FANYA MAMBO MATANO (5) KABLA HUJAINGIA MWAKA 2021


Maandalizi husaidia sana katika kufika malengo ya mtu kuliko mtu ambaye hana maandalizi. Kuna mambo matano ambayo ni muhimu kuyafanya kabla hujaingia mwaka 2021.


1. SAMEHE

Japo ni jambo gumu sana kusamehe kila kosa lakini unatakiwa ujijengee tabia hio. Mtu ambaye hana kawaida ya kusamehe mara nyingi huumia kuliko yule ambaye anatakiwa amsamehe.

 Maana ukimuona unachukia wakati yeye hana habari nawe. Mwisho wa suku utajikuta una maumivu sana kuliko yeye. Usimchukie kila mtu hata amekufanyia makosa. Maana ndivyo maisha yalivo. Jenga tamaduni ya kusamehe. Hivyo kabla ya kufika mwaka 2021 ni vyema kuwasamehe wale wote ambao walikukosea kwa namna moja au nyingine.


2. KUWA MWANAFUNZI HURU

Jaribu kujifunza kwa kila mtu. Usiridhike na elimu uliyonayo. Huenda unajiona kuwa umesoma sana labda una PHD, DEGREE, DIPLOMA na kadhalika lakini tambua kwamba mwanadamu anatakiwa kujifunza mpaka anakufa. Dunia kila siku ina mambo mapya. Jitahidi kukijua kila kitu kizuri ambacho una uwezo wa kukifahamu.

Jiwekee muda wa kusoma vitabu, jiwekee muda wa kusoma kutoka wa wengine kwani utakuwa na maarifa mengi sana. Jitahidi kuwa mwanafunzi huru kabla mwaka 2020 haujaisha.

Soma

Faida 7 za kusoma vitabu

Maarifa humjenga mtu zaidi kuliko mtu ambaye amekosa maarifra.


3. FIKIRI KUHUSU KUSUDIO LAKO

Fikiria zaidi kuhusu  kusudio lako na kuanza kulielekea kusudio hilo. Kile ambacho kiko katika akili yako na matamanio yako. unatamani kuwa nani? unatamani kufanya nini? je ni kitu gani unatamani kuwa nacho ili ufike pale ambapo unataka kufika?

Anza sasa kulielekea kusudio na mawazo yako na uanze kuyafanyia kazi sasa. jitahidi kutekeleza japo kidogo kidogo na hatimaye utafikia ndoto yako.


4. SHUGHULIKA NA JICHO LAKO

Usishughulike na macho ya watu, shughulika na jicho lako. Usitazame kuwa nikifanya hivi fulani ataniaonaje, cha muhimu ni kutazama je? ninachokifanya ni sawa?, na kitanifikisha malengo yangu? lakini usiumizwe na maisha ya watu kwani unafanya kwa ajili yako na sio kwa ajili ya kuwafurahisha watu.

Jitazame wewe usiwatazame wengine.


5. JIANDAE NA CHANGAMOTO

Mwanadamu hawezi kuwa mwanadamu bila ya changamoto, ingawa akili zimeumbwa kuzichukia. Lakini uhalisia wa mafanikio yetu ni mpaka kupitia changamoto.

Ili ung'are ni mpaka upitie changamot nyingi. Utasemwa, utadharauliwa, utatukanwa lakini usikimbe. Vumilia na tafuta utatuzi wa hizo changamoto zako.

Yafanyie kazi mambo haya kabla mwaka huu haujaisha na utaona mafanikio yake. Na kwa uwezo wa MUNGU utauanza mwaka mwingine kivingine.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: FANYA MAMBO MATANO (5) KABLA HUJAINGIA MWAKA 2021
FANYA MAMBO MATANO (5) KABLA HUJAINGIA MWAKA 2021
https://1.bp.blogspot.com/-QDmz8F_fKZE/X9dra0APnaI/AAAAAAAAbgs/pRQXyqaHDaIIvj9CZFxtoGh3jpPHKYNKQCLcBGAsYHQ/s320/challenge.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-QDmz8F_fKZE/X9dra0APnaI/AAAAAAAAbgs/pRQXyqaHDaIIvj9CZFxtoGh3jpPHKYNKQCLcBGAsYHQ/s72-c/challenge.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/12/fanya-mambo-matano-5-kabla-hujaingia.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/12/fanya-mambo-matano-5-kabla-hujaingia.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content