Wasiliana na Mwandishi wa Makala hii kwa namba - 0625 71 80 40

Makala hii tumeiweka katika makala za Fafya kwa sababu nao ni ugonjwa na unahitaji tiba. Na mwisho wa makala hii tumekuwekea tiba sahihi ya tatizo hili.
Utakuta mtu akimkosea kidogo atapayuka na kukasirika kwa haraka na kwa muda mrefu mpaka umma ukashangaa. Wengine hata akiwepo mgeni hawana simile, inafikia kipindi wewe ndie unaona aibu kutokana na maneno makali yatokayo katika kinywa husika.
Ingawa yapo mambo ambayo husababisha hasira lakini viko vichochezi ama sababu ambazo zinaweza kusababisha hasira kwa kiwango kikubwa na kuwa kero.
Hizi hapa ni sababu 10 ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kuwa ni mwenye hasira sana kwa jamii yake.
Tazama jinsi ya ku comment kwenye blog yetu
1. HOMONI
Mzunguko wa homini za mwanamke kuna kipindi huwa na joto na hasira. Hasa kipindi ambacho anakuwa katika mzunguko wake wa siku za hedhi.
Hivyo kwa baadhi ya wanawake huwa na hasira kupita kiasi wakati huu, na siku za kawaida anakuwa mpole tu.
2. HAMU YA MAPENZI
Huenda ameolewa na mume yupo mbali, au hana mume wala mpenzi na imempelekea kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi. Hii ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo zinaweza kumpelekea mwanamke kuwa na hasira za mara kwa mara.
Nadhani nadharia hii ni maarufu sana katika jamii zetu na ina ukweli.
3. SELF CONDEMNATION (Kujihukumu)
Kujihukumu kwa makosa yaliyopita ni jambo baya sana. Ndio maana waswahili wakasema kuwa "Yaliyopita si ndwele"
Huenda mwanamke anajilaumu kutokana na kujiingiza katika hali fulani ambayo ilimuathiri hapo kipindi cha nyuma.
Hii hasira huwa anajilaumu yeye na hakulaumu wewe. Kikubwa ni kumuusia na kumkumbusha Maneno ya Mungu amabyo yatamliwaza.

4. DISSAPOINTMENT (Kukatishwa tamaa)
Kuna muda mwanamke anajiskia kukatishwa tamaa na watu wa karibu yake. Aweza kuwa mzazi, mume au ndugu mwingine ambaye hasapoti harakati za mapambano yake.
Hii inaweza kumletea hasira nyingi katika mambo mbali mbali.
5. PAST ABUSE (Mabaya yaliyopita)
Haya ni mambo mabaya ambayo yamewahi ku pitia katika maisha yake. Huenda aliwahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia, kijamii au kitu chochote kibaya ambacho kila akikikumbuka anapatwa na hasira kali.
Na kwa kuwa mtu anapopata jambo baya ni rahisi kukumbuka na mabaya yaliyopita hivyo kwa mwanamke yaweza kuwa ni sababu ya kuwa na jasira nyingi zaidi hata anapokwazwa kidogo.
6. KUYUMBA KIUCHUMI
Ukosefu wa uchumu na vitega uchumi waweza kuwa kikwazo kwa mwanamke. Huenda alishazoea kushia pesa ghafla zikaja zikamuondoka. Hii inaweza kuwa ni sababu kubwa ya kusababisha kuwa na hasira hata kwa watu ambao wasio na hatia.
Soma NJIA 10 NYEPESI ZA KUONDOSHA HASIRA
7. JEALOUS (Wivu/Husda)
Hasidi hana sababu
Hasa wivu ambao umeambatana na roho mbaya kwa mtu mwingine. Mwenzake ana kitu ambacho yeye hana na anakitamani. Hii inaweza kusababisha mwanamke mwenye wivu wa kupitiliza kuwa na hasira nyingi kwa kuona kuwa yeye ana haki zaidi kuliko yule mwenye nacho.
Mapenzi, maisha na mafanikio mengine ni vitu ambavyo wanawake huhusudiana sana baina yao.
Wapo wanawake ambao hawapendi wenzao kuwa na amani katika mahusiano yao. Basi yeye humnyima raha na kumfanya kuwa na hasira za ovyo.

8. STRESS ZA KAZI
Pengine mwanamke ni mtumishi sehemu fulani au amejiajiri. Anaweza kuchanganya machungu aliyokutana nayo kazini na kuyaleta nyumbani.
9. REJECTION (Kukataliwa)
Hakuna asiyejua maumivu ya kukataliwa na marafiki, ndugu au hata mpenzi. Hii kwa mwanamke ni mara mbili au zaidi. Hapa ndipo hasira huja na kuathiri hata wasiohusika.
Ufahamu UGONJWA WA KUPENDA KULALA SANA
10. ANXIENT (Hofu)
Wasi wasi wa kupata au kukosa jambo huweza kumfanya mtu kuwa mkali. Anatarajia kupata au kukosa kitu ni lazima mwanamke awe na hasira kwa kuwa akili yake inasimama katika jambo moja tu.
SILUHISHO
Kama una mwanamke ambaye ana tatizo la kuwa na hasira kupita kiasi huenda ana moja kati ya sababu hizi kumi.
Kama ni mtu wako wa karibu unatakiwa uielewe hali yake na kumpa moyo, ushauri, neno la dini na kuwa naye na subira.
COMMENTS