IDEA 26 BORA KWA WANAOTAKA KUANZISHA YOUTUBE CHANNEL - 1

Wasiliana na Mwandishi wa Makala hii kwa namba - 0625 71 80 40

(SEHEMU - 1)

Kwa asilimia kubwa ulimwengu wa sasa umehamia katika matumizi ya mtandao ya internet ambako mambo mengi huendeshwa huko

Youtube ni miongoni mwa mitandao ambayo hutembelewa sana na watu kwa madhumuni mbali mbali ikiwemo kupata habari, kujifunza, kuburudika na kadhalika.

Huenda nawe unatamani kuanzisha channel yako ya youtube lakini hujui kitu gani uanze nacho. Hii ni hali ambayo inawakumba wengi hasa wenye kutaka kuanza tasnia hii.

Ukweli ni kwamba kuna mawazo (ideas) nyingi ambazo unaweza kuangalia ambayo unaiweza na kuanza leo kufungua channel yako ya youtube.

Hapa nimekuorodheshea idea 30 tu ambazo bila shaka zinaweza kukupatia mwanga katika jambo lako.

1. (NEWS) HABARI 
Watu wanahitaji kusikia yaliyojiri kutoka sehemu na kona zote za nchi na ulimwengu kwa ujumla. Hii inaweza kuwa fursa kwako kwa kuwapikia watu habari zilizojiri.

Unaweza kujikita katika aina fulani ya habari kama vile;-
(a) Zilizojiri (Breaking news)
(b) Habari za michezo (Sports)
(c) Habari za burudani (Entertainment)
Na nyinginezo nyingi.

Ni vema pia kuwa na elimu ya habari ili kuepuka makosa ya kisheria kutokana na nchi husika.

2. TOURS (SAFARI)
Safari na kusafiri sehemu tofauti inaweza kuwa ni mada ambazo unaweza kuzirusha katika channel yako ya youtube. Watu wanapenda kufahamu miji, vijiji na maeneo mbali mbali na utamaduni wake, vivutio, watu wake na kadhalika.

Watu wanapenda kutazama kabla ya kufika sehemu. Hivyo itumie fursa hii kama ni mpenzi wa kusafiri hata ikiwezekana nje ya nchi na kuchukua matukio ya maeneo husika.

3. AFYA
Kila siku watu wanaumwa na kutafuta suluhisho sehemu mbali mbali ikiwemo mitandaoni. Kwakuwa youtube ni moja ya mitandao ambayo hutembelewa sana, hivyo kama una utaalamu katika tasnia ya afya unaweza kuendesha darasa zako huko.

Lakini mbali na magonjwa, pia watu huhitaji kuweka miili yao katika afya njema. Hivyo unaweza kuzungumzia mambo mbali mbali ikiwemo kupunguza uzito, kitambi na kadhalika.

Ziko channel nyingi ambazo hufanya vizuri sana katika upande huu, miongoni mwako ni Bongoclass afya

4. TEKNOLOJIA

Katika upande wa teknolojia unaweza kuzungumzia kuhusu masuala mbali mbali ikiwemo habari mpya zinazohusiana na simu, kompyuta na kadhalika.

Watu wanapenda kujua undani wa vitu vinavohusiana na teknolojia, watu wanataka kujua kuhusu kuzuia virusi katika simu zao, program mpya na mambo mengine mengi kwani segment hii ni pana mno.

Tazama

Ujio wa simu mpya ya infinix NOTE 9


5. MAPISHI

Unaweza kupika?

Basi watu wengi wanapenda kula vizuri na kupika vyakula vipya kila siku. Kama una utaalamu juu ya mapishi anza sasa kuwafundisha watu.

Wanawake wengi wanapenda kupika lakini hawana walimu wa kuwafundisha ama kuona aibu kwenda kwa wataalamu. Hivyo atakapoingia katika channel yako atakuwa anajifunza mwenyewe kadiri ya uwezo wake.


6. VICHEKESHO

Kuna muda tunapenda kufurahi na kucheka ili kusahau shida zetu.

Je wewe una kipaji cha kuchekesha?  Basi unaweza kukitumia kwa kurekodi clip zako na kuziweka youtube kisha tukazifurahia.


7. MAPENZI NA MAHUSIANO

Watu kila siku wanakuwa na kuingia katika mahusiano. 

Watu kila siku wanaachwa na kuumizwa. Lakini pia sambamba na hilo watu huhitaji kuingia katika mahusiano mapya na kuhitaji ushauri wa kumaliza mawazo yao yanayowaumiza.

Kama utakuwa na elimu juu ya mapenzi, ndoa, mahusiano ni wakati wako sasa kuleta darasa hilo katika ulimwengu wa mtandao kila siku.


8. UMBEA WA WATU MAARUFU

Kama ijulikanavyo kuwa watu maarufu kama vile wasanii, wanasiasa, wafanya biashara nk huwa na watu wengi nyuma yao ambao huwapenda na kuwasikiliza. Mashabiki wao hufuatilia sana maihsa ya mastaa wao.

Hivyo basi kila kukicha wanapenda kusikia mapya kuwahusu. Yawe mazuri, mabaya au katika mtiririko wa kazi na maisha yao ya kawaida.

Kama una uwezekano wakupata habari zao kila siku hii ni sehemu nzuri ya kujipakulia maujiko kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa youtube.


9. MUSIC

Kama una kipaji cha kuimba unaweza kuutumia mtandao wa youtube kuwaburudisha watu. Fungua channel ya youtube na uweke kazi zako huko.


10. MUSIC UPDATES

Mbali na kuimba, pia unaweza kujihusisha na uchambuzi wa muziki mpya kutoka kwa wasanii mbali mbali. Unaweza kutoa ufafanuzi wa mziki kwa ujumla kama vile video, audio, washiriki, udhaifu ama ukubwa wake.

Hii inaweza kuambatana na kutoa kasoro ambazo zipo kwenye wimbo wa msanii sambamba na kuutangaza ukubwa wake aidha katika nchi husika ama dunia kwa ujumla.


11. MUSIC COVER

Hapa pia ni kwa mwenye kipaji cha kuimba. Lakini cover ni kitendo cha kuimba nyimbo ya mtu mwingine kwa mara nyingine.

Watu kadhaa wamefaulu katika hili baada ya kuonekana na watu maarufu wakiwa wanaimba cover za watu hao.


12. DANCING (KUCHEZA)

Inataka kufanana na music cover lakini hapa utakuwa unajihusisha na kucheza tu. Hizi ni miongoni mwa burudani ambazo watu hupenda sana hasa baada ya msanii mkubwa kutoa nyimbo.

Ukicheza vizuri una asilimia kubwa ya kuliteka soko la burudani hasa kwa wapenzi wa mziki mzuri.


12. INTERVIEWS

Hapa unaweza kujihusisha sana na interview za watu maarufu. Watu wanapenda kusikia mengi kutoka kwa watu wao.

Mfano wa watu ambao hufanya vizuri sana katika interview za watu maarufu ni pamoja na channel ya YAH STONE TOWN ya Salama Jabir na ZAMARADI TV na nyingine nyingi.


14. MIKASA YA MAISHA

Tunajua wazi kuwa maisha ni safari ndefu na watu wengi hupitia magumu. Yapo ya kujifunza, kustaajabisha na hata kuelimisha sambamba na kuburudisha.

Yapo ya kutisha ambayo watu hupitia kiasi kwamba huwezi kuamini mpaka utakapo mpata mhusika akakusimulia. 

Visa na mikasa ni miongoni mwa vitu ambavyo watu wengi wanapenda kusikia. Unaweza kujikita katika tasnia hii na kuwatafuta watu wa aina hiyo.

Mfano wa channel zinazofanya vizuri katika upande huu ni pamoja na DAVISTA MATA MEDIA na BUNDUKI TV


15. UNBOXING

Unboxing ni kitendo cha kufungua bidhaa mpya. 

Tunafahamu kuwa kila siku kunatoka bidhaa mbali mbali mpya. Unaweza kuiwahi fursa hii na kuzama sokoni kuangalia kuna kitu gani kipya na ukakifikisha kwa raia kabla hawajapata maamuzi ya kukinunua.

Inaweza kuwa ni simu, kompyuta, tv na vingine vingi. Hii itapendeza zaidi kama utakuwa unawaeleza watu uimara wake na udhaifu wake ili wafahamu vema kabla ya kufanya maamuzi.

Leo wacha tuishie hapa ili nikupe nafasi ya kusubiri sehemu ya pili ambayo tutamalizia niches 11 zilizobaki.

Una maoni yoyote,  ushauri au maswali?

Shuka chini sehemu ya comment na utuandikie nasi tutayapitia.

COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: IDEA 26 BORA KWA WANAOTAKA KUANZISHA YOUTUBE CHANNEL - 1
IDEA 26 BORA KWA WANAOTAKA KUANZISHA YOUTUBE CHANNEL - 1
Wasiliana na Mwandishi wa Makala hii kwa namba - 0625 71 80 40
https://1.bp.blogspot.com/-iJYzd2vn7ak/YAk1AMhSu2I/AAAAAAAAbug/KTiePyETR1Y0zZmzaogdUQRJ_Wwfv8QigCLcBGAsYHQ/s0/niche.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-iJYzd2vn7ak/YAk1AMhSu2I/AAAAAAAAbug/KTiePyETR1Y0zZmzaogdUQRJ_Wwfv8QigCLcBGAsYHQ/s72-c/niche.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/01/idea-30-bora-niches-kwa-wanaotaka.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/01/idea-30-bora-niches-kwa-wanaotaka.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content