MAMBO 16 USIYOYAFAHAMU KUHUSU NCHI (KONGWE) YA UGIRIKI


Kwa jina jingine hujulikana kama Uyunani. Huyu ndiye mama wa nchi za Ulaya (Europe). Nchi hii inapatikana upande wa kusini mashariki mwa Bara la Ulaya. Nchi hii imepakana na nchi ya Albania, Macedonia ya Kaskazini, Bulgaria na Uturuki. Lakini pia imepakana na Bahari ya mediteranea.

Nchi ya Ugiriki ilipata Uhuru wake mwaka 1821. Ni nchi inayokadiriwa kuwa na watu milioni 10. Mji wake Mkuu unaitwa ATHENS.

Asilimia kubwa ya nchi hii imetawaliwa na ardhi yenye milima.

Wagiriki wamewahi kuitawala Ufaransa, Uturuki na Urusi.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kushangaza ambayo huenda huyafahamu kuhusiana na nchi hii (Ugiriri / Uyunani)


1. Ndio nchi ya kwanza kuanzisha Demokrasia

Hii ndio nchi ya kwanza kuanzisha mfumo wa demokrasia kwa kuruhusu watu kupiga kura. Mfumo huu ulianzishwa tangu Karne ya 5 kwa kuchagua viongozi. 

Lakini mfumo huu ulikuwa ni kwa baadhi ya watu ambao ni wanaume na watu wazima tu. Wanawake hawakuruhusiwa kupiga kura enzi hizo.


2. Lugha ya ki giriki ni lugha Kongwe

Lugha ya Kigiriki ndio lugha kongwe zaidi duniani inayoandikwa ambayo bado inatumika mpaka sasa. Huwezi kuzitaja lugha kongwe duniani bila kuitaja lugha hii. 

Ni lugha ambayo ilikuwepo tangu zaidi ya miaka 5000 iliyopita mpaka leo.


3. Ni Ugiriki au Uyunani?

Jina halisi la nchi hii ni Uyunani na sio Ugiriki kwani hili sio jina halisi.


4. Asili ya neno "Music"

Neno music asili yake ni jina la Kigiriki ambalo maana yake ni Mungu wa sanaa katika imani za Wagiriki.


5. Watalii ni wengi kuliko raia

Kutokana na vivutio vyake na ukongwe wake, nchi hii imekuwa ikitembelewa sana na watalii kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Idadi ya watalii kwa mwaka ni nyingi kuliko idadi ya raia wake. Kwani inakadiriwa kutembelewa na watu zaidi ya milioni 16 wakati idadi ya raia ni milioni 10 kama tulivosoma hapo awali.


6. Athens ni mji mkongwe zaidi barani Ulaya

Mji mkuu wa nchi hii (Athens) ndio mji mkongwe zaidi barani Ulaya kwani ulianza kukaliwa miaka 7000 iliyopita na ndio kitovu cha ustaarabu wa Ulaya sambamba na siasa, falsafa, michezo, fasihi, historia na kadhalika.

Pia zaidi ya asilimia 40% ya Wagiriki huishi katika Mji huu. 

Athens - Mji mkuu wa Ugiriki


7. Mafuta ya mzeituni hupatikana kwa wingi

Ugiriki ni miongoni mwa nchi zinazozalisha mafuta ya mzeituni kwa wingi na kuna baadhi ya miti ilipandwa toka karne ya 13 hadi leo na bado inazalisha.


8. Alexander The Great 

Huyu ndiye kiongozi wa kwanza kuweka sura yake kwenye sarafu yao. Kabla ya hapo walikuwa wakiweka Miungu yao.


9. Raia wake hupenda mapenzi zaidi

Hii ndiyo nchi inayoongoza kwa raia wake kufanya mapenzi Duniani ikifuatiwa na nchi ya Brazil.


10. Ukiwa Ugiriki Kuwa makili katika

Usimsalimie mtu  kwa kumpungia mkono huku ukiwa umechanua kiganja chako. Kwani ishara hiyo kwa upande wao ni matusi. Kunja kiganja kisha ndipo mpungie mtu mkono.


11. Ina visiwa lukuki

Nchi hii inakadiriwa kuwa na visiwa zaidi ya 2000, wakati vinavyo kaliwa na watu ni 170 tu.

Yako mengi ya kufahamu kuhusu nchi ya Ugiriki.

 Endelea na makala hii na usisahau kutuandikia maoni yako sehemu ya chini katika COMMENTS

12. Unaambiwa asilimia 10 ya wagiriki hawana ajira. Hata ukiwa msomi ni ngumu kupata ajira.

13. Asilimia 7 ya marumaru Duniani kote hutokea Ugikiri.

14. Hii ndio nchi yenye kiwango kidogo cha talaka barani Ulaya pamoja na kuwa na kiwango kikubwa  cha utoaji mimba kwa wanawke.

15. Michezo ya Olimpiki ilianzia nchini humo na ilikuwa ni mwaka 1896.

16. Raia wa Ugiriki ni lazima kupiga kura na sio hiyari. Kuanzia umri wa miaka 18 mtu anatakiwa kupiga kura.

Asante kwa kuwa nasi,  unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii kama inavyooneshwa hapo chini. 

 

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MAMBO 16 USIYOYAFAHAMU KUHUSU NCHI (KONGWE) YA UGIRIKI
MAMBO 16 USIYOYAFAHAMU KUHUSU NCHI (KONGWE) YA UGIRIKI
https://1.bp.blogspot.com/-BIi-6dFVtmo/YAvbjLaXnvI/AAAAAAAAb0k/QptaArwEIuMHT3nXxAkJ-livwHpL5qADQCLcBGAsYHQ/s0/greece.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-BIi-6dFVtmo/YAvbjLaXnvI/AAAAAAAAb0k/QptaArwEIuMHT3nXxAkJ-livwHpL5qADQCLcBGAsYHQ/s72-c/greece.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/12/mambo-15-usiyoyafahamu-kuhusu-nchi.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/12/mambo-15-usiyoyafahamu-kuhusu-nchi.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content