Basi nakukaribisha kuisoma makala hii na kupata ufumbuzi.
Leo hii ukiimuuliza mtu ambaye hapendi kusoma atakujibu moja kati ya majibu haya 9 ambayo nimeyaita ni visingizio.
Sasa kwa kulitambua hili tumeweka na njia za kupambana na visingizio hivyo.
1. SINA MUDA
"Sina muda wa kusoma" ni miongoni mwa majibu na visingizio vingi vya watu. Kuna mtu anaamini kuwa hana muda wa kushika kitabu kabisa katika ratiba ya siku yake. Hivi ni kweli?
Hapana bwana Sio kweli.
Ili uamini kama sio kweli, huyo anayesema kuwa hana muda wa kusoma muda mwingi utamkuta ameshika simu yake ya mkononi na kuperuzi.
Sasa kama wewe ni miongoni mwa ambao wanaamini kuwa hawana muda wa kusoma, fanya hivi - Badala ya kushika simu yako ya mkononi, shika kitabu na usome japo kurasa 4 kisha weka alama na uendelee na majukumu yako.
Hapo utakuwa umeongeza kitu katika ubongo wako. Kwani miongoni mwa faida za kusoma vitabu ni kuongeza uwezo wa ubongo ama akili yako.
Soma
2. VITABU NI GHALI SANA
Point hii ilitaka kufanana na ukweli, lakini kwa ulimwengu wa sasa vitabu hupatikana popote mtandaoni bure au kwa gharama nafuu karibu na bure.
Unaweza kuandika jina la kitabu upendacho na kukipata kwa ukamilifu wake
3. SIJUI NISOME NINI
Mwingine anaweza kujiuliza kuwa nisome nini sasa?
Nikweli inaweza kuwa hivyo. Kama ndivyo muulize mtu ambaye anapenda kusoma akuelekeze. Nenda maktaba muulize muhudumu, wauzaji wa vitabu ama pia waalimu na anaweza kukupa muongozo.
Lakini pia viko vitabu mbali mbali ambavyo vinapatikana bure kabisa katika mtandao wetu wa bongoclass.com
Bofya hapa chini
Bila shaka utafurahia na kupata faida kwa kuanza na vitabu hivyo.
4. KUSOMA KUNANIWEKA MACHO USIKU
Kwa baadhi ya watu ambao wamejikita sana na ni wapenzi wa kusoma wanaweza kujikuta usiku wanautumia kwa kusoma tu. Nukta hii mtu ambaye si mpenzi wa kusoma anaweza kuitumia kama kisingizio kuwa kusoma kunaweza kukamfanya awe macho sana usiku.
Msomaji anatakiwa kujua kuwa kila kitu ni ratiba. Kama akiziweka ratiba zake vema anaweza kusoma kabla au baada ya kulala badala ya kusoma usiku wa manane.
Lakini sambamba na hilo unaweza kuutumia usiku kwa kusoma ikiwa hutohofia juu ya shughuli zako siku ifuatayo au kama itakuwa ni siku ya mapumziko.
5. KUSOMA NI KUGUMU
Kusoma sio kugumu, ila unaweza ukajenga dhana kuwa kusoma ni kazi kubwa na ngumu. Kwanza uambie ubongo wako kuwa unasoma kwa ajili gani. Kisha uambie ubongo wako kuwa kusoma ni moja kati ya burudani zake.
Lakini anayesema kusoma ni kugumu huenda pia alikutana na maandiko ambayo yameandikwa bila kuzingatia kanuni na taratibu za uandishi hasa mitandaoni.
Hii ni kutokana na kukithiri kwa waandishi wengi wasio na taaluma hasa za uandishi wa MAKALA mbali mbali. Mtu anaweza kuwa na elimu ya jambo ambalo analiandika lakini asiwe na taaluma ya uandishi. Hii inaweza kuwafanya watu kutopenda kusoma.

Basi kama wewe ni mwandishi na umebahatika kusoma makala hii hujachelewa. Hapa nimekuwekea mbinu bora za uandishi wa makala.
Njia bora za uandishi wa makala - 1
Njia bora za uandishi wa makala - 2
7. SINA TABIA HIYO
Mwingine anaweza kujitoa katika kundi na kuona kuwa sio tabia yake wala sio haki yake kupenda kusoma. Kuna wakati anaweza akatamani kupenda kusoma lakini akaona kuwa tabia ya kusoma ni kwa watu fulani.
Fanya hivi
Anza kusoma kidogo kidogo, anza na vitabu vidogo vidogo ambavyo vinafurahisha stori zake. Baada ya muda itakuwa ni tabia yako na utajikuta nawe unapenda kama walivyo wengine.
8. NIKISOMA SIELEWI
Mwingine atakwambia kuwa akisoma huwa haelewi anachokisoma. Yaani anakwenda mbele huku anasahau alichokisoma.
Ni kweli inaweza kuwa hivi lakini dawa yake ni ndogo tu. Unatakiwa wakati unasoma (hasa unapoanza) uwe sehemu tulivu. Kwani vitabu vingi unapokianza unaweza usikielewe.
Sambamba na hilo pia unatakiwa usome kwanza maudhui ya kitabu kuwa kinahusiana na nini kabla ya kukianza. Lakini pia unatakiwa usome kiasi kidogo tu kisha kuendelea na mambo mengine. Mwisho wa siku utajikuta unaelewa.
9. NINA MATATIZO YA MACHO
Kweli kuna watu wana matatizo ya macho. Akisoma huwa anatoka machozi, macho kuuma, kupoteza uwezo wa kuona na kadhalika (Hili ni tatizo)
Kama ndivyo unashauriwa kumuona daktari wa macho kwa ushauri zaidi. Lakini pia kuzingatia ushauri wake kama vile kutumia miwani, kuweka kitabu chako au kifaa chako cha kusomea umbali unaotakiwa na kadhalika.
HITIMISHO
Visingizio vipo vingi lakini hivi ni baadhi ambavyo watu wengi huvihusisha na tabia za kutopenda kusoma vitabu. Lakini pia tumeeleza jinsi gani unaweza kuviepuka visingizio hivo.
Ni matumaini yetu kuwa pia umeipitia makala ya umuhimu wa kusoma vitabu ili kupata motisha zaidi na kujua unasoma kwa malengo gani.
Kwa maoni ushauri mapendekezo tuandikie hapo chini sehemu ya COMMENT.
Asante kwa kuwa nasi.
COMMENTS