IDEA 26 BORA KWA WANAOTAKA KUANZISHA YOUTUBE CHANNEL - 2

Wasiliana na Mwandishi wa Makala hii kwa namba - 0625 71 80 40

 

(SEHEMU - 2)

Kwa bahati mbaya kama umeikosa sehemu ya kwanza nimekuwekea hapa chini. Ni vema kuanza na sehemu ya kwanza kisha utaendelea na sehemu hii ya pili.

Idea 26 Bora kwa wanaotaka kuanzisha youtube channel - 1

 Baada ya kuimaliza sehemu hiyo ya kwanza, sasa nakukaribisha kuendelea na sehemu hii ya pili.


16. KILIMO NA UFUGAJI

Labda unajihusisha na mambo ya shamba kwa kilimo au ufugaji. Hii pia yaweza kuwa fursa kubwa kwa kuanza kuwaonesha watu kile unafanya sambamba na kuwapa elimu.

Huu ni uwanda mkubwa kiasi kwamba kila mtu anaweza kusimama katika nukta ambayo ataona kwake ni nyepesi. Kinaweza kuwa kilimo kikubwa, kilimo kidogo, bustani au ufugaji wa wanyama na jinsi ya kuwahudumia.


17. ELIMU (DARASA)

Ingawa yote yaliopita hapo juu yamehusiana na elimu, lakini hapa tunazungumzia elimu ya shule. Unaweza kufundisha masomo ya darasani kwa level ambayo utakuwa na uwezo nayo.

Unaweza kuwa mwalimu wa chekechea, msingi, sekondari au hata chuo. Utaangalia upo vizuri katika somo gani hasa na kuanza kufundisha.


18. KUTOA HAMASA KWA JAMII

Unaweza kuita "Motivation speakers"

Wako vijana wana madini ambayo ukiyatumia unaweza kufanikiwa katika maisha yako. Sasa nawe kama una kitu unahisi unaweza kuongea na jamii na kukuelewa anza kwani wakati ni sasa.

Njia za kufuata ili uwe tajiri, Njia za kuacha ili ufanikiwe, marafiki wasiofaa, kukabiliana na changamoto za maisha n.k

Hivi ni vitu ambavyo vinahitajika sana na miongoni mwa wanaofanya vizuri katika sekta hii ni pamoja na Successfull network path na Joel nanauka.

Tunaendelea na somo letu ambalo ni

Idea / mawazo 30 kwa ambaye anataka kuanzisha channel ya youtube.


19. MTINDO WA MAISHA

Kwa kiingereza hujulikana kama 'life style'

Huenda maisha yako ni sehemu ya fursa. Huenda kuna kitu ambacho tunaweza kujifunza kupitia maisha yako ya kila siku. Tumia fursa hii kutuwekea katika channel yako ya youtube.

Kwa mfano wako watanzania ambao wanaishi nchi nyingine za mbali kiasi kwamba kule kila kitu ni kigeni kulinganisha na huku kwetu. Wao hutumia fursa ya kuishi kule kama darasa kwetu kwa sisi ambao hatujui kuhusiana na miji ya watu.

Lakini pia si lazima  uwe unaishi nchi za nje, popote ulipo lazima kuna kitu ambacho ukikifanyia kazi kinaweza kuwa fundisho wa wengine. Anza sasa wakati ni wako.


20. UREMBO

Hii point nimeiweka mbali lakini nadhani ilitakiwa iwe namba moja au mbili.

Bila shaka utakubaliana nami kuwa jamii zetu hupenda sana kupendeza. Hasa kwa upande wa dada zetu (wanawake).

Urembo una marefu na mapana yake, unaweza kuwa pengine ni msusi, mpambaji, mtu wa makeup, mshonaji wa nguo, mtengenezaji wa viatu na mengine mengi.

Huku utaweza kuwashika watazamaji wengi sana wa mtandao wa youtube hasa ukiwa unakwenda sambamba na fashion mpya.


21. UJASIRIAMALI

Unaweza ukawa na elimu ya ujasiria mali na matumizi sahihi ya pesa. Hii ni fursa kubwa kwa vijana ambao wana mitaji lakini hawajui nini cha kufanya.

Matumizi mabaya ya pesa na rasili mali nyingine ni vitu ambavyo huwakumba sana watu hasa vijana. Elimu ya jinsi ya kuviepuka vitu hivi ni muhimu na inahitajika sana katika jamii.


22. MOVIE NA TV SHOWS

Katika  upande wa filamu ni kila siku hutoka filamu mpya na watu kuifuatilia. Kama wewe ni mpenzi wa movie unaweza kuitumia fursa hii kwa watu kuwafafanulia kile ambacho wewe umekiona kwanza kabisa.

Lakini pia unaweza kutafsiri filamu ambazo zipo katika lugha nyingine za kigeni kama kiingereza,  kihindi, kikorea n.k.


23. PARODIES 

Tafuta sehemu ya mihadhara ya watu maarufu kama vile wasanii au viongozi, kisha unaweza kuvaa uhusika wao na kuigiza kwa kwa kutumia sauti zao. 

Watu wanapenda sana siku hizi kuona kitu hiki na hata ukipita katika mitandao ya kijamii kama tiktok na like ni lazima utakutana nazo (parodies).


24. MAMBO YA KIHISTORIA

Tunaishi katika dunia iliyojaa mambo mengi ya kihistoria. Kila kitu kina historia yake ambayo watu wengi hawaijui.

Unaweza kufuatilia na kuanza kuwaletea watu ili wajifunze na kuburudika pia.


25. BOOK REVEW

Kama ilivyo katika kufuatilia movie na video mpya, hapa unaweza kuwa unafuatilia vitabu vipya kisha kuvielezea na kurusha katika chennel yako ya youtube.

Ukizingatia ulimwengu tulionao watu wengi ni wavivu wa kusoma vitabu, hivyo ikitokea unawarahisishia watakupenda na kukufuatilia kila siku.


26. GAMES

Kama kuna suala ambalo limeiteka sana jamii basi ni GAMES. Kuna mamimilioni ya games mbali mbali na za viwango tofauti. Lakini pia kila siku zinatoka games mpya.

Unaweza kufuatilia game zinazotoka na kuanza kuzielezea namna ya uchezaji wake, changamoto zake lakini pia uzuri wake. Watu wa rika karibu zote huoenda sana kucheza magem. Unaweza kutumia fursa hii ya wazi wazi katika channel yako ya youtube.

Kwa kuongezea unaweza kusoma makala hii

Makosa 10 ya kuepuka kama una youtube channel

Kama una maoni tuwekee hapo chini kabisa ya bandiko hili. Asante kwa kutufuatilia

COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: IDEA 26 BORA KWA WANAOTAKA KUANZISHA YOUTUBE CHANNEL - 2
IDEA 26 BORA KWA WANAOTAKA KUANZISHA YOUTUBE CHANNEL - 2
Wasiliana na Mwandishi wa Makala hii kwa namba - 0625 71 80 40
https://1.bp.blogspot.com/-OfPs0uzdgGc/YA5okWW813I/AAAAAAAAb1Y/SgR8Duwqr3kr_MXjmkMua7hSm2ggny64gCLcBGAsYHQ/s0/niche.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-OfPs0uzdgGc/YA5okWW813I/AAAAAAAAb1Y/SgR8Duwqr3kr_MXjmkMua7hSm2ggny64gCLcBGAsYHQ/s72-c/niche.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/01/idea-26-bora-kwa-wanaotaka-kuanzisha.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/01/idea-26-bora-kwa-wanaotaka-kuanzisha.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content