Binafsi sikuwa nazifahamu hizi nafaka. Nilipokutana nazo na kuonja ladha yake nilizipenda na kuanza kuzifuatilia faida zake.


"FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA ALMONDS"
1. Uboreshaji wa meno na mifupa
Almonds zina vitamin na madini kama calcium, magnesium, manganeze, copper, vitamin K na zink. Madini haya huimarisha mifupa na meno kwa ujumla.
2. Husaidia kwa wenye kisukari
Nafaka hizi zina mafuta na asidi ambazo zina kazi muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Husawazisha kiwango cha sukari kwenye damu na kudhibiti jinsi inavotumiwa na mwili. Kwa maana kwamba mlozi unaweza kusawazisha vema kiwango chako cha sukari mwilini.
3. Hupunguza unene & uzito
Unene hutokana na vyakula ving vya mafuta na sukari ambayo huzalisha cholestrol kwa wingi. Lakini Mlozi zina nyuzi nyuzi na mafuta ya asili ambayo hupunguza mafuta ya ziada mwilini. (mafuta yaliyozidi)
Soma
4. Huzuia saratani
Kutokana na kuwa na vitami E, huzuia seli za kansa kuenea. Hii ni kwa wale wanaozitumia mara kwa mara. Sambamba na hilo, pia kutokana na vitamin E kupatikana kwa wingi ndani ya almonds imekuwa ni tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya moyo
Lakini pia watu wenye saratani hushauriwa kutafuna karanga na korosho.
5. Huimarisha ubongo
Hapa tunazungumzia uwezo wa kufikiri na kumbukumbu nzuri. Hii ni kutokana na madini ya riboflavin na L carnitine ndio hufanya ubongo wako kuwa imara na kupunguza hatari ya kupata mtindio wa ubongo.
Soma pia
Hizi ni faida chache katika nyingi ambazo hutokana na kula almonds. Kama una maoni tuandikie hapo chini sehemu ya COMMENTS
COMMENTS