MAZOEZI 6 YA KUONGEZA ONGEZA NGUVU ZA KIUME

Pamoja na vyakula lakini yapo mazoezi ambayo kama utadumu nayo ni tiba kubwa juu ya tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.

Neno "nguvu za kiume" huhusisha mambo mengi ikiwemo - Hamu ya kufanya mapenzi, kusimama kwa uume vizuri, kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo, uwezo wa kurudia tendo, pumzi ya kutosha na mengineyo.

Hivyo ni kwamba kuna viungo vingi katika mwilini ambavyo huhusika na jambo hili. Viungo hivyo ni pamoja na Ubongo, moyo, mapafu, mishipa, mirija ndani ya uume na kadhalika.

Kwahiyo kukosa nguvu za kiume hutokea pale ambapo moja kati ya viungo hivyo havifanyi kazi ipasavyo.

Kuna mambo kadhaa yanayosababisha ukosefu wa nguvu za kiume kwa mfano kupatwa na maradhi, vyakula unavyokula na mtindo wa maisha. Baadhi ya maradhi hayo ni ugonjwa wa sukari, presha ya kupanda, presha ya kushuka.

Tabia zinazosababisha viungo kutofanya kazi ni kama uvutaji wa sigara, kuchelewa kulala, kutopata usingizi, unywaji wa pombe, utumiaji wa madawa ya kulevya  au kufanya kazi kupita kiasi na kukosa wakati wa kupumzika. 
Sababu nyingine ni kama kutumia nguvu nyingi kusukuma choo kwa sababu ya tatizo la kusukuma choo, kutokunywa maji, uzito mwingi, kitambi na hasa kutofanya mazoezi
Tatizo la choo kigumu hutokana na matatizo katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Soma

Makala iliyopita tulizungumzia kuhusiana na Vyakula vinavyo ongeza nguvu za kiume. 

Pamoja na vyakula lakini yapo mazoezi ambayo kama utadumu nayo ni tiba kubwa juu ya tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.

Mazoezi katika ujumla wake yana umuhimu mkubwa sana katika kujenga afya ya mwili wako. Na mtu ambaye hajishughulishi na mazoezi walau kidogo yupo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa kama presha, kisukari na kadhalika.

Soma 

Faida 20 za Kufanya mazoezi

Yafuatayo ni baadhi ya mazoezi yenye uwezo wa kuimarisha uwezo wa nguvu za kiume na kuweza kudumisha ndoa / mahusiano yako;-


1. SQUATTING

Hili ni zoezi la kuchuchumaa na kusimama (mara nyingi)

Unaambiwa hili ndilo zoezi linalokubalika zaidi katika kuongeza nguvu za kiume kwani husaidia kuimarisha misuli katika eneo lako la chini ya mwili kuanzia tumbo (sixparks), mgongo hadi miguuni.

Ukiwa na utaratibu wa kufanya zoezi hili kila siku sahau kuhusu kitambi kwakuwa huimarisha misuli ya tumbo.

Lakini pia kwa asilimia fulani zoezi hili husaidia kuchoma mafuta mwilini.

Chuchumaa na kusimama mara 15 hadi 20 kisha pumzika kwa dakika moja na unendelee tena. Fanya hivyo kwa mizunguuko mitano. Kadiri siku zinavozidi kwenda utazidi kuimarika na unaweza kuongeza kwa kubeba kitu kingine kizito ingawa sio lazima sana.

Wakati unafanya zoezi hili unaweza kuweka mikono yako shingoni, kiunoni au kuinyoosha mbele kisha unachuchumaa mpaka unakaribia kugusa visigino. Kumbuka kuwa usisimame na vidole. Simama na mguu wote (unyayo)


2. KUTEMBEA KWA MIGUU

Karibu kila mtu mwenye utimamu wa mwili na afya anaweza kufanya zoezi hili. Unaweza kufanya muda wowote na sehemu yoyote. Lakini sehemu bora ya kutembea ni sehemu ya wazi yenye hewa safi.

Sambamba na hilo pia zoezi hili unaweza kulitumia kama unataka kupunguza uzito. Tembea kwa muda wa dakika 60 bila kupumzika (kila siku asubuhi na jioni)


3. PUSH UP

Nafikiri hili ni zoezi maarufu ambalo watu wengi hulifahamu namna ya kulifanya.

Ingawa ni zoezi gumu kulifanya lakini husaidia kuongeza msukumo wa damu mwilini hivyo huimarisha sana uwezo wa nguvu zako za kiume.

Sambamba na hilo lakini pia huimarisha misuli ya mikono, mabega kifua na tumbo.

Kama ndio mara yako ya kwanza unaweza kuanza na push up 5 hadi 10 huku unaongeza idadi kadiri unapopata uzoefu.

Si lazima kukunja ngumi na kuumiza vidole vyako kwani lengo letu si kukomaza vidole vya mikono (nakoz) ila kama kuna sababu nyingine unaweza kufanya hivyo.

Hakikisha umenyoosha miguu yako vizuri kisha nenda chini lakini usilale katika ardhi, kisha rudi juu. Na hiyo inahesabika ni pushapu moja.

Wakati wa kunyanyuka usitangulize kichwa wala kiuno. Hakikisha unakwenda mwili mzima na unarudi hivyo hivyo


4. JOGGING

Tofauti na kutembea, hii ni kukimbia kwa mwendo mdogo mdogo maarufu kama jogging. Hili ni miongoni mwa mazoezi ambayo husaidia kwa haraka sana msukumo wa damu mwmilini.

Zoezi hii pia huimarisha misuli ya miguu (vigimbi) na kuongeza pumzi. Misuli imara ya miguu ni muhimu sana katika suala la mzunguko mzuri wa damu.5. KUOGELEA
Kuogelea ni kitendo cha kuingia katika maji mengi na kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kutembea chini.

Unapoogelea misuli ya miguu na mikono huongezeka kutokana na ile nguvu unayotumia. Hivyo mishipa ya damu ni lazima ipeleke damu nyingi sehemu zote za mwili.

6. PUMZIKA / LALA
Hili si zoezi lakini nimeliweka hapa kwa sababu ni lazima liendane na mazoezi tajwa hapo juu. Baada ya mazoezi yako mwisho wa siku ni lazima utahitaji muda mzuri wa kupumzika.

MUHIMU
Mazoezi hayo hapo juu ni lazima yafanywe kila siku ili kupata matokeo yaliyokusudiwa. Unaweza kuchagua zoezi moja ambalo ni rahisi kwako na kutenga muda wa kulifanya kila siku na utaona matokeo yake.

Lakini kwa ambao wana matatizo makubwa zaidi ya ukosefu wa nguvu za kiume ni vizuri kupata ushauri wa daktari.

COMMENTS

BLOGGER: 16
 1. Vip tatizo la kuwahi kufika kileleni, linaondolewaje??

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kama ukipata muda unaweza kunitafuta mkuu. KWA maelekezo zaidi🙏🙏 0625 718040

   Delete
  2. Mbna sikuoni Mkuu whatsapp

   Delete
  3. NAPATIKANA KWA NAMBA HII - 0625 71 80 40

   Delete
 2. Ukifanya zoezi la kuchuchumaa nasimama misuli ya uume inakakama ndo matokeo?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nimiongoni mwa mazoezi yanayoimarisha sana nguvu za kiume mkuu

   Delete
 3. Replies
  1. Mazoezi ni muhimu na yana mchango mkubwa sana. Lakini kama tatizo ni kubwa iko haka ya kutumia dawa za asili

   Delete
 4. Naomba kusaidiwa namna ya kuimarisha misuli ya uume has a baada ya mpigo mmoja

  ReplyDelete


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MAZOEZI 6 YA KUONGEZA ONGEZA NGUVU ZA KIUME
MAZOEZI 6 YA KUONGEZA ONGEZA NGUVU ZA KIUME
Pamoja na vyakula lakini yapo mazoezi ambayo kama utadumu nayo ni tiba kubwa juu ya tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.
https://1.bp.blogspot.com/-mpvZW_WOifk/X9dPcEGWm0I/AAAAAAAAbgY/tqjvDvBgAhgJQtG0_Z4VrK3VpBQzkKnNQCLcBGAsYHQ/s320/nguvu%2Bza.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-mpvZW_WOifk/X9dPcEGWm0I/AAAAAAAAbgY/tqjvDvBgAhgJQtG0_Z4VrK3VpBQzkKnNQCLcBGAsYHQ/s72-c/nguvu%2Bza.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/12/mazoezi-6-yanayo-ongeza-nguvu-za-kiume.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/12/mazoezi-6-yanayo-ongeza-nguvu-za-kiume.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content