
Miongoni mwa sababu zake ni mfumo wa ulaji wa vyakula, Kutofanya mazoezi, msongo wa mawazo, kujichua kwa muda mrefu na kadhalika.
Vyakula hivi saba (7) vinaweza kurudisha uwezo wako wa nguvu za kiume na kuilinda ndoa yako. Kwani kukosekana kwa nguvu za kiume ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya migogoro ndani ya nyumba.
Anza leo kubadilisha mfumo wako wa vyakula na kutumia zaidi vyakula hivi ambavyo nimekuorodheshea hapa chini
1. UGALI WA DONA
Achana na mazoea ya kula vyakula vilivyo kobolewa kama ugali wa sembe na kadhalika. Ugali wa dona na nafaka ambazo hazijakobolewa zina virutubisho na ambavyo ni muhimu kwa afya ya mwanaume.
Ikiwa ladha ya dona inakuchosha unaweza kuchanganya na ngano kisha kusaga pamoja. Hii huufanya ugali wako kuwa mlaini na mtamu zaidi. Fanya hivi katika utaratibu wa vyakula vyako vya kila siku utaona mabadiliko.
2. KITUNGUU SWAUMU
Tafuna punje kadhaa za kitunguu swaumu kisha kunywa na maji yasiopungua glasi 3. Punje zaweza kuwa 8 hadi10.
Kula hivi mara mbili kwa siku. Lakini pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama kiungo kingine katika vyakula vyako vingine.
3. CHUMVI YA MAWE
Chumvi ya asili ambayo bado haijapitia kiwandani, ni ile chumvi ambayo imetoka moja kwa moja baharini. Tumia chumvi hii katika vyakula vyako vya kila siku. Ni tiba kubwa ya tatizo hili la nguvu za kiume.
4. MBEGU ZA MABOGA
Unaweza kutafuna zikiwa mbichi unaweza kuzikaanga bila kuziunguza. Tafuna takriban punje mia moja kwa siku mara tatu. Fanya hivi ndani ya mwezi mmoja na matokeo yatakuwa mazuri zaidi
Lakini pia sifa ya mbegu hizi ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (sperms) kama una tatizo hili hii ndio njia sahihi.
5. TIKITI MAJI
Kula vipande vya tikiti maji kila siku huku ukitafuna na mbegu zake. Chagua tikiti lilioiva vizuri.
6. MAJI
Kunywa maji mengi kila siku. Unatakiwa usikose glass 8 hadi 10 kwa siku moja. Maji ni muhimu katika kuufanya mzunguko wa damu kuwa vizuri.
Je? wewe ni mvivu wa kunywa maji? Fahamu umuhimu wake mwilini na mbinu ambazo zitakufanya unywe maji mengi zaidi.
Soma
MBINU 5 ZITAKAZOKUFANYA UNYWE MAJI MENGI ZAIDI
7. ASALI NA MDALASINI
Chukua asali lita moja, changanya na mdalasini wa unga vijiko vinne. Kula kijiko kimoja kila unapokwenda kulala. Hii ni tiba nzuri sana fanya kwa mwezi mmoja utaona matokeo yake mazuri.
8. CHAI YENYE TANGAWIZI
Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Na nguvu za kiume hutegemea zaidi msukumo wa damu na mtiririko mzuri, kwa hiyo tangawizi ni moja kati ya njia mujarrabu sana.
Unaweza pia kutafuna tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo au kunywa chai yenye tangawizi nyingi.
Unashauriwa unapokunywa chai ya tangawizi usiweke kiungo kingine chochote (kama majani na kahawa). Pia ni vizuri badala ya sukari ukaweka asali
COMMENTS