
Kwa jina jingine tunaweza kusema ni 'Makosa 10 wanayoyafanya youtubers (hasa) wachanga'
1. Kutowafahamu walengwa wako
Kwani unataka kurusha maudhui gani? Ukishajua maudhui ambayo unataka kuyarusha katika hiyo channel yako basi hapo moja kwa moja utajua kuwa watazamaji wako watakuwa ni watu wa aina gani hasa?
Hili ni jambo muhimu sana kwasababu kila rika la watu huwa na lugha zao na namna ya kuwafikishia ujumbe. Hivyo tunasema kuwa ni vizuri kuwafahamu walengwa wako kwanza.
Mfano unataka kujishughulisha na;- MAPISHI na UREMBO - Ujue wafuasi wako wengi watakuwa ni wanawake
MICHEZO na MAZOEZI - Hapo wafuasi wako watakuwa zaidi ni vijana
AFYA, LISHE, FAMILIA - Hapo wafuasi wako wengi zaidi watakuwa ni akina mama. Na kadhalika na kadhalika.
2. Kuweka kila kitu
Iko wazi kuwa huwezi kuwa mtaalamu wa kila fani. Hivyo katika nyanja ambazo utazizungumzia jitahidi kusimama katika point hizo.
Ukitaka kuleta kila kitu watu watakuchoka na hatimaye kukukimbia.
NB:-
Kama unataka kuongeza maudhui ni vema kuwapa taarifa watazamaji wako na kuhakikisha unakuwa na utaalamu wa jambo hilo jipya.
Hakuna ambaye anaweza kuwa bora katika kila jambo. Chagua kule ambako unahisi utafanya vizuri.
Soma
Password ambazo ni rahisi kudukuliwa
3. Audio mbaya
Uchunguzi unaonesha kuwa, mtu atakuwa tayari kutazama video mbaya lakini ambayo sauti inasikika vizuri lakini hayupo tayari kutazama video nzuri ambayo sauti yake haisikiki.
Hili utaniunga mkono kwa asilimia mia kwani yako baadhi ya maudhui watu husikiliza sauti tu bila video na hufurahia.
4. Kutokuwa na muendelezo
Watu wanapenda vitu endelevu. Hivyo kama umeanza jambo fulani ni bora ukaendelea nalo mpaka mwisho.
Usiwanyime watu haki yao kwa kuwakatisha utamu. Kumbuka kabla hukuwepo hawakukujua hivyo usiwafanye wajute kukufahamu.
5. Uongo
Hapa ndipo baadhi ya watu hufeli kwa kuona kuwa wanatengeneza kumbe wanaharibu. Utakuta anaandika kichwa cha habari chenye maudhui tofauti na habari yenyewe ili tu kuwavuta watazamaji.
MFANO;-
Kichwa cha habari kinasema "Ona jamaa alivoshindwa kutongoza demu" kisha unafungua video unakutana na audio au video ya msanii mchanga ambaye anaimba singeli😀
Ni kweli watu wata click kwa kudhani kuwa watapata watakacho lakini kiukweli baada ya hapo hawatorudi tena na watakutukana. Huenda hata wewe ni shahidi na umeshawahi kukutana na watu hawa.
Pale utakuwa umepata views lakini watu hawatoweza ku subscribe ili kuendelea kupata habari mpya kila utakaporusha.
JITAHIDI KUWA MKWELI KATIKA KAZI YAKO
6. Kupuuzia mitandao
Kuwa imara katika baadhi ya mitandao mikubwa ya kijamii. Kwani kuna wengine hawaifahamu channel yako ila wanakufahamu katika mitandao mingine ya kijamii. Hivyo ni vema kuwashirikisha ili wakufahamu.
Facebook, twitter na instagram ni mitandao maarufu na yenye watumiaji wengi sana. Itumie itakusaidia usiipuuze.
7. Kuiga
Kuiga hakukatazwi, ila unakatazwa kuiga kila kitu na kutaka uwe kama mtu fulani. Mfano katika staili ya uandishi wa vichwa vya habari, maelezo na hata picha (thumbnails)
Jitahidi uwe na utambulisho wako (identitity) ili watu wakujue wewe kama wewe.
Soma pia
8. Kutokuwa na playlist
Playlist ni list ambayo imewekwa ili kumsaidia mtu kupata maudhui ya aina moja sehemu moja. Kama unajihusisha na aidha MICHEZO, UDAKU, SIASA ni bora kila video unayopandisha uiweke katika playlist husika.
Hii humsaidia mtu anapoingia na kuamua kuangalia playlist fulani kutopata taabu.
'Weka playlist'

9. Kupumzika
Usijipe likizo. Watu hawataki likizo wanataka kazi. Kama umejiewekea utaratibu wa kupandisha video kila baada ya siku mbili, au kwa wiki mara mbili basi zingatia ratiba yako.
Usiwe mvivu kwani hauko peke yako. Watu wakikosa jambo kwako watakukimbia na kutafuta kwingine na hatimaye kutokurudi tena.
'Usijipe likizo'
10. Kujaza logo kwenye video
Unataka watu wakufahamu sawa hatukatai. lakini sio kujaza logo kuubwa katika kioo ama katikati ya picha. Hilo ni jambo ambalo watu wanakereka sana na wengine wanaweza kuondoka katika channel yako ikiwa jambo analolitazama halijamvutia.
Weka logo sehemu ndogo ya video kiasi kwamba isiwe kero kwa mtazamaji wako.
Yako makosa mengi ambayo watu wanaoanza kazi hizi huyafanya. Haya ni baadhi tu.
Jaribu kuyafanyia kazi kwa kuyaepuka ili sisi watazamaji wako tufurahie kazi zako.
Kwa maoni na ushauri tuandikie katika sehemu ya comment chini ya makala hii. Asante sana
Baba nimeona nimejifunza nimefunguka
ReplyDeletePamoja sana kiongozi wangu
Delete