
Nachomeka hii huk, ikikuchoma yahusu
Nimesha chanjia muk, nakunywa al kasusu
Ushamba wa face book, ndilo somo lina husu
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Ni ushamba na ujinga, wacha ikikupendeza
Wengi wao watapinga, kuona nawachunguza
Mapema sipojikinga, hii itakupoteza
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Asubuhi kukikucha, Mimacho mtandaoni
Tayari kutuma picha, Hata uko msalani
Tongo macho hujafuta, Ndugu hebu jithamini
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Eti watafuta demu, huko hakuna wandele?
Ukosefu wa elimu, ushamba peleka mbele
Juzi umepata simu, basi kutwa makelele
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Kila mwanamke “MAMBO”, mara nipe namba yako
Linakera hili jambo, ijue thamani yako
Utakuja chapwa fimbo, wengine ni dada zako
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Ukigombana na mwenza, tayari umesha posti
Siri zako basi tunza, mitambo itakukosti
Kwani we ndio wa kwanza, wacha hayo mambo shosti
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Kidari chenyewe huna, kutwa upo tumbo wazi
Mbavu mbili zimetuna, kama kitoto cha mbuzi
Heri kaka kuuchuna, Ulimbukeni ni kazi
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Eti 'shea picha hii', kasha nitakupa namba
Unaleta usanii, uliojaa ushamba
Nawe watia bidii, heti wataka mchumba
Huko kwenu bwana wewe, hakunaga wanawake?
Tupu yako mali yako, na unayemuamini
Usiifanye ni jiko, lisilojua thamani
Dada uendako siko, jaribu kujithamini
Neno langu si sheria, maoni yaruhusiwa
Mimi natukana mamba, na ng’ambo nitatoboa
Tena natunga naimba, nawe utaitikia
Baba huo ni ushamba, jifunze unapotea
Aaaaaaaa uo ni ushamba.
COMMENTS