwamba  imefanywa kutengenezwa (photoshop) na haina uhalisia wowote na ni jambo lisilowezekana kabisa.

Umepata mwangaza kidogo? Au una cha kuongezea? Basi usisite kutuachia maoni yako hapo chini

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MARUBANI HUJIBURUDISHA NA NINI WAWAPO SAFARINI? (FAHAMU MAMBO 10)
MARUBANI HUJIBURUDISHA NA NINI WAWAPO SAFARINI? (FAHAMU MAMBO 10)
https://1.bp.blogspot.com/-VUrvOl-7-no/X74c5J7LcLI/AAAAAAAAa9M/xtnlksyvcq8xJAuz4VHPpo6Ony60NQ4mQCLcBGAsYHQ/w320-h251/pilot-fake-mid-flight-selfies-instagram-daniel-centeno-1-59b244246ed58__700.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-VUrvOl-7-no/X74c5J7LcLI/AAAAAAAAa9M/xtnlksyvcq8xJAuz4VHPpo6Ony60NQ4mQCLcBGAsYHQ/s72-w320-c-h251/pilot-fake-mid-flight-selfies-instagram-daniel-centeno-1-59b244246ed58__700.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/11/usichokijua-kusu-nini-marubani-hufanya.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/11/usichokijua-kusu-nini-marubani-hufanya.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content