PASSWORD 5 AMBAZO NI RAHISI KUIBIWA NA WADUKUZI

----------------------
Password / Nywila /Neno la siri

Limeitwa neno la siri kwa sababu huficha mambo binafsi ya mtu katika jambo lake. Na halitakiwi kwa mwingine yeyote kulifahamu (bila idhini yake) Kitendo hiki ni kuingilia faragha ya mtu mwingine na ni makosa kisheria.

Wadukuzi ni wataalamu wa mtandao ambao mara kadhaa hujaribu kuingia kwa njia za kitaalamu katika akaunt ya mtu na kufanya uhalifu. Udukuzi huo unaweza kuwa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, instagram, twitter lakini pia barua pepe na hata account za benk.

Burudika na shairi

Mshamba wa facebook

Pamoja na kwamba kuibiwa account yako yaweza kuwa ni jambo baya, ila kuna aina za password ambazo kama utazitumia ni rahisi sana kwa wadukuzi kukuibia account yako.

Tazama baadhi hapa

1. Namba

Baadhi ya watu hupenda kutumia namba hasa namba ambazo zina mtiririko maalum na ambazo ni rahisi kukaririka ili isiwe rahisi kusahaulika. mfano wa namba hizo ni kama vile 12345, 123123, 987654, 


2. Majina

Imekuwa ni kawaida mtu kutumia jina lake kama neno yake la siri. Hii ni rahisi kwa mtu kubuni neno lako na kuweza kukuibia akaunti yako.


3. Maneno maarufu

Baadhi ya watu hutumia maneno maarufu katika jamii kama neno lake la siri. Mfano - i loveyou, welcome, password.

Sambamba na hilo pia baadhi ya watu hutumia maneno ya dini kama vile GOD, ALLAAH, JESUS.

Wengine wakaenda mbali zaidi kwa kutumia matusi makubwa makubwa ambayo nadhani unayafahamu kama maneno yao ya siri katika akaunti zao mbali mbali. Hii ni rahisi kwa mtu kubuni na kupatia.


4. Maneo maarufu

Wengine hutumia maeneo maarufu aidha ya Miji mikubwa, maziwa, majengo maarufu lakini pia hata mitaa yao.


5. Namba ya simu

Nadhani hasa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook watu wengi hasa ambao hujiunga kwa kutumia namba zao za simu badala ya barua pepe hufanya mambo haya.

Anaweza kutumia namba yake ya simu kwa kuweka namba za mwisho au namba za kwanza. Nadhani hii ni njia rahisi zaidi kwa wadukuzi kukuibia akaunti yako.

Soma pia

Mambo 10 yatakayo kushangaza kuhusu kangaroo

Baada ya kusoma dondoo hizi chache unaweza kuchukua hatua kama unaona neno lako la siri linalingana ama kuendana na mada hii.

"Weka neno la siri ambalo unahisi linaweza kuwa la pekee. Unaweza kufanya neno lako la siri kuwa maandishi yasiypfikirika kwa haraka ikifuatiwa na tarakimu"

Udukuzi ni hatari kwani hujui aliyeiba akaunti  yako anataka kuifanyia nini, lakini pia anakuwa amekurudisha nyuma kimaendeleo.

Tunaomba maoni yako sehemu ya comment hapo chini kwa ushauri, maoni na mapendekezo.


COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: PASSWORD 5 AMBAZO NI RAHISI KUIBIWA NA WADUKUZI
PASSWORD 5 AMBAZO NI RAHISI KUIBIWA NA WADUKUZI
https://1.bp.blogspot.com/-XQcI6H0W9v8/X-2M0bLBOiI/AAAAAAAAbqI/VmIUAwoRggsd8EjHRcZmKMk9dbT7ZEtUACLcBGAsYHQ/s320/online-password-hacker.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-XQcI6H0W9v8/X-2M0bLBOiI/AAAAAAAAbqI/VmIUAwoRggsd8EjHRcZmKMk9dbT7ZEtUACLcBGAsYHQ/s72-c/online-password-hacker.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/12/password-5-ambazo-ni-rahisi-kuibiwa-na.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/12/password-5-ambazo-ni-rahisi-kuibiwa-na.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content